Jumatano, 23 Desemba 2015

Rais Magufuli amemalizia kuwateua Mawaziri Wanne Waliokuwa Wamebaki


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemalizia kujaza nafasi za uteuzi wa Mawaziri na Naibu Waziri alizobakiza wakati akitangaza baraza la Mawaziri la kwanza katika awamu ya tano yautawala wake

Uteuzi huo ni kama ifuatavyo;
1.Profesa Jumanne Maghembe -Ameteuliwa kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii.

2.Dkt. Philip Mpango – Ameteuliwa kuwa Waziri wa Fedha na Mipango (Ni baada ya kumteua kuwa Mbunge).

3.Mhandisi Gerson Lwenge – Ameteuliwa kuwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji.

4.Dkt. Joyce Ndalichako – Ameteuliwa kuwa Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi.(Ni baada ya kumteua kuwa Mbunge)

5.Mheshimiwa Hamad Masauni – Ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi

6.Prof.Makame Mbarawa –Amehamishwa kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji na kwenda Wizara ya Ujenzi, uchukuzi na Mawasiliano

Katika hatua nyingine Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewatakia heri watanzania wote katika Sikukuu za Maulid, Christmas na Mwaka Mpya na kuwataka washerehekee kwa amani na utulivu.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
23 Desemba, 2015

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...