Alhamisi, 27 Agosti 2015

DKT. MAGUFULI; UKINUNUA MADARAKA IPO SIKU UTAWAUZA ULIOWANUNUA

 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuliakihutubia wakazi wa Mbalizi na kuendelea kusisitiza elimu itakuwa bure kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha nne,kuongeza maslahi ya walimu pamoja na jeshi la polisi.
 
Mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dr. John Pombe Magufuli amewaomba wananchi wa Mbalizi Jimbo la Mbeya Vijijini mkoani Mbeya, kummpa kura za ndiyo ili aweze kuongoza watanzania na kutatua matatizo mbalimbali yanayoikabili jamii ya watanzania wa hali ya chini.

Aliyasema hayo jana katika viwanja vya stendi Tarafani mjin hapo, na kwamba ametumikia nchi hii kwa miaka 20 serikalini akiwa Waziri na amekuwa mkweli na muwazi ndiyo maana ameweza kuisimamia vizuri kila wizara au jukumu alilopewa na wakubwa wake akiwatumikia Watanzania na sasa anaomba nafasi ya urais ili aweze kutekeleza vyema jukumu lake la kuwatumikia Watanzania .

Aliongeza kuwa ndiyo maana katika mchakato mzima wa kugombea urais ndani ya Chama cha Mapinduzi  alifanya kimya kimya na hakutumia fedha yoyote hivyo hakuna mtanzania yeyote anayemdai fedha ila anadaiwa utumishi uliotukuka wenye uaminifu, kujituma na kutetea maslahi ya watanzania na taifa kwa ujumla katika  taifa la Tanzania, Ameongeza kwamba ukitumia fedha kuingia madarakani na kununua madaraka ipo siku utawauza uliowanunua.
 
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuliakihutubia wakazi wa Mbalizi na kuendelea kusisitiza elimu itakuwa bure kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha nne,kuongeza maslahi ya walimu pamoja na jeshi la polisi.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuliakihutubia wakazi wa Mbalizi na kuendelea kusisitiza elimu itakuwa bure kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha nne,kuongeza maslahi ya walimu pamoja na jeshi la polisi.

Wananchi waliokusanyika kumsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Magufuli kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika stendi ya mabasi mjini Mbalizi wakishangilia huku wakipiga makelele kwamba anatosha na anafaa kuwa Rais na wameahidi kumpigia kura ya ndiyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...