Shule waliyosoma Rais Joseph Kabila (wa DRC), Assah Mwambene yachakaa vibaya!
Shule hiyo inatwajwa kuongoza kutoa matokeo bora ya kitaaluma tangu kuanzishwa kwake, ambapo pia shule inatwajwa kuwa ndiyo waliyosoma viongozi maarufu Nchini Tanzania akiwemo Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Assa Mwambene na Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Uchunguzi uliofanywa na FikraPevu leo Agosti 19, 2014 mkoani humo umebaini kuwa licha ya viongozi hao kusoma shuleni hapo, ufaulu wa shule hiyo umeshuka kwa kiwango kikubwa tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
Makamu Mkuu wa shule hiyo, Aliko Mwanjala, amebainisha kuwa shule hiyo haina miundombinu ya kutosha licha ya kuwa na uhaba wa vifaa vya kufundishia huku akisema hali ya majengo ya shule hiyo kuwa sio rafiki.
Amesema awali shule hiyo ilikuwa ni shule ya mfano kitaaluma na kimalezi katika mkoa wa Mbeya na kuwa juhudi za kuinusuru na kuiinua kupitia kwa wadau mbalimbali wakiwemo wanafunzi waliowahi kusoma katika shule hiyo bado zinaendelea.
Mmoja wa watu waliowahi kusoma katika shule hiyo akiwemo Sambwee Shitambala, ambaye sasa ni Mwanasheria alikaririwa na FikraPevu akisema “Nitajitahidi kuwashirikisha wenzangu kuhusu hali hii naona majengo yamechakaa sana tofauti na tulivyokuwa tunasoma hapa kikiwemo jingo lenye chumba alichokuwa analala, Rais Kabila”.
Sehemu ya madarasa ya Shule ya Irambo
Chumba ambacho kilikuwa bweni ambalo,
Rais Joseph Kabila, wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), alikuwa
akikitumia kwa ajili ya kulala kwa sasa hili ni darasa la kidato cha
pili, aliyesimama ni mwandishi wa habari Gordon Kalulunga
CHANZO; FIKRA PEVU YA JF
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni