Alhamisi, 31 Desemba 2015

MAMBO MAKUBWA ALIYOWAHI KUYAFANYA MH MBUNGE DR MARY MWANJELWA KATIKA MIAKA MITANO ILIYOPITA

MBUNGE wa viti maalumu mkoa wa Mbeya (CCM), Dk.Mary Mwanjelwa akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Ileje,Mh. Aliko Kibona, wakati wa ziara yake ya kikazi wilayani humo, Mwaka 2011 ambapo alitoa msaada wa magodoro 60 kwa hospitali ya wilaya hiyo.
Dk. Mwanjelwa anamkabidhi rasmi msaada wa magodoro 70,Mkuu wa kitengo cha Wazazi Meta, Dk.Peter Msafiri.
Mbunge wa Viti Maalum wa mkoa wa Mbeya,Dk.Mary Mwanjelwa akimkabidhi msaada wa magodoro,Mganga Mkuu wa jiji la Mbeya, Dk.Samuel Razalo, kwa ajili ya kusaidia wodi ya Wazazi iliyopo kituo cha Afya Ruanda-Mwanjelwa, mjini Mbeya.

DR.MARY MWANJELWA MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA MBEYA AMBAYE PIA NI M-NEC TAIFA AKIWA ANAWASILI KATIKA OFISI YA AFISA MTENDAJI KATA YA MAJENGO MBEYA [​IMG]
DR.MARY MWANJELWA MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA MBEYA AMBAYE PIA NI M-NEC TAIFA AKISAINI KITABU CHA WAGENI KATIKA OFISI YA AFISA MTENDAJI KATA YA MAJENGO MBEYA
[​IMG]
DR.MARY MWANJELWA MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA MBEYA AMBAYE PIA NI M-NEC TAIFA AKIPATA MAELEZO YA KINA JUU YA UJENZI WA MSIKITI ULIOPO MAJENGO MBEYA KUTOKA KWA SHEHE HASSAN KUCHINJA

[​IMG]
DR.MARY MWANJELWA MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA MBEYA AMBAYE PIA NI M-NEC TAIFA AKISIKILIZA MAELEZO JUU YA MSIKITI HUO
[​IMG]
DR.MARY MWANJELWA MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA MBEYA AMBAYE PIA NI M-NEC TAIFA PAMOJA NA WANANCHI MBALIMBALI WAKIWA NDANI YA MSIKITI HUO
[​IMG]
[​IMG]
DR.MARY MWANJELWA MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA MBEYA AMBAYE PIA NI M-NEC TAIFA AKIWA NA VIONGOZI WA DINI CHAMA NA SERIKALI WAKIELEKEA KATIKA VIWANJA VYA SHULE MAJENGO KWA AJILI YA MKUTANO MFUPI PAMOJA NA KUKABIDHI MSAADA HUO KWA AJILI YA KUJENGA MSIKITI WA MAJENGO

[​IMG]


[​IMG]


[​IMG]


[​IMG]


WANANCHI MBALIMBALI WA KATA YA MAJENGO JIJINI MBEYA WAKIWA KATIKA MKUTANO MFUPI ULIO ANDALIWA KWA AJILI YA KUPOKEA MSAADA WA MABATI KWA AJILI YA UJENZI WA MSIKITI ULIOPO KATIKA KATA HIYO 


[​IMG]


[​IMG]
BAADHI YA VIONGOZI WA CHAMA ,SERIKALI NA WAZEE WAKIWA KATIKA MKUTANO HUO


[​IMG]
MUHESHIMIWA DIWANI WA KATA YA MAJENGO JIJINI MBEYASAMWEL MWAMBOMA (ALIYE SIMAMA) AKIMKARIBIASHA MGENI RASMI DR.MARY MWANJELWA MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA MBEYA AMBAYE PIA NI M-NEC TAIFA ILI AWEZE KUZUNGUMZA NA WANANCHI WA MAJENGO NA MAENEO YA JIRANI WALIOFIKA KATIKA MKUTANO HUO
[​IMG]
DR.MARY MWANJELWA MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA MBEYA AMBAYE PIA NI M-NEC TAIFA AKIWASALIMIA WANANCHI WA KATA YA MAJENGO 
[​IMG]
DR.MARY MWANJELWA MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA MBEYA AMBAYE PIA NI M-NEC TAIFA AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA KATA YA MAJENGO , PAMOJA NA HAYO ALIWAPONGEZA WAUMINI WA DINI YA KISLAM KWA HATUA WALIO ICHUKUA KUJENGA MSIKITI KATIKA ENEO HILO ILI NAO WAPATE KUWA NA NYUMBA YA IBADA, ALIWASHUKURU WATU MBALIMBALI KWA KUTOA MISAADA MBALIMBALI ILI KUKAMILISHA UJENZI WA NSUKITI HUO MAPEMA. PIA ALIWATAKA WANANCHI MBALIMBALI KUWA NA AMANI,MSHIKAMANO NA UPENDO


DR.MARY MWANJELWA MBUNGE ALIWATAKA AKINA MAMA, WAZEE WASTAAFU PAMOJA NA VIJANA KUUNDA VIKUNDI MBALIMBALI ILI KUWEZA KUJIKWAMUA NA KUONDOKANA NA UMASIKINI .
[​IMG]
DR.MARY MWANJELWA MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA MBEYA AMBAYE PIA NI M-NEC TAIFA AKIHIMIZA JAMBO WAKATI WA MKUTANO HUO



[​IMG]


[​IMG]
DR.MARY MWANJELWA MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA MBEYA AMBAYE PIA NI M-NEC TAIFA AKIKABIDHI MSAADA WA MABATI ISAHIRINI(20) KWA AJILI YA UJENZI WA MSIKITI WA MAJENGO
[​IMG]
DR.MARY MWANJELWA MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA MBEYA AMBAYE PIA NI M-NEC TAIFA AKIKABIDHI MIPIRA MIWILI KWA AJILI YA TIMU YA VIJANA ILIYOPO MAJENGO
[​IMG]
DR.MARY MWANJELWA MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA MBEYA AMBAYE PIA NI M-NEC TAIFA AKIWAPONGEZA VIJANA HAO KWA AJILI YA TIMU YAO




[​IMG]
DR.MARY MWANJELWA MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA MBEYA AMBAYE PIA NI M-NEC TAIFA AKIUNGANA NA WANANCHI WOTE KUFUNGA MKUTANO HUO KWA DUA
[​IMG]
WAZEE MBALIMBALI WAKIWA WANAMSHUKURU DR.MARY MWANJELWA MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA MBEYA AMBAYE PIA NI M-NEC TAIFA KWA KUFIKA KATIKA KATA YA MAJENGO JIJINI MBEYA, NA KUMSHUKURU KWA KUSIKILIZA BAADHI YA MAMBO YAO AMBAYO WALIYAZUNGUMZIA.

[​IMG]
DR.MARY MWANJELWA MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA MBEYA AMBAYE PIA NI M-NEC TAIFA AKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA VIONGONGOZI MBALIMBALI WA DINI, SERIKALI NA WANANCHI WA MAJENGO


UNAYAKUMBUKA HAYA YA USHINDI DR MARY MWANJELWA MWAKA 2015

Mbunge viti maalum mkoa wa mbeya Dr.Mary Mwanjelwa  alivunja rekodi
katika kura za maoni kutoka kwa wajumbe wa ccm mkoa wa mbeya na kupata
ridhaa ya kulejea tena katika kiti  cha ubunge viti maalum mkoa wa Mbeya
kwa ushindi wa kishindo wa asilimia 97 na kuwashinda wagombea kumi (10)
kati ya kumi na moja (11) walio kuwa wakigombea na kutaka kuteuliwa na
wajumbe wa ccm mkoa wa mbeya

Jumatano, 23 Desemba 2015

Rais Magufuli amemalizia kuwateua Mawaziri Wanne Waliokuwa Wamebaki


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemalizia kujaza nafasi za uteuzi wa Mawaziri na Naibu Waziri alizobakiza wakati akitangaza baraza la Mawaziri la kwanza katika awamu ya tano yautawala wake

Uteuzi huo ni kama ifuatavyo;
1.Profesa Jumanne Maghembe -Ameteuliwa kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii.

2.Dkt. Philip Mpango – Ameteuliwa kuwa Waziri wa Fedha na Mipango (Ni baada ya kumteua kuwa Mbunge).

3.Mhandisi Gerson Lwenge – Ameteuliwa kuwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji.

4.Dkt. Joyce Ndalichako – Ameteuliwa kuwa Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi.(Ni baada ya kumteua kuwa Mbunge)

5.Mheshimiwa Hamad Masauni – Ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi

6.Prof.Makame Mbarawa –Amehamishwa kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji na kwenda Wizara ya Ujenzi, uchukuzi na Mawasiliano

Katika hatua nyingine Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewatakia heri watanzania wote katika Sikukuu za Maulid, Christmas na Mwaka Mpya na kuwataka washerehekee kwa amani na utulivu.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
23 Desemba, 2015

Jumamosi, 12 Desemba 2015

Rais Magufuli Awaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri Ikulu Dar es Salaam




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Mhongo katika hafla fupi ya kuwaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri, leo katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii na Jinsia, wazee na watoto, Ummy Mwalimu katika hafla fupi ya kuwaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri , leo katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha waziri wa Katiba na Sheria, Harrison Mwakyembe katika hafla fupi ya kuwaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri, leo katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha Naibu waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.Ashantu Kijaji katika hafla fupi ya kuwaapisha Mawaziri, leo katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha  Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Lameck Nchemba katika hafla fupi ya kuwaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri, leo katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimwapisha waziri wa Sera, Bunge, Kazi ,Vijana,Ajira na Walemavu, Dkt. Abdallah Possi katika hafla fupi ya kuwaapisha Mawaziri, na manaibu Waziri leo katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.

Alhamisi, 10 Desemba 2015

SERIKALI: TUTALINDA HAKI ZA BINADAMU

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiingia katika ukumbi wa Karimjee wakati wa maadhimisho ya Haki za Binadamu Duniani yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akihutubia wadau mbalimbali hawapo pichani wakati wa maadhimisho ya Haki za Binadamu Duniani yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu akipeana mkono na  mhutimu wa Chuo Kikuu Mzumbe mara baada ya kutoa burudani fupi wakati wa maadhimisho ya Haki za Binadamu Duniani yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akipokea maandamano katika Ukumbi wa Karimjee yaliyofanywa na wadau mbalimbali wa Haki za Binadamu wakati wa maadhimisho hayo Duniani yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
Kikosi cha Bendi ya Askari magereza waliobeba bango lenye ujumbe wa siku ya maadhimisho ya haki za Binadamu Duniani wakiwa katika maandamano yaliyofanyika Jijini Dar es salaam.
Kikosi cha Bendi ya Askari magereza wakiongoza maandamano kwa ajili ya kuadhimisha siku ya haki za Binadamu Duniani yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
Wadau mbalimbali wakiwa katika maandamano kwa ajili ya kuadhimisha siku ya haki za Binadamu Duniani yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
Wananfunzi waliobeba mabango yakiwa na ujumbe mbalimbali unaosisitiza haki za Binadamu zizingatiwe wakiwa katika maandamano ya kuadhimisha siku ya Haki za Binadamu Duniani yaliyofanyika leo Jijini Dar es salaam.
Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa(UN) wakiwa na wadau mbalimbali katika maandamano ya kuadhimisha siku ya Haki za Binadamu  duniani yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
PICHA ZOTE NA ALLY DAUD - MAELEZO.

Na Shamimu Nyaki _Maelezo.
 SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesema itahakikisha Haki Za Binadamu zinalindwa na kuheshimiwa na kila mtu katika jamii anayotoka bila kujali itikadi yoyote ili kuleta usawa na uhuru katika jamii.

Akizungumza katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Haki za Binaadamu yaliyofanyika katika ukumbi wa Karimjee leo jijin Dar es Salaamu, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema atahakikisha anasimamia uhuru na haki kwa wananchi wote kwakuwa binaadamu wote ni sawa na wote wana haki sawa.

Mhe Samia ameongeza kuwa Serikali itahakikisha  inakomesha mauaji ya albino,ukatili wa kijinsia hasa kwa wanawake na wasichana, ndoa za utotoni,ukeketaji pamoja na mateso kwa mahabusu kwa vile wote ni Binadamu na wana Haki sawa.

Aidha amesema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizoridhia mikataba mbalimbali inayohusu Haki za Binadamu kama vile Mkataba wa kuondoa aina zote za ubaguzi wa mwaka 1965, Mkataba wa kuondoa Ubaguzi wa aina yoyote dhidi ya wanawake wa mwaka 1979 na Mkataba wa kimataifa wa haki za watoto wa mwaka 1989.

“Serikali yetu imekwisha ingiza baadhi ya mikataba hii katika sharia zetu za nchi,ama kwa kuunda sharia mpya au kurekebisha zile zilizopo”Alisema Mhe Samia.

Awali Mkurugenzi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bw Bahame Tom Nyanduga katika hotuba yake  amesema kuwa Tume ya Haki za Binaadamu imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutoa elimu kuhusu haki za binaamu kwa wananchi wote japokua kuna changamoto ndogo ndogo kwa maeneo ya vijijini na wanaendelea na jitihada za kuwafikia wananchi hao.

“Haki na Wajibu ni vitu vinavyoambatana hivyo watu wote washiriki. “Alisema Bw Bahame.
Ameongeza kuwa ni lazima Haki za Binaadamu zilindwe na kuheshimiwa ili kuleta maendeleo katika uchumi wa jamii kwa ujumla kwa kuwa bila  Uhuru na Haki watu watakosa elimu bora,maji safi,uhuru wa kupata habari,kwa kuzingatia kuwa binadamu wote wamezaliwa huru na ni sawa.

Maadhimisho hayo  ni ya 67 tangu yalipoanzishwa  na Azimio la  Ulimwengu la Haki za Binaadamu Mwaka 1948 yamehudhuriwa na watu mbalimbali kutoka Serikalini,Umoja wa Mataifa,Wadau wa Haki za Biadamu, na wanachi kwa  ujumla ambapo kauli mbiu inasema “Haki Zetu,Uhuru Wetu Daima”.

Hata hivyo Tume ya Haki za Binadamu imedhamiria kuleta maendeleo chanya kupitia Mpango wa Maendeleo endelevu utakaonza januari mwakani ambao umekuja na malengo kumi na saba ikiwemo elimu bora,afya bora, pamoja na kuondoa umaskini ili kufikia malengo ya Millenia.

BARAZA LA MAWAZIRI LATANGAZWA RASMI LEO NCHINI TANZANIA


RAIS wa Tanzania, Dkt. John Pombe MAGUFULI, ametangaza baadhi ya mawaziri wa serikali yake hii leo.

 

Amesema baraza lake litakuwa na mawaziri 19, ambapo baadhi ya wizara zitakuwa na mawaziri na hazitakuwa na manaibu waziri. Lengo ni kuwa na baraza dogo kupunguza gharama. 

   
Kuhusu semina elekezi kwa mawaziri hao, ameeleza kwamba, zilitengwa bilioni 2, lakini fedha hizo zitapelekwa ama kwenye madawati ama kuboresha (elimu bure).
 
 
"Wizara ni 18 lakini Mawaziri ni 19 kwa sababu wizara ya Ofisi ya Rais menejimenti ya Utumishi wa Umma naiunganisha na Utawala bora hivyo itakua na mawaziri wawili. Wizara ni kama ifuatavyo";




 
1. Ofisi ya Rais, Tamesemi utumishi na utawala bora, Mawaziri; Simbachawene na Kairuki, Naibu waziri Jaffo
 
2. Mazingira: January Makamba, naibu Makamba
 
3. Ajira, walemavu: Jenista Mhagama, Naibu nimemtua mbunge, Pos Abdallah ambae ni mhadhiri Dodoma
 
4. Ulemavu: Waziri ni Anthonu Mavunde
 
5. Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi : Waziri ni Mwigulu Lameck Nchemba na Naibu wake ni William Nash
 
6. Ujenzi, uchukuzi na mawasiliano: Waziri bado sijamtafuta, naendelea kumfikiria, Naibu waziri Ngonyani.
 
7. Fedha na mipango: Waziri bado, naibu Kijachi
 
8. Nishati na madini: Waziri ni Muhongo, Naibu bado
 
9. Katiba na sheria: Waziri Mwakyembe
 
10. Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki: Augustino Mahiga nimemteua mbunge na waziri, Naibu Dr Suzan
 
11. Ulinzi na kujenga taifa: Waaziri Dr. Hussein Mwinyi naibu bado
 
12. Ardhi na maendeleo ya makazi: Waziri ni Wiliam Lukuvi, Naibu Angelina Mabula
 
13. Utalii: Waziri bado
 
14. Viwanda na biashara: Waziri Charles Mwijage
 
15. Sayansi na ufundi: Waziri bado, Naibu ni Stella Manyanya
 
16. Afya na Ustawi wa jamii: Ummy Mwalimu, Naibu ni Kingwangala
 
17. Wizara yaHabari l,Utamaduni na Wasanii : Waziri ni Nape Nnauye,
 
18. Wizara ya maji na umwagiliaji: Waziri Makame Mbarawa, Naibu ni Kamwene

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...