Shule tano za mkoa wa Mwanza zafungwa baada ya Kipindupindu kuua watu Nane
Shule hizo ambazo ni za Buruza, Nabweko, Sambi na Kulazu, ambazo ni za msingi pamoja na shule ya Sekondari ya Irugwa, zimefungwa leo baada ya wanafunzi 22 wa shule za Msingi Nabweko kuambukizwa kipindupindu na watu wengine waliokuwa wanakusmbuliwa na ugonjwa huo.
Diwani wa kata hiyo ya Irugwa, Juma Msongi ameithibitishia FikraPevu kwamba tangu ugonjwa huo ulipolipuka wiki iliyopita katika baadhi ya maeneo ya Kata hiyo, watu 8 wamefariki na hali inazidi kuwa mbaya kutokana na kukosekana kwa huduma madhubuti.
Kwa mujibu wa diwani huyo, kutokana na hali ilivyo sasa wananchi wanatakiwa kuzingatia usafi wa mazingira ikiwemo matumizi sahihi ya kutumia vyoo na kujiepusha na ulaji ovyo wa vyakula.
FikraPevu inaendelea kufuatilia tukio hilo kwa karibu na kadri tutakapopata taarifa zaidi tutawataarifu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni