Jumatatu, 16 Juni 2014

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 16.06.2014.


Kamanda wa polisi mkoani Mbeya,Ahmed Msangi.


KATIKA TUKIO LA KWANZA:

MTU MMOJA MWANAUME ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE, MWENYE UMRI KATI YA MIAKA 35- 40 AMEFARIKI DUNIA BAADA YA GARI GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.974 CMC AINA YA CANTER LIKITOKEA MBEYA MJINI KUELEKEA MAKAMBAKO LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA AMBAYE BADO KUFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI KULIGONGA GARI T.777 AHF/T.107 BVB AINA YA SCANIA LILILOKUWA LIMEHARIBIKA NA KUEGESHWA PEMBENI YA BARABARA.

AJALI HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 15.06.2014 MAJIRA YA SAA 19:15 JIONI KATIKA KIJIJI NA KATA YA IMEZU, TARAFA YA TEMBELA, WILAYA YA KIPOLISI MBALIZI, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA KUU YA MBEYA/NJOMBE. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA, DEREVA ALIKIMBIA  NA KULITELEKEZA GARI  MARA ENEO LA TUKIO, JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.  MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO HASA KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE.

KATIKA TUKIO LA PILI:

MWANAFUNZI WA KIDATO CHA PILI KATIKA SHULE YA SEKONDARI SWAYA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA SIMON JULIUS (16) MKAZI WA IYELA AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA GARI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.745 NBA AINA YA CANTER LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA BARAKA ABDI (25) MKAZI WA IYELA KUPINDUKA.

AJALI HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 15.06.2014 MAJIRAYA SAA 14:00 MCHANA KATIKA ENEO LA MAKABURINI IYELA, KATA YA IYELA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. AIDHA KATIKA AJALI HIYO WATU WENGINE WANNE WALIPATA MAJERAHA KATI YAO WANAWAKE WATATU NA MWANAUME MMOJA WOTE WAMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. DEREVA AMEKAMATWA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO HASA KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.


KATIKA MISAKO:

MSAKO WA KWANZA:

MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKAKWA JINA LA ELIAS LUCAS (38) MKAZI WA KIJIJI CHA ITUMBI ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 25.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 15.06.2014 MAJIRA YA SAA 17:50 JIONI KATIKA KIJIJI CHA ITUMBI, KATA YA MATUNDASI, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA.



MSAKO WA PILI:

MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA BARAKA MWAMBUNGU (23) MKAZI WA KIJIJI CHA ITUMBI ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA BHANGI GRAM 500.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 15.06.2014 MAJIRA YA SAA 18:00 JIONI KATIKA KIJIJI CHA ITUMBI, KATA YA MATUNDASI, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] NA BHANGI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.


MSAKO WA TATU:

MTU MMOJA MKAZI WA NAKONDE NCHINI ZAMBIA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA JAMES SILUMBWE (28) ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NOTI BANDIA 02 ZA TSHS 10,000/= SAWA NA TSHS 20,000/= ZIKIWA NA NAMBA BU-7282385. 

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 15.06.2014 MAJIRA YA SAA 10:30 ASUBUHI KATIKA MTAA WA TUKUYU, KATA NA TARAFA YA TUNDUMA, MKOA WA MBEYA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUCHUKUA TAHADHARI NA MATAPELI PIA KUTOA TAARIFA ZA MTANDAO WA WATU WANAOJIHUSISHA NA UTENGENEZAJI WA NOTI BANDIA ILI WAKAMATWE.


MSAKO WA NNE:

MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA TIMOTH KAPALISYA (33) MKAZI WA KYELA  ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA BIDHAA ZILIZOPOGWA MARUFUKU NA SERIKALI.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 15.06.2014 MAJIRA YA SAA 15:00 ALASIRI KATIKA MTAA WA BENKI- MWANJELWA, KATA YA RUANDA, TARAFA YA SISIMBA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA ALIKAMATWA AKIWA NA POMBE KALI [VIROBA] AINA YA DOUBLE PUNCH ZIKIWA KWENYE MIFUKO MIKUBWA MITATU YA  SANDARUSI KILA MMOJA UKIWA NA UJAZO WA DEBE SITA [06] BAADA YA  KUINGIZWA NCHINI KUTOKA NCHINI MALAWI.

Imetolewa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...