MBUNGE wa viti maalum mkoa wa Mbeya, Dkt. Mary Mwanjelwa(CCM), kesho kutwa Tarehe 23.02.2015. anataraji kuanza ziara ya kikazi katika Jimbo la Mbeya Vijijini.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari kutoka ofisi ya Mbunge huyo, imesema kuwa, pamoja na mambo mengine, atawawezesha vijana wapenda soka mipira.
Jumatatu, 23 Februari 2015
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 23.02.2015.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
WATU WATATU KATI
YAO MWANAUME MMOJA UMRI KATI YA MIAKA 45 – 50, MWANAMKE MMOJA UMRI KATI YA
MIAKA 65 – 70 NA MTOTO WA KIKE UMRI KATI YA MIAKA 10 – 12 WAMEFARIKI DUNIA
BAADA YA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.144
CGX/T.569 CKC AINA YA FAW TRACK LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA
ASIYEFAHAMIKA KUYAGONGA MAGARI MATATU AMBAYO NI T.158 BSJ AINA YA TOYOTA PICK-UP LIKIENDESHWA NA EMANUEL SHEDAFA (28) MKAZI WA
MWAKIBETE, GARI T.584 DRB AINA YA
TOYOTA HIACE LIKIENDESHWA NA DENIS
VICTOR (27) MKAZI WA NZOVWE NA GARI T.623
ADQ AINA YA TOYOTA HIACE LIKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA AMBALO
LILIPOTEZA UELEKEO NA KUTUMBUKIA MTONI NA KUSABABISHA VIFO.
AJALI HIYO
ILITOKEA MNAMO TAREHE 22.02.2015
MAJIRA YA SAA 16:45 JIONI HUKO ENEO
LA MLIMA MBALIZI, KATA YA SONGWE, TARAFA YA USONGWE, WILAYA YA MBEYA VIJIJINI,
MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA KUU YA MBEYA/TUNDUMA. AIDHA KATIKA AJALI HIYO WATU 14 WALIJERUHIWA KATI YAO 13 WAMELAZWA HOSPITALI TEULE YA IFISI
NA MMOJA AMELAZWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.
KATI YA MAJERUHI
HAO 04 NI WANAWAKE NA 10 NI WANAUME. CHANZO CHA AJALI BADO
HAKIJAFAHAMIKA. DEREVA WA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T. NA T.144 CGX/T.569 CKC AINA YA FAW TRACK ALIKIMBIA NA KULITELEKEZA
GARI ENEO LA TUKIO, JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
TAARIFA ZA MISAKO:
KATIKA
MSAKO WA KWANZA, JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WAHAMIAJI
HARAMU WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1.
SIFA BUKULU (35) NA 2. NYOTA
RAMADHANI (30) PAMOJA NA WATOTO WADOGO WATATU WOTE RAIA NA WAKAZI WA SANGE
NCHINI KONGO WAKIWA WAMEINGIA NCHINI BILA KIBALI.
WAHAMIAJI HAO
WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 22.02.2015
MAJIRA YA SAA 18:00 JIONI HUKO ENEO
LA MAJENGO, KATA NA TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA. TARATIBU
ZA KUWAFIKISHA IDARA YA UHAMIAJI KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA ZINAENDELEA.
KATIKA
MSAKO WA PILI, JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI
WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. AMANI
MBEGA (43) MKAZI WA MOSHI NA 2. HAKIMU
WATSON (40) MKAZI WA MAJENGO WAKIWA NA SILAHA BUNDUKI AINA YA SHOTGUN
ILIYOTENGENEZWA KIENYEJI NA RISASI MOJA.
WATUHUMIWA
WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 22.02.2015
MAJIRA YA SAA 22:00 USIKU HUKO
KATIKA KIJIJI CHA ITUMBA, TARAFA YA USONGWE, WILAYA YA KIPOLISI MBALIZI, MKOA
WA MBEYA BAADA YA KUFANYIKA MSAKO. SILAHA HIYO ILIKUWA IMEFICHWA KWENYE DARI LA
NYUMBA YAO.
KATIKA
MSAKO WA TATU, WATU WAWILI WOTE WAKAZI WA MPEMBA WALIOFAHAMIKA KWA
MAJINA YA 1. LUCAS KAYUNI (28) NA 2. MANENO KAYUNI (20) WANASHIKILIWA NA
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA WAKIWA NA MICHE 10 YA BHANGI IKIWA IMEPANDWA
KWENYE SHAMBA.
