KATIKA TUKIO LA KWANZA:
KIJANA MMOJA
MKAZI WA KIJIJI CHA TOTOE WILAYANI CHUNYA MKOANI MBEYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA
LA DAUD CHARLES (20) ALIUAWA KWA
KUPIGWA NA KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI WAKITUMIA
SILAHA ZA JADI NA KISHA KUCHOMWA MOTO.
TUKIO HILO LIMETOKEA
MNAMO TAREHE 13.05.2015 MAJIRA YA SAA 05:40 ALFAJIRI HUKO KATIKA OFISI YA
SERIKALI YA KIJIJI CHA TOTOE, KATA YA TOTOE, TARAFA YA SONGWE, WILAYA YA
CHUNYA, MKOA WA MBEYA.
INADAIWA KUWA
CHANZO CHA TUKIO HILO NI TUHUMA ZA WIZI. UCHUNGUZI ZAIDI WA TUKIO HILI
UNAENDELEA IKIWA NI PAMOJA NA KUWABAINI WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI.
KAIMU KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI NYIGESA R. WANKYO ANATOA WITO KWA WANANCHI KUACHA TABIA YA
KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE WAJENGE
TABIA YA KUWAFIKISHA WATUHUMIWA WANAOWAKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI KATIKA
MAMLAKA HUSIKA KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.
TAARIFA ZA MISAKO:
JESHI LA POLISI
MKOANI MBEYA LINAWASHIKILIA WAHAMIAJI HARAMU WANNE WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. DANACHO WOLD (24) 2. NATABILA MARCOS (23) 3. KABOWO BURE (21)
NA 4. ATSON MASEBO (24) WOTE RAIA NA WAKAZI WA NCHINI ETHIOPIA WAKIWA
WAMEINGIA NCHINI BILA KIBALI.
WAHAMIAJI HAO
WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 13.05.2015
MAJIRA YA SAA 22:00 USIKU HUKO
KATIKA ENEO LA KYELA KATI, KATA YA KYELA, TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA YA KYELA,
MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZA KUWAKABIDHI IDARA YA UHAMIAJI KWA HATUA ZAIDI ZA
KISHERIA ZINAENDELEA.
KAIMU KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI NYIGESA R. WANKYO ANATOA WITO KWA WAGENI KUTII SHERIA BILA SHURUTI
KWA KUFUATA TARATIBU ZA KUINGIA NCHINI ILI KUEPUKA MADHARA YANAYOWEZA
KUEPUKIKA.
Imesainiwa na:
[NYIGESA R. WANKYO – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni