KATIKA
TUKIO LA KWANZA:
WATU
WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1.
ABILAH PHILIMON (17) MKAZI WA ILEMI,
DEREVA WA BAJAJI NA 2. BARAKA SELEMANI (23) MKAZI WA SIMIKE
WALIFARIKI DUNIA BAADA YA BAJAJI YENYE NAMBA ZA USAJILI MC 276 APL ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA MAREHEMU KUGONGA GARI T.588
AMR AINA YA MITSUBISHI FUSO ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA DEREVA EMANUEL FRANSIS (35).
AJALI
HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 21.09.2015
MAJIRA YA SAA 17:00 JIONI HUKO
KIJIJI CHA HATWELO, KATA YA HATWELO, TARAFA YA TEMBELA, WILAYA YA MBEYA
VIJIJINI, MKOA WA MBEYA.
AIDHA
KATIKA AJALI HIYO, WATU SITA KATI YAO WANAUME
WATANO NA MWANAMKE MMOJA
WALIJERUHIWA. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI WA BAJAJI. MIILI YA MAREHEMU
IMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA, MAJERUHI WAMELAZWA HOSPITALINI HAPO.
KATIKA
TUKIO LA PILI:
MTU
MMOJA MKAZI WA TEWELE – NAKONDE –ZAMBIA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA FRAID AINKALA (67) AFARIKI DUNIA BAADA YA BAJAJI YENYE NAMBA ZA USAJILI MC 630 AFC IKIENDESHWA NA DEREVA
ASIYEFAHAMIKA KUACHA NJIA NA KUPINDUKA.
AJALI
HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 21.09.2015
MAJIRA YA SAA 15:00 ALASIRI HUKO
KIJIJI CHA NKANGAMO, TARAFA YA NDALAMBO, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA, BARABARA
KUU YA TUNDUMA/SUMBAWANGA.
AIDHA
KATIKA AJALI HIYO, WATU WAWILI WALIJERUHIWA AMBAO NI 1. MAGRETH MTAMBO (52)
NA 2. ANASTAZIA NYAMUNGALA (55) WOTE WAKAZI WA KAKOZI –NAKONDE –
ZAMBIA. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI.
MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KITUO CHA AFYA TUNDUMA NA MAJERUHI WAMELAZWA
KITUONI HAPO.
KATIKA
TUKIO LA TATU:
MTU
MMOJA AMBAYE BADO KUFAHAMIKA JINA LAKE, TINGO WA BASI MALI YA KAMPUNI YA SAI
BABA AFARIKI DUNIA BAADA YA BASI HILO LENYE NAMBA ZA USAJILI T.668 BLD AINA YA SCANIA LILILOKUWA
LIKITOKEA DAR ES SALAAM KUELEKEA SUMBAWANGA KUGONGA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI
T.771 ATV/T.771 AUU SCANIA LORI
ILIYOKUWA IMEEGESHWA BAADA YA KUHARIBIKA ENEO LA MLIMA NYOKA.
AJALI
HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 21.09.2015
MAJIRA YA SAA 22:00 USIKU HUKO ENEO
LA MLIMA NYOKA, KATA YA NSALAGA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA KATIKA
BARABARA YA MBEYA/NJOMBE.
AIDHA
KATIKA AJALI HIYO, ABIRIA WAWILI AMBAO PIA MAJINA YAO BADO KUFAHAMIKA
WALIJERUHIWA NA WOTE WAMELAZWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. MWILI WA MAREHEMU
UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI WA BASI
HILO. DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA
TUKIO, JITIHADA ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA
SHERIA/MICHORO NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA
KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO DEREVA
WA BASI LA SAIBABA AZITOE ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI
YAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE.
Imesainiwa
na:
[AHMED
Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni