JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA
YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI
LA POLISI TANZANIA.
R.P.C Ofisi
ya Kamanda wa Polisi,
Mkoa
wa Mbeya,
Namba
ya simu 2502572 S. L. P. 260,
Fax
-+255252503734 MBEYA.
E-mail:rpc.mbeya@tpf.com.tz
Unapojibu
tafadhali taja
MBR/C.5/900/VOL.I/251. Tarehe:
26 Agosti, 2014.
Inspekta
Jenerali wa Polisi,
Makao
Makuu ya Polisi,
S.L.P
9141,
DAR ES SALAAM.
YAH: TAARIFA YA ULINZI NA USALAMA KANDA NO 2 MKOA
WA MBEYA TAREHE 26.08.2014.
WA MBEYA TAREHE 26.08.2014.
Tafadhali
husika na kichwa cha habari tajwa hapo juu.
Pamoja
na barua hii ninakutumia taarifa ya hali ya ulinzi na usalama Kanda no 2 Mkoa
wa Mbeya ya masaa 24 yaliyopita kufikia tarehe 26.08.2014.
Naomba kuwasilisha tafadhali.
[Barakael Masaki – ACP].
Kny KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
Nakala kwa: Mkurugenzi wa Upelelezi
wa Makosa ya Jinai,
Makao
Makuu ya Upelelezi,
S.L.P 9093,
DAR ES SALAAM. -
Kwa
taarifa tafadhali.
Mkuu
wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai,
Mkoa wa Mbeya,
S.L.P 260,
MBEYA – Kwa
taarifa
[i]
MATUKIO YA UHALIFU/AJALI ZA USALAMA BARABARANI.
S/NO
|
Tarehe
|
Muda
|
Maelezo
ya Kosa / Tukio.
|
Watuhumiwa
|
01.
|
26.08.2014
|
03:30hrs
|
MB/IR/6898/2014
– AJALI YA MOTO.
Huko Iyunga, Kata na
Tarafa ya Iyunga, Jiji na Mkoa wa Mbeya. Mtu mmoja aitwaye DAVID S/O IMWMAMU, miaka 39, Mkurya, DSO
– Mbeya, Mkazi wa Iyunga aligundua kuungua kwa Nyumba aliyopanga
inayomilikiwa na RICHARD S/O YAONDE,
miaka 45, Mnyiha, Mfanyabiashara na Mkazi wa Sumbawanga yenye Vyumba Vitano
[05]. Moto huo uliteketeza vitu vyote vilivyokuwa sebuleni, stoo pamoja na
Master Bed Room na paa lote la Nyumba hiyo isipokuwa sehemu ndogo sana ya paa
hilo. Chanzo cha moto huo bado hakijafahamika. Moto huo ulizimwa kwa Jitihada
za Kikosi cha Zima moto na Uokoaji, Askari Polisi pamoja na Wananchi. Thamani
halisi ya mali iliyoteketea bado kufahamika. Hakuna madhara yoyote ya kibinadamu
yaliyoripotiwa. Kiongozi wa Zone namba 01 Kanda A amekagua tukio, Upelelezi
unaendelea.
|
---
|
[ii]
MATUKIO YATOKANAYO NA MAFANIKIO YA DORIA/MISAKO.
S/NO
|
Tarehe
|
Muda
|
Maelezo
ya Kosa / Tukio.
|
Watuhumiwa
|
01.
|
25.08.2014
|
16:30hrs
|
MB/IR/6880/2014
– KUPATIKANA NA BHANGI.
Huko Ilolo, Kata ya
Sinde, Tarafa ya Sisimba, Jiji na Mkoa wa Mbeya, Zone namba 05, Kanda A.
Askari Polisi wakiwa Doria/Msako waliwakamata 1. HANS S/O PIUS, miaka 27, Kyusa, Mkazi wa Ilolo 2. ZAWADI S/O ANDREW, miaka 22,
Msafwa na Mkazi wa Sinde B 3. KINGSLEY
S/O MWAMAJA, miaka 24, Kyusa, Mkulima na Mkazi wa Isanga na 4. SIKUJUA S/O ELIA, miaka 25, Kyusa,
Mkulima na Mkazi wa Sangu wakiwa na Bhangi Uzito wa Gramu 03 ndani ya Mfuko
wa kaki.
|
04
|
02.
|
25.08.2014
|
12:14hrs
|
MBO/IR/1261/2014
– KUPATIKANA NA RISASI ZA SMG NA SHORT GUN.
Huko katika Kitongoji
cha Ilembo “B” Mtaa wa Ilembo, Kata na Tarafa ya Vwawa, Wilaya ya Mbozi, Mkoa
wa Mbeya, Zone namba 06 Kanda B. Askari Polisi wakiwa Doria/Msako walimkamata
GABRIEL S/O MWAMPASHI, miaka 25,
Mnyiha, Mkazi wa Ilembo “B” akiwa na risasi 07 za Bunduki aina ya SMG na
risasi 01 ya Bunduki aina ya Short Gun nyumbani kwake wakati akiwa
anapekuliwa kutokana na kuhusika na makosa ya Uvunjaji.
|
01
|
03.
|
25.08.2014
|
15:30hrs
|
MKI/IR/961/2014
– KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO].
Huko katika Kitongoji
cha Mamba, Kata ya Mamba, Tarafa ya Kipembawe, Wilaya ya Chunya, Mkoa wa
Mbeya, Zone namba 23. Askari Polisi wakiwa Doria/Msako waliimkamata DAUDI S/O GABRIEL@ BUKUKU, miaka 32,
Kyusa, Mkulima na Mkazi wa Mamba “A” akiwa na Pombe Haramu ya Moshi [Gongo]
ujazo wa lita 07 Nyumbani kwake. Mtuhumiwa ni Muuzaji wa Pombe hiyo.
|
01
|
[iii]
MATUKIO YATOKANAYO NA UNYANYASAJI WA KIJINSIA.
S/NO
|
Tarehe
|
Muda
|
Maelezo
ya Kosa / Tukio.
|
Watuhumiwa
|
--
|
--
|
--
|
--
|
--
|
A:
Migogoro /Maafa- Hakuna.
Ø Kisiasa
– Umefanyika Mkutano wa Chama cha Siasa cha Chadema Huko katika Kata ya Itiji,
Tarafa ya Sisimba, Mkoa wa Mbeya. Katika Mkutano huo Mgeni Rasmi alikuwa ni
Mbunge wa Mbeya Mjini Mh.Joseph Mbilinyi ambaye alikuwa amefuatana na Viongozi
Waandamizi wa Chadema ngazi ya Mkoa na Wilaya. Agenda zilikuwa ni kufanya
tathmini juu ya ahadi zake kwa Wananchi zilizotolewa na Mbunge huyo. Katika
Mkutano huo Hapakuwa na Lugha za Matusi na Mkutano ulimalizika majira ya saa
18:20 jioni na wananchi kutawanyika kwa amani na utulivu.
Ø Wakulima
na Wafugaji – hakuna.
Ø Wakulima/Wananchi
na Wawekezaji – Hakuna
Ø Dini
– Hakuna.
B:
Idadi ya watendaji.
Ø Jumla
ya askari 1,458 waliingia kazini,
doria na malindo mbalimbali.
Ø Jumla
ya watumishi raia waliopo ni 17.
Ø Jumla
ya vikundi vya ulinzi jirani
vilivyopo Mkoa wa Mbeya 262,
jumla ya vikundi
vilivyoshiriki ni 101 na walinzi
394 walishiriki katika doria/malindo
mbalimbali.
Ø Jumla
ya askari Mgambo waliopo Mkoa wa Mbeya ni 2,253.
Ø Jumla
ya Polisi wasaidizi waliopo ni 420.
C: Mafanikio yaliyopatikana.
§ Mafanikio
yaliyopatikana kupitia doria,misako na operesheni ni kama ifuatavyo:-
v Bhangi
–
v Dawa
za kulevya {drugs} – Hakuna.
v Pombe
ya Moshi – Hakuna.
v Silaha
– Hakuna
v Nyara
za Serikali – Hakuna.
D: Ukamataji wa makosa ya Usalama Barabarani.
§ Jumla
ya makosa yaliyokamatwa –
262
§ Jumla
ya makosa yaliyolipa - 237
§ Jumla
ya magari yaliyokaguliwa kwa siku –
Hakuna.
§ Tozo
lililopatikana kutokana na ukaguzi wa magari – Hakuna.
§ Kesi
zilizopelekwa Mahakamani – Hakuna.
§ Jumla
ya Tozo [Notification] Tshs 7,110,000/=.
E: Watuhumiwa waliokamatwa kwa
makosa mbalimbali.
- Jumla ya watuhumiwa waliokamatwa ni 43.
- Jumla ya wahalifu wazoefu{harbitual} Mkoa wa Mbeya 139.
- Wahalifu wazoefu {Harbitual} – waliokamatwa – 05.
- Jumla ya wahalifu waangaliwa {Supervisee} Mkoa wa Mbeya 86.
- Wahalifu waangaliwa {Supervisee} – waliokamatwa – 03.
- Jumla ya kesi zilizofikishwa Mahakamani – 65.
- Kusomewa Mashitaka {fresh Cases} – 07.
- Jumla ya kesi zilizosikilizwa {Hg}– 50.
- Jumla ya kesi zilizotajwa {M}– 65.
- Kusomewa maelezo ya awali {Phg} – 26.
- Watuhumiwa waliofungwa {Convicted} – 04.
- Watuhumiwa waliachiliwa huru {Acquited} - Nil.
F:
HITIMISHO:
Kwa leo tarehe
26.08.2014 kumekuwa na idadi ya matukio “Hakuna” kama ifuatavyo:-
- Mauaji – Hakuna.
- Unyang’anyi wa Kutumia Silaha – Hakuna.
- Ajali ya Gari Kusababisha Vifo – Hakuna.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni