Na
Adili Mhina.
Ofisi ya Rais, tume ya
mipango imepongezwa kwa hatua kubwa iliyopiga katika kutekeleza majukumu
mbalimbli ya kitaifa.
Pongezi hizo zimetolewa
na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo wakati akifungua mkutano wa Baraza
la Wafanyakazi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango lililofanyikia mjini Kibaha
mwishoni mwa juma.
Mheshimiwa Ndikilo
alieleza kuwa Tume ya mipango imepiga hatua kubwa katika kutekeleza majukumu
yake ambayo ni pamoja na kutayarisha mpango wa taifa wa kila mwaka, kusambaza
machapisho mbalimbali ya Tume ya Mipango, Kufuatilia utekelezaji wa miradi ya
maendeleo ya taifa, na kufanya mapitio ya utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa
miaka mitano (2011/12-2015/16).
Pamoja na mafanikio
makubwa katika kutekeleza majukumu ya Tume, Mkuu wa Mkoa alieleza kufurahishwa
kwake na ufanisi wa viongozi pamoja na watumishi wa Tume ya Mipango kwa kuandaa
mwongozo wa usimamizi wa uwekezaji wa umma, “ninaipongeza tume ya mipango kwa
kundaa mwongozo wa usimamizi wa uwekezaji wa umma (Public Investment Management
Manual), pamoja na kukamilisha tafiti mbalimbali zinazoharakisha mendeleo ya
uchumi wa nchi yetu na mahitaji ya kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Mendeleo
2025.”
Vilevile uongozi wa
Tume ya mipango umepongezwa kwa kuendelea kuwajengea uwezo watumishi wake wa
kada mbalimbali kwa kuwapeleka mfunzo ya muda mrefu na mfupi, semina na warsha
zinazofanyika ndani na nje ya nchi ili kuongeza ufanisi katika utendaji wa kazi
za kila siku.
Aidha Mheshimiwa Ndikilo
amesisitiza wajumbe wa baraza hilo kuwaelimisha watumishi wenzao juu ya umuhimu wa kila mfanyakazi kutimiza wajibu
wake katika sehemu ya kazi ili kufikia malengo ya pamoja baina ya mwajiri na
watumishi.
“Pamoja na mambo
mengine Baraza linawajibu wa kuishauri Tume kwa lengo la kuleta tija na
mshikamano baina ya mtumishi na mwajiri, si jambo la busara kwa watumishi
kutumia muda mwingi katika kudai maslahi zaidi kuliko kupima kiwango cha
utekelezaji wa wajibu wao,” alisisitiza mhandisi Ndikilo.
Awali, Kaimu Katibu
Mtendaji kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri ambaye
alikuwa Mwenyekiti wa Baraza hilo, alieleza kuwa katika mkutano huo wajumbe
watapata fursa kujadili mada nne amabazo ni mpango wa makisio ya mapato na
matumizi ya mwaka wa fedha 2015/16, Elimu ya jinsia mahala pa kazi, utekelezaji
wa sheria ya manunuzi ya umma ya mwaka 2011 na kanuni zake za mwaka 2013, na
haki na wajibu wa mwajiriwa mahala pa kazi. Lengo la mada hizo ni kutoa fursa
kwa watumishi kujifunza zaidi ili kuweza kuboresha utendaji wao wa kazi ili
kufikia lengo la Tume ya mipango la kukuza uchumi wa Taifa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni