Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa, Charles Kajege, akizungumza neno mbele ya viongozi waliokuwa wamehudhuria, wakiwemo wakuu wa wilaya zote za mkoa wa Mbeya.
Baadhi ya wenyeviti wa Halmashauri za mkoa wa Mbeya, wakisikiliza.
Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa, Charles Kajege.
Wakuu wa wilaya za Ileje na Kyela mkoani Mbeya, wakisikiliza na kufurahia...
Mkuu wa wilaya ya Rungwe, akifurahia jambo baada ya kutaniwa na Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, ambaye aliuwa mgeni rasmi.
Wakuu wa wilaya za Mbarali na Mbozi.
Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mbeya, Dr. Norman Sigalla.
Picha ya pamoja kati ya viongozi wa Bima ya Afya, Mkuu wa mkoa wa Mbeya na wakuu wa wilaya za Mbeya. Kisha zikafuata picha zingine za pamoja.
Meneja wa NHIF Mkoa wa Mbeya, Dr. Mohamed Kilolile(kushoto), wakiwa na Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro baada ya kufungua mkutano huo.
Baadhi ya waganga wakuu wa Hospitali za wilaya za mkoa wa Mbeya.
Meneja Matekelezo wa NHIF makao makuu, Grace Lobulu, ambaye alimwakilisha Naibu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, akitoa mada.
Afisa wa NHIF Mbeya.
Meneja wa NHIF Mkoa wa Mbeya, Dr. Mohamed Kilolile, akizungumza jambo katika mkutano wa CHF kwa viongozi wa mkoa wa Mbeya wakiwemo Wakuu wa wilaya za Mbeya, Wakurugenzi, waganga wakuu, Wenyeviti wa Halmashauri na wenyeviti wa bodi za afya za halmashauri, ulioandaliwa na Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa, (NHIF).
Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, akifungua mkutano wa CHF kwa viongozi wa mkoa wa Mbeya wakiwemo Wakuu wa wilaya za Mbeya, Wakurugenzi, waganga wakuu, Wenyeviti wa Halmashauri na wenyeviti wa bodi za afya za halmashauri, ulioandaliwa na Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa, (NHIF).
Mjumbe wa
Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa, Charles Kajege, alisema lengo la
mkutano huo na viongozi hao, ni kuhakikisha viongozi hasa wakuu wa wilaya
kupanga mipango ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma zkiwemo dawa kwa
wanachama wa CHF.
“Fedha zipo
nyingi kwenye mfuko wetu kwa ajili ya dawa na vifaa tiba, leteni maombi ya
mahitaji, tutawapeni ili wananchi wapate huduma’’ alisema Kajege.
Meneja
Matekelezo wa NHIF makao makuu, Grace Lobulu, ambaye alimwakilisha Naibu
Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, alisema kuwa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),
ulianza rasmi jukumu la kusimamia mfuko wa Afya ya Jamii(CHF), Kitaifa mwezi
Julai 2009.
Meneja wa
NHIF Mkoa wa Mbeya, Dr. Mohamed Kilolile, alizitaja sababu za kuanzishwa kwa
CHF kuwa ni Kushirikisha jamii kutoa mawazo yao ili kuboresha huduma za afya
kupitia mikutano na kamati mbalimbali watakazozichagua wao wenyewe.
“Kuiwezesha jamii
kumiliki hudum za Afya zinazowahusu katika maeneo wanayoishi na kuboresha
huduma za matibabu kupitia utaratibu rahisi na nafuu wa uchangiaji kwenye
mifuko ya bima ya jamii’’ alisema Dr. Kilolile.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni