MKUU WA MKOA WA MBEYA ABBAS KANDORO.
Kutokana na
mkoa wa Mbeya kuwa ni moja ya mikoa hapa nchini yenye milango ya kupitisha dawa
hizo na pombe zinazoitwa haramu(viroba), Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro,
alisema Mkoa wake umepata bahati ya kuwa mwenyeji wa maadhimisho ya siku ya kupiga
vita dawa za kulevya kitaifa.
Aliitaja
siku hiyo kuwa ni kesho kutwa June 26, mwaka huu na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa
Makamu wa Rais, Dr. Mohmed Gharib Bilal na shughuli zote zimeanza katika
viwanja vya Ruanda Nzovwe Jijini Mbeya tangu leo Juni 24, mwaka huu.
Alitaja
lengo la maadhimisho hayo kuwa ni kuiasa na kuikumbusha jamii juu ya athari za
utumiaji wa madawa ya kulevya na pia kuihamasisha jamii kuachana na matumizi ya
dawa hizo.
“Maonyesho
yatakuwa na lengo la kutoa elimu ya jinsi ya kuzuia uingiaji wa dawa hizo,
kupima waathirika na kutoa tiba kwa waathirika na taasisi zaidi ya 10
zitashiriki zikiwemo TFDA, Mkemia Mkuu wa serikali, Hospitali ya mkoa wa Mbeya,
Rufaa, Ofisi ya kamanda wa polisi na NGO’s’’ alisema Kandoro.
Sanjari na
hayo, alisema mkoa wa Mbeya unazalisha bangi, jambo ambalo serikali imeendelea
kupambana nalo kwa kushirikiana na serikali za mitaa na vijiji ili kufichua
wanaolima zao hilo.
*Tani 2.5
zanaswa
Wafanyabiashara
wakubwa wa dawa za kulevya nchini, wamekamatwa huku wengine wakiendelea
kusakwa.
Akieleza
mbele ya waandishi wa habari, mchambuzi mkuu wa tume ya kudhibiti dawa za
kulevya nchini, January Ntisi, alisema kuwa wafanyabiashara hao tayari
wamefikishwa kwenye vyombo vya sheria.
“Kwa muda wa
miezi sita tayari dawa za kulevya tani 2.5 zimekamatwa katika baadhi ya njia
kuu ikiwemo bahari ya Hindi, bandari ya Dar es Salaam na wanaendelea kukamatwa’’
alisema Ntisi.
Mbali na
jitihada hizo za serikali kudhibiti dawa hizo za kulevya hapa nchini, alisema
kuna kazi ngumu ya kupambana na vigogo hao ambao alikiri kuwa mtandao wao ni
mkubwa na wana uwezo wa kununua hata boti ziendazo kasi na manohari, lakini
vyombo vingi vinaendelea kushughulika nao.
Kiongozi
huyo, alilazimika kueleza jambo hilo baada ya kuulizwa kama tume yake
inashindwa kutokomeza tatizo hilo nchini ili kuendelea kulinda ajira zao
kwasababu wakitokomeza, kitengo hicho kinaweza kufutwa.
Ofisa kutoka
kitengo cha mkemia mkuu wa serikali, Grolia Omary, alisema ofisi yake inafanya
kazi kwa uadilifu mkubwa, hivyo tatizo la kwamba dawa zinabadilika kutokea
ofisi yake si kweli, bali wao wanapima wanachopelekewa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni