Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, amepokea msaada wa mashine 40 za kufyatulia tofali za kisasa, zenye
thamani ya Tsh.18,000,000,000/= kwa ajili ya
vikundi vya vijana kutoka halmashauri 10 za mkoa huo.
‘’Shirika lenu linafanya vizuri
sana, mnastahili pongezi,’’alisema.
Alisema
msaada huo umeongeza chachu
ya mahitaji ya nyumba bora kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kuongeza ajira kwa
vijana.
Meneja (NHC)mkoa wa Mbeya
Antony Komba alisema mashine hizo ni kati ya mashine nyingi zilizotolewa
na Shirika hilo kwa ajili ya kuwasaidia vijana kutokana na kuwepo kwa makazi
duni ya walio wengi nchini.
Awali, Shirika hilo, liliziomba halmashauri kuunda vikundi kwa kila halmashauri
iwe na vikundi vinne vyenye jumla ya watu kumi ambavyo vitachagua
viongozi na kufungua akaunti ya kikundi na baadaye watapatiwa mafunzo.
Shirika linatarajia kutoa Tsh. 500, 000/= kwa kila
kikundi ikiwa ni mtaji wa kuanzia shughuli hizo.
Halmashauri ni Chunya,Mbeya, Kyela, Rungwe, Ileje,
Mbarali,Mbozi,Mbeya mjini,Momba na Busokelo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni