Jumuiya ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi( UVCCM) Mkoa wa Mbeya,
litafanya kikao chake cha Baraza la mkoa kesho, kwa mujibu wa kanuni za jumuiya
hiyo.
Baada
ya baraza hilo la mkoa, Jumuiya hiyo itafanya mkutano wa hadhara katika
viwanja vya Ruanda Nzovwe Jijini Mbeya, Julai 6, mwaka huu na
kuwaapisha makamanda wa wilaya zote tisa za mkoa huo, wakiongozwa na
kamanda wa mkoa, Yona Sonelo.
Mwenyekiti
wa Uvccm Mkoa wa Mbeya, Amani Kajuna, amejitokeza mbele ya waandishi wa habari, na kueleza kwamba, baraza hilo, litafanyika ofisi za CCM Mkoa wa Mbeya zilizopo sokomatola.
Amewaomba wananchi kujitokeza katika viwanja vya Ruanda Nzovwe, ili
kuwasikiliza vijana hao na kushuhudia tukio la uapishwaji wa makamanda hao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni