| Sehemu ya kwanza kabisa kuiona unapopanda mlima Kilimanjaro ni misitu uliotokana na kupandwa kwa miti inayotumika kwa ajili ya utengenezaji wa Mbao. | 
|  | 
| Baadae unaicha hiyo misitu kisha unakutana na uoto wa asili wa miti mifupi . | 
| Kadri unavyo panda juu hali ya uoto inabadirika na hatimaye kukutana na nyasi fupi fupi iliyojishikiza kwenye miamba. | 
| Kwa watali wa ndan sasa wanaweza tumia barabra maalum kupanda na magari yao kwenda kujionea mandhari ya mlima Kilimanjaro ukiwemo uoto huo wa asili na miamba. | 
| Maua ya aina mbalimbali yanapendezesha maeneo hayo. | 
| Hali ya hewa katika maeneo hayo hubadilika kila baada ya dakika kadhaa,wakati mwingine mnaweza msionane. | 
| Wakati mwingine hali ni nzuri sana unatizama kila pembe ya mlima. | 
| Mawe yaliyotokana na kurushwa kwa uji uliotokana na Volcano. | 
| Maumbile mbalimbali ya vilima vilivyosalia kutokana na volcano hiyo. | 
| Hali ya hewa inabadilika pole pole kila eneo utakalo pita. | 
| Mabonde makubwa yaliyoambatana na mito kutoka katika miinuko ya mlima. | 
| Viwanja vya ndege aina ya Helcopter katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya uokoaji kwa watalii wanaopata matatizo. | 
Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii kanda ya kaskazini.

 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni