Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiingia
katika ukumbi wa Karimjee wakati wa maadhimisho ya Haki za Binadamu
Duniani yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akihutubia
wadau mbalimbali hawapo pichani wakati wa maadhimisho ya Haki za
Binadamu Duniani yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu akipeana mkono
na mhutimu wa Chuo Kikuu Mzumbe mara baada ya kutoa burudani fupi
wakati wa maadhimisho ya Haki za Binadamu Duniani yaliyofanyika leo
jijini Dar es salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akipokea
maandamano katika Ukumbi wa Karimjee yaliyofanywa na wadau mbalimbali
wa Haki za Binadamu wakati wa maadhimisho hayo Duniani yaliyofanyika leo
jijini Dar es salaam.
Kikosi
cha Bendi ya Askari magereza waliobeba bango lenye ujumbe wa siku ya
maadhimisho ya haki za Binadamu Duniani wakiwa katika maandamano
yaliyofanyika Jijini Dar es salaam.
Kikosi cha
Bendi ya Askari magereza wakiongoza maandamano kwa ajili ya kuadhimisha
siku ya haki za Binadamu Duniani yaliyofanyika leo jijini Dar es
salaam.
Wadau
mbalimbali wakiwa katika maandamano kwa ajili ya kuadhimisha siku ya
haki za Binadamu Duniani yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
Wananfunzi
waliobeba mabango yakiwa na ujumbe mbalimbali unaosisitiza haki za
Binadamu zizingatiwe wakiwa katika maandamano ya kuadhimisha siku ya
Haki za Binadamu Duniani yaliyofanyika leo Jijini Dar es salaam.
Wafanyakazi
wa Umoja wa Mataifa(UN) wakiwa na wadau mbalimbali katika maandamano ya
kuadhimisha siku ya Haki za Binadamu duniani yaliyofanyika leo jijini
Dar es salaam.
PICHA ZOTE NA ALLY DAUD - MAELEZO.
Na Shamimu Nyaki _Maelezo.
SERIKALI
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesema itahakikisha Haki Za
Binadamu zinalindwa na kuheshimiwa na kila mtu katika jamii anayotoka
bila kujali itikadi yoyote ili kuleta usawa na uhuru katika jamii.
Akizungumza
katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Haki za Binaadamu
yaliyofanyika katika ukumbi wa Karimjee leo jijin Dar es Salaamu, Makamu
wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema atahakikisha anasimamia uhuru
na haki kwa wananchi wote kwakuwa binaadamu wote ni sawa na wote wana
haki sawa.
Mhe
Samia ameongeza kuwa Serikali itahakikisha inakomesha mauaji ya
albino,ukatili wa kijinsia hasa kwa wanawake na wasichana, ndoa za
utotoni,ukeketaji pamoja na mateso kwa mahabusu kwa vile wote ni
Binadamu na wana Haki sawa.
Aidha
amesema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizoridhia mikataba
mbalimbali inayohusu Haki za Binadamu kama vile Mkataba wa kuondoa aina
zote za ubaguzi wa mwaka 1965, Mkataba wa kuondoa Ubaguzi wa aina yoyote
dhidi ya wanawake wa mwaka 1979 na Mkataba wa kimataifa wa haki za
watoto wa mwaka 1989.
“Serikali
yetu imekwisha ingiza baadhi ya mikataba hii katika sharia zetu za
nchi,ama kwa kuunda sharia mpya au kurekebisha zile zilizopo”Alisema Mhe
Samia.
Awali
Mkurugenzi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bw Bahame Tom
Nyanduga katika hotuba yake amesema kuwa Tume ya Haki za Binaadamu
imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutoa elimu kuhusu haki za binaamu kwa
wananchi wote japokua kuna changamoto ndogo ndogo kwa maeneo ya vijijini
na wanaendelea na jitihada za kuwafikia wananchi hao.
“Haki na Wajibu ni vitu vinavyoambatana hivyo watu wote washiriki. “Alisema Bw Bahame.
Ameongeza
kuwa ni lazima Haki za Binaadamu zilindwe na kuheshimiwa ili kuleta
maendeleo katika uchumi wa jamii kwa ujumla kwa kuwa bila Uhuru na Haki
watu watakosa elimu bora,maji safi,uhuru wa kupata habari,kwa
kuzingatia kuwa binadamu wote wamezaliwa huru na ni sawa.
Maadhimisho
hayo ni ya 67 tangu yalipoanzishwa na Azimio la Ulimwengu la Haki za
Binaadamu Mwaka 1948 yamehudhuriwa na watu mbalimbali kutoka
Serikalini,Umoja wa Mataifa,Wadau wa Haki za Biadamu, na wanachi kwa
ujumla ambapo kauli mbiu inasema “Haki Zetu,Uhuru Wetu Daima”.
Hata
hivyo Tume ya Haki za Binadamu imedhamiria kuleta maendeleo chanya
kupitia Mpango wa Maendeleo endelevu utakaonza januari mwakani ambao
umekuja na malengo kumi na saba ikiwemo elimu bora,afya bora, pamoja na
kuondoa umaskini ili kufikia malengo ya Millenia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni