Wanakikundi cha Matumaini wakiwa na vifaa vya kilimo kwa ajili ya 
shamba lao lililopo katika kijiji cha Ikokoto, Wilayani Kilolo. Ni 
kijiji cha mwisho kuanza mlima kitonga.
Mmoja wa wanakikundi akilisha mifugo yake..
NA FRANK KIBIKI
Kikundi cha watu wanaoishi na VVU, cha matumaini kilichopo Ikokoto, 
Wilayani Kilolo kimepania kujikwamua kiuchumi, kutokana na shughuli zao 
za kilimo, ili kuondokana na ugumu wa maisha.
Wanachama wote wa kikundi hicho, wamekuwa wakijadili masuala yahusuyo 
afya zao, sambamba na namna ya kupata lishe bora ili waweze kuwasaidia 
watoto wao na familia zao.
Wenyewe, hawana wasi wasi na wanaufurahia umoja wao, kwani wawapo kazini
 hufanya kazi kwa bidii na wanaimani, kwamba hakuna maisha magumu ikiwa 
utaamua kupiga kazi....
Chanzo;mwitikio blog 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni