Wabunge
wa Bunge la Kumi na Moja wamewachagua Wenyeviti wa tatu wa Bunge ambao
watasaidiana na Spika wa Bunge na Naibu Spika katika kuliongoza Bunge la
Kumi na Moja katika kipindi cha Nusu ya Uhai wake.
Waliochaguliwa
ni Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria Ndogo Mhe. Andrew Chenge (MB),
Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii Mhe. Dr Mary
Mwanjelwa (MB) na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria na Katiba
Mhe.Najma Giga (MB).
Akizungumza
kabla ya uchaguzi wa Wenyeviti hao Katibu wa Bunge Dkt Thomas
Kashililah alisema Kamati ya Uongozi iliwapitisha Wabunge watatu
kugombea nafasi hizo tatu za Uenyekiti wa Bunge.
Dkt
Kashililah alisema kwa kuwa Wagombea waliopitishwa ni watatu na kwa
kuwa nafasi zilikuwa tatu hivo Bunge lilikuwa na kazi ya kuwadhibitisha.
Hivyo
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai aliwaita Wagombea wote watatu kujinadi
mbele ya Bunge kabla ya kupigiwa kura ya pamoja ya Ndio au Hapana.
Ambapo
Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria Ndogo Mhe. Andrew Chenge (MB),
Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii Mhe. Dr Mary
Mwanjelwa (MB) na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria na Katiba
Mhe.Najma Giga (MB) walichaguliwa kwa kura nyingi za Ndio kuwa Wenyeviti
wa Bunge.