Ijumaa, 9 Mei 2014

WATOTO WAWILI WATEKETE KWA MOTO, BIBI WA MIAKA 69 AUAWA KWA KUKATWA NA KITU CHENYE NCHA KALI, MJUU WAKE ABAKWA NA KULAZWA!




KAMANDA WA POLISI WA MKOA WA MBEYA, AHMED MSANGI.
 
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
WATOTO WAWILI WALIOTAMBULIWA KWA MAJINA YA 1. BARAKA LACKSON (04) NA 2. ESTER LACKSON (02) NA MIEZI 10 WAMEFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA MOTO ILIYOTOKEA WILAYA YA MBEYA VIJIJINI BAADA YA NYUMBA WALIMOKUWA WAKIISHI KUUNGUA MOTO.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 08.05.2014 MAJIRA YA SAA 19:30 JIONI HUKO KATIKA MTAA WA MAGEUZI MJI MKONGWE, KATA YA  NSALAGA, TARAFA YA  UTENGULE USONGWE, WILAYA YA  MBEYA VIJIJINI , MKOA WA MBEYA. 

AIDHA MTOTO MARTIN KABWILILE (09) ALIJERUHIWA KWA KUUNGUA MOTO MIGUUNI   NA AMELAZWA KATIKA HOSPITALI TEULE YA IFISI. 

INADAIWA KUWA CHANZO CHA TUKIO NI MSHUMAA ULIOKUWA UMEWASHWA NA WAHANGA CHUMBANI  NA WAO KULALA. 

MOTO ULIZIMWA NA WANANCHI KWA KUSHIRIKIANA NA ASKARI POLISI. THAMANI HALISI YA MALI ILIYOTEKETEA BADO KUFAHAMIKA. 

MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA HOSPITALI YA IFISI. WAKATI WA TUKIO WAZAZI HAWAKUWEPO NYUMBANI.


KATIKA TUKIO LA PILI:
BIBI WA MIAKA 69 MKAZI WA KATABE WILAYA YA RUNGWE AITWAYE AIDA MWANGOSIM AMEUAWA KWA KUKATWA NA KITU CHENYE NCHA KALI KICHWANI NA USONI NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA AKIWA NYUMBANI KWAKE.


TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 08.05.2014 MAJIRA YA SAA 13:30 MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI CHA KATABE, KATA YA KYIMO, TARAFA YA UKUKWE   WILAYA YA RUNGWE   MKOA WA MBEYA. 

AIDHA KATIKA TUKIO HILO HAWA GEORGE (12) MWANAFUNZI  SHULE YA MSINGI KATABE DARASA LA PILI AMBAYE NI MJUKUU WA MAREHEMU ALIJERUHIWA KWA KUKATWA KITU CHENYE NCHA KALI KICHWANI KISHA KUBAKWA NA AMELAZWA HOSPITALI YA  MAKANDANA-TUKUYU.

CHANZO CHA TUKIO KINACHUNGUZWA, NDANI YA NYUMBA YA  MAREHEMU KUMEKUTWA SHOKA NA JIWE MOJA KUBWA AMBAVYO  VINADHANIWA KUTUMIKA KATIKA TUKIO HILO. UCHUNGUZI ZAIDI WA TUKIO HILI UNAENDELEA.


NB; Uongozi wa Mtandao huu, unalaani matukio ya namna hii ya kikatili na kuomba mamlaka zinazohusika kufanya jitihada za makusudi ili kuwabaini wahusika.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...