KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MWENDESHA
PIKIPIKI ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA BONY
ALLY MWENYE UMRI KATI YA MIAKA 25-30
MKAZI WA NZOVWE JIJINI MBEYA ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA PIKIPIKI
ALIYOKUWA AKIENDESHA YENYE NAMBA ZA USAJILI MC 709 AFQ AINA YA KINGLION KUGONGANA NA GARI LENYE NAMBA ZA
USAJILI T.101 BFB AINA YA TOYOTA PRIMEO LILILOKUWA LIKIENDESHWA
NA DEREVA AITWAYE SETH MWAKYALABA (54) MKAZI WA MWAKIBETE.
TUKIO HILO
LIMETOKEA MNAMO TAREHE 19.04.2015
MAJIRA YA SAA 16:30 JIONI HUKO ENEO
LA MBEMBELA, KATA YA NZOVWE, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA KATIKA
BARABARA KUU YA MBEYA/TUNDUMA. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. DEREVA
AMEKAMATWA, GARI NA PIKIPIKI ZIPO KITUO CHA POLISI. MWILI WA MAREHEMU
UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA
SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
TAARIFA ZA MISAKO:
KATIKA
MSAKO WA KWANZA, JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WANNE
WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. FRANK
JOSEPH (24) MKAZI WA MWANJELWA 2.
BURTON MWAIPOPO (37) MKAZI WA SAE 3.
HARUNA JOSEPH (24) MKAZI WA MAJENGO NA 4.
BENEDICTOR DAUD (28) MKAZI WA ITIJI WAKIWA NA BHANGI MISOKOTO MITATU YENYE SAWA
NA UZITO WA GRAM 15.
WATUHUMIWA
WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 19.04.2015
MAJIRA YA SAA 11:00 ASUBUHI KATIKA
MSAKO ULIOFANYIKA HUKO ENEO LA STENDI KUU YA MABASI, KATA NA TARAFA YA SISIMBA,
JIJI NA MKOA MBEYA. TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KATIKA
MSAKO WA PILI, JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA
MKAZI WA KITONGOJI CHA MAPILI WILAYANI CHUNYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA NYAMIZI LUBHANGA (23) AKIWA NA NYARA ZA SERIKALI VIPANDE VINNE VYA MAGAMBA YA KAKAKUONA, MKIA WA NGIRI NA MAFUTA
YA SIMBA.
MTUHUMIWA
ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 19.04.2015
MAJIRA YA SAA 11:00 ASUBUHI KATIKA
MSAKO ULIOFANYIKA HUKO KITONGOJI CHA MAPILI, KIJIJI CHA BITIMANYANGA, KATA YA
MAFYEKO, TARAFA YA KIPEMBAWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA MBEYA.
KATIKA
MSAKO WA TATU, JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA
MKAZI WA HALUNGU – MGOMBANI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MICHAEL SHUGHULI (22) AKIWA NA BHANGI KETE TATU SAWA NA UZITO WA GRAM
15.
MTUHUMIWA
ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 19.04.2015
MAJIRA YA SAA 09:00 ASUBUHI KATIKA
MSAKO ULIOFANYIKA HUKO KIJIJI CHA MPONA, KATA YA TOTOWE, TARAFA YA SONGWE,
WILAYA YA CHUNYA, MKOA MBEYA. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MTUHUMIWA MAHAKAMANI
ZINAENDELEA.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII
KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA
AFYA YA MTUMIAJI.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni