MNAMO TAREHE 24.04.2015 MAJIRA YA SAA 09:30 ASUBUHI HUKO MAENEO YA MTAA
WA SOGEA KATIKA MJI MDOGO WA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA, VIJANA
WAWILI WALIOTAMBULIKA KWA MAJINA YA 1.
MATHEW ANGANILE MWAFONGO @ RASI (27)
MKAZI WA TUNDUMA NA MWENZAKE AITWAYE SALEHE
TABULEI SICHALWE (22) MKAZI WA
MAJENGO TUNDUMA WALIKAMATWA NA POLISI BAADA YA WANANCHI WA ENEO HILO KUWATILIA
MASHAKA KUWA NI WAHALIFU, HII NI KUTOKANA NA MVAO WAO AMBAO ULIKUWA UMEFICHA
SURA ZAO.
VIJANA HAO
WALIKUWA WAKITUMIA PIKIPIKI YENYE NAMBA ZA USAJILI
T.855 CDQ AINA YA T-BETTER NA WALIKUWA NA BEGI MOJA AMBALO MMOJA WA VIJANA
HAO ALIKUWA AMELIVAA MGONGONI.
POLISI
WALIPOWAPEKUA KATIKA BEGI HILO WALIKUTA VISU VIWILI, MANATI MBILI, MAWE
AROBAINI YA KURUSHWA KWA MANATI NA NATI NNE ZA KURUSHWA KWA MANATI, KOFIA MBILI
ZA JESHI, BUTI JOZI MBILI, MIWANI MIKUBWA INAYOTUMIWA NA POLISI KATIKA
MISAFARA, SHEEGUARD JOZI NNE (VIFAA MAALUM VYA KUVAA KWENYE MAGOTI NA VIWIKO
VYA MIKONO), MAKOTI MAWILI MAREFU, VIFAA VYA KUFANYIA MAZOEZI YA “PUSH UP” NA
KAMBA YA KUFANYIA MAZOEZI YA KURUKA.
AIDHA KATIKA
BEGI HILO KULIKUTWA PIA T-SHIRT MOJA YA CHADEMA, BENDERA MBILI NDOGO ZA CHADEMA,
KITAMBAA/KILEMBA KIMOJA NA BARUA TATU ZA KUWATAMBULISHA WATUHUMIWA KWENDA KUTOA
MAFUNZO KWA RED BRIGADE HUKO MAENEO YA KATA YA CHITETE, MSANGANO NA KAMSAMBA WILAYANI MOMBA.
KATIKA KUHOJIWA,
WATUHUMIWA HAO WALIKIRI KUWA WANAENDA KUTOA MAFUNZO KWA VIJANA WA RED BRIGADE
KATIKA KATA HIZO TAJWA HAPO JUU. KUTOKANA NA MATISHIO TULIYONAYO YA USALAMA NA
VIASHIRIA VYA UVUNJIFU WA AMANI NA UTULIVU NCHINI, WATUHUMIWA HAO WALIFIKISHWA
POLISI MKOA KWA MAHOJIANO ZAIDI NA BAADA YA UCHUNGUZI, JALADA LITAPELEKWA KWA
MWANASHERIA WA SERIKALI KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANAWASHUKURU WANANCHI
KWA KUCHUKUA TAHADHARI ZA KIUSALAMA KWA KUTOA TAARIFA HARAKA. AIDHA ANAENDELEA
KUTOA WITO KWA WANANCHI KUTOA TAARIFA HARAKA KATIKA VYOMBO VYA USALAMA PALE
WANAPOTILIA MASHAKA MTU/WATU AU VITENDO VYA MTU/WATU AU KIKUNDI CHA WATU ILI
HATUA STAHIKI ZICHUKULIWE HARAKA IWEZEKANAVYO.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.