Jumatatu, 14 Julai 2014

MBUNGE VITI MAALUM MKOA WA MBEYA, DR. MARY MWANJELWA AFANYA ZIARA WILAYA ZA MKOA WA MBEYA, SASA YUPO MBEYA MJINI

 Mbunge viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa, akizindua tawi la VIJANA wakareketetwa wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), eneo la Kagera, kata ya Ilomba, Jijini Mbeya jana.

 Iyena iyena.......
 Risala kwa mgeni rasmi kutoka kwa vijana wa UVCCM tawi la Kagera Car wash. Mbunge Dr. Mary Mwanjelwa, aliwakabidhi wanawak wajasiliamali kiasi cha Tsh.100,000/= baada ya kusema kuwa wanao mfuko wao wa Tsh.300,000. Vijana waliahidiwa Jozi moja ya Jezi na kwamba waandike barua ili wasaidiwe mambo ya kuwakomboa kiujasiliamali ingawa walisema kuwa wanahitaji mashine ya kuoshea magari.
 Mbunge, Dr. Mary Mwanjelwa, hakutoka bure eneo la Kagera, alipewa zawadi ya chungu cha maua na kinyago.
 Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr.Mary Mwanjelwa, akihutubia wananchi na wanachama wa CCM eneo la Kagera Car wash Jijini Mbeya na baadae alitoa kadi kwa wanachama 19 ambao waliamua kujiunga na chama hicho jana.
 Hongera sana kwa kujinga na Chama Cha Mapinduzi, umechukua maamuzi sahihi.

 Chukua Laki moja hii iwasaidie kama chama hapa Kagera kwenye mradi wenu wa ujenzi kwa kiwanja mlichoniambia kuwa mnacho. Alisema na kukabidhi kiasi hicho cha fedha, Mbunge, Dr. Mary Mwanjelwa jana eneo la Kagera kata ya Ilomba Jijini Mbeya.
 Wasanii nao walipatiwa Tsh.50,000/= baada ya kuimba vizuri na kuomba kuendelzwa vipaji vyao.
 Mbunge Dr. Mary Mwanjelwa, akisikiliza risala katika tawi la Tonya, kata ya Ilomba alikofika kuzindua kijiwe cha vijana wakereketwa wa Chama Cha Mapinduzi,(CCM), ambao wanajishughulisha na usafirishaji wa abiria kutumia pikipiki (bodaboda).

 Hapa ni tawi la Itende, kata ya Itende pembezoni mwa Jiji la Mbeya, wilaya ya Mbeya Mjini, Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa, akicheza ngoma ya utamaduni wa wasafya, alipofika kukutana na wanawake wajasiliamali na viongozi wa CCM tawi hilo. Mbunge aliahidi kushirikiana nao kutatua kero ya daraja linalounganisha eneo la kata ya Itende na Iwambi na kupatikana kwa hati miliki ya jengo na eneo la CCM.

 Watoto hoyeeeeee...hoyeeeeee
 Akihutubia wananachi na wanachama wa CCM tawi la Itende.
 Mungu awabariki nimefurahi sana kwa kunipokea vizuri.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...