WATUHUMIWA
WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 22.02.2015
MAJIRA YA SAA 12:00 MCHANA HUKO
KATIKA KIJIJI CHA MPEMBA, KATA YA CHIWEZI, TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA,
MKOA WA MBEYA.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII
WANANCHI NA KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO DEREVA ALIKIMBIA AZITOE
KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
Imesainiwa
na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Jumapili, 1 Februari 2015
CHAMA CHA WALIMU TANZANIA MKOA WA MBEYA
Katibu wa chama cha Walimu Mkoa wa Mbeya (CWT) Kasuku Bilago akitoa taarifa ya Mkoa
TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
Ndugu Waandishi wa habari,
CWT mkoa wa Mbeya kinawasilisha hoja mbalimbali
za walimu kwa serikali yao kama ifuatavyo:-
1. MADAI YA WALIMU YA MUDA MREFU
Walimu wa mkoa wa Mbeya wana madai yao serikalini ambayo
yalihakikiwa Septemba 2013. Baada ya uhakiki huo uliofanyika nchi nzima kiasi
cha madai ya mkoa wa Mbeya yaliyokubaliwa na serikali yalikuwa kiasi cha zaidi
ya sh. 4.6 Bilioni. Serikali haijaonyesha nia thabiti ya kumaliza madai haya
kwa walimu wa mkoa wa Mbeya kwani walimu
bado wanaidai serikali kwa mchanganuo ufuatao:-
JUMLA
YA MADENI YA WALIMU MKOA WA MBEYA MPAKA DISEMBA 2014
|
|
WILAYA
|
KIASI
CHA DENI
|
MBEYA JIJI
|
1,220,620,843.00
|
MBEYA VIJIJINI
|
154,436,695.07
|
RUNGWE
|
220,000,000.00
|
KYELA
|
165,723,474.00
|
MBOZI/MOMBA
|
998,554,540.83
|
ILEJE
|
164,418,518.00
|
CHUNYA
|
463,871,400.24
|
MBARALI
|
230,666,235.66
|
JUMLA
KUU
|
3,618,291,706.80
|
Kwa hali hiyo CWT Mkoa wa Mbeya kinaitaka serikali kulipa
madai haya kabla au ifikapo tarehe 30/4/2015 ili kurudisha ari ya ufundishaji
kwa walimu. Kama serikali haitalipa madai haya Chama cha Walimu kitawaelekeza
walimu kuchukua maamuzi magumu kwa serikali mwaka huu wa 2015. Aidha, ieleweke
kuwa madai haya ni ya muda mrefu kuanzia 2007 hadi 2014 jambo ambalo CWT
hakiwezi kuvumilia kuendelea kuona serikali inavunja Sheria na Kanuni za
utumishi wa umma. Madai haya yalikubalika kwenye Kamati ya uhakiki.
Aidha, kuna baadhi ya watendaji wa serikali ambao wamekuwa na
upotoshaji mkubwa juu ya madai ya walimu kwamba yamelipwa yote au yamebaki
kidogo sana kama milioni 200 tu. CWT inasikitishwa sana na kauli kama hizo
kwani ni za uchochezi na kuwakatisha tamaa walimu. Mfano halisi ni madai
yaliyohakikiwa mkoa wa Mbeya ambayo hayajalipwa hadi sasa ni zaidi ya 3.6
Bilioni.
2. MALIPO YA LIKIZO KUTOLIPWA
Tangu Desemba 2013 serikali ilibadili utaratubu wa kulipa
walimu nauli za likizo kabla ya kwenda likizo zao. Hivyo, walimu wamekuwa
wakienda likizo bila kulipwa stahili zao. Likizo zifuatazo walimu hawajalipwa;
Desemba 2013, Juni 2014 na Desemba 2014 jambo linalokwenda kinyume na Kanuni za
Utumishi wa Umma, 2003; Kifungu cha 97 (5) kinachomtaka mwajiri kulipa nauli ya
likizo kwa kila mtum ishi wa umma mara moja katika kipindi cha miaka miwili.
3. KUTOPANDA KWA MADARAJA YA WALIMU KWA WAKATI
Kwa kawaida walimu wanatakiwa kupanda madaraja yao kila baada
ya miaka 3 kama hakuna tatizo la kiutumishi. Utaratibu huu umekiukwa na serikali
kwa madai ya ukomo wa bajeti (ceiling) jambo linaloathiri maslahi na haki ya
walimu ya kupanda daraja. CWT kinaitaka serikali kuwapandisha madaraja walimu
wote wa mkoa wa Mbeya waliofikia muda wa kupanda ili kuwapa motisha wa kuipenda
kazi yao.
4. KUUNGA MKONO TAMKO LA BARAZ LA CWT TAIFA
Chama cha Walimu Tanzania mkoa wa Mbeya kinapenda kuunga
mkono maazimio manne ya Baraza la CWT taifa lililofanyika mjini Morogoro katika
ukumbi wa Midland Hotel kuanzia tarehe 21-23 Januari, 2015. Maazimio haya yanataka
uwajibikaji wa dhati wa Serikali ikiwa ndio mwajiri Mkuu wa walimu wote wa
shule na Taasisi za Umma kama ifuatavyo:-
(i)
Utekelezaji
wa Waraka wa maendeleo ya utumishi Na.1 wa 2014 juu ya miundo ya utumishi wa
kada za ualimu chini ya WEMU Kumb. Na.AC.87/260/01/G/9.15/7 wa 2014 unaohusisha
miundo ya watumishi wa kada za walimu walio chini ya Wizara ya Elimu na Mafunzo
ya Ufundi uliopanua wigo wa ngazi za mishahara ya walimu na kuagiza utekelezaji
wake kuanza tarehe 01 Julai, 2014.
AZIMIO:
Walimu wote waliogota muda mrefu kwenye ngazi zilizofunguliwa
wapandishwe vyeo kuanzia tarehe 01 Julai, 2014 na kulipwa malimbikizo ya
mishahara hiyo kabla au ifikapo tarehe 30 Aprili, 2015.
(ii)
Walimu/Wanachama wa CWT wamekopwa na Serikali
stahili zao kwa muda mrefu. Hadi
mwishoni mwa Desemba, 2014 walimu wanaidai Serikali jumla ya T.sh 16 Bilioni.
Kwa mujibu wa uhakiki uliofanyika Desemba, 2013.
AZIMIO:
Baraza linaitaka Serikali kuwa imelipa madeni yote ya walimu
kabla au ifikapo tarehe 30 Aprili, 2015.
(iii)
Mamlaka
ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) ilibadili vikokotoo vya mafao kwa ajili ya wastaafu
bila kushirikisha wala kupata ridhaa ya wadau ambao ni wanachama wa Mifuko ya
Hifadhi husika wakiwemo walimu.
AZIMIO:
Kuitishwe mjadala wa wadau wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii,
wadau na SSRA kabla au ifikapo tarehe 30 Aprili, 2015 ili kutafuta ufumbuzi wa
suala hilo. Hiyo itakuwa ni kutekeleza
ahadi ya Mhe. Waziri Mkuu aliyoitoa
katika hotuba aliyoitoa katika Sherehe za Siku ya Mwalimu Duniani iliyofanyika
Mjini Bukoba-Kagera Kitaifa tarehe 5 Oktoba, 2014 juu ya kuliangalia upya suala
hilo.
(iv)
Madai
na kilio cha muda mrefu cha walimu tangu awamu ya tatu ya uongozi wa Taifa hili
ni kuwa na mwajiri mmoja- Chombo kimoja cha kushughulikia huduma zote za walimu
kuliko ilivyo leo ambapo walimu wanaajiriwa na kuhudumiwa na Wizara na Taasisi
zaidi ya nne. Sasa kilio hiki kifike
mwisho kwa kuwa hata Bunge la 16 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha
Azimio la kuanzishwa kwa chombo kimoja cha kuajiri walimu.
AZIMIO:
Baraza la Taifa lina tamka kuwa chombo kimoja cha ajira ya
walimu kiundwe na kuanza utekelezaji wake kabla au ifikapo tarehe 30 Aprili,
2015. Aidha mchakato wa Sheria ya kutaka
walimu waajiriwe na Mamlaka za Halmashauri za Wilaya uachwe mara moja kwani
hauna tija kwa walimu na Elimu ya nchi hii.
MWISHO:
CWT mkoa wa Mbeya kinaitaka serikali kuhakikisha kwamba
inawalipa madai walimu wote pamoja na kuwapandisha madaraja wanaostahili
sambamba na kulipa fedha za likizo zao. Endapo haya hayatatekelezwa kwa muda
mwafaka Chama kitawaelekeza
walimu/wanachama wake kuchukua maamuzi magumu juu ya serikali mwaka huu wa
2015.
Taarifa hii imetolewa na:
NELUSIGWE KAJUNI
MWENYEKITI CWT MKOA WA MBEYA
31/1/2015
RAIS KIKWETE AWASILISHA TAARIFA YA KAMATI YA VIONGOZI KUHUSU MABADILKIKO YA TABIA NCHI
Mwenyekiti wa Kamati ya Viongozi wa Afrika Juu ya mabadiliko ya Tabia nchi,Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasilisha ripoti ya utendaji wa kamati hiyo katika mkutano wa Viongozi wa Umoja wa Afrika uliofanyika jijini Addis Ababa Ethiopia.Mkutano huo ulimalizika jana
Mwenyekiti wa Kamati ya Viongozi wa Afrika Juu ya mabadiliko ya Tabia nchi(The Committee of African Heads of State and governments on Climate change) Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimakabidhi nakala ya Ripoti ya utendaji mwenyekiti mpya wa kamati hiyo Rais wa Misri Abdel Fattah el Sisi wakati wa Mkutano wa wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika uliofanyika Addis Ababa Ethiopia.Rais Kikwete alipongezwa kwa kuiwezesha kamati hiyo kupata mafanikio makubwa.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...