Jumatano, 23 Aprili 2014

MAFURIKO HUKO KYELA ENEO LA KAJUJUMELE YALIVYO LETA SHIDA, MH. MWAKYEMBE(MB) ATUA HUKO .

Mbunge wa Kyela Dr. Mwakyembe akikagua Barabara iendayo Bandari ya Kiwira Muda huu
 Baadhi ya watu wakigangaika kupita juu ya maji hayo yaliyotokana na Mafuriko.

 Baadhi ya watu mbalimbali wakiwa wanashuhudia Mafuriko hayo muda huu.
 Gari Likiwa limekwama katika tope lililotokana na Mafuriko hayo, hili ni eneo la Bujonde.
Picha kwa Hisani ya Kaka yetu mdau Mkubwa wa Mbeya yetu Blog Felix Mwakyembe.

Na Mbeya yetu

Jumatatu, 21 Aprili 2014

DC CHANG'A AFARIKI DUNIA

Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, mkoani Rukwa, Moshi Chang’a enzi za uhai wake akifafanua jambo. Picha na Maktaba 

Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, mkoani Rukwa, Moshi Chang’a amefariki dunia. Kiongozi huyo alifariki dunia jana saa 10: 15 jioni katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, alikokuwa amelazwa kwa zaidi ya siku 20.
Ofisa Habari wa hospitali hiyo, Aminieli Aligaesha alisema DC Chang’a alifika hospitalini hapo Machi 29, mwaka huu akiwa anaumwa na kulazwa.
Alisema madaktari wamekuwa wakimpatia matibabu, lakini ilipofika jana saa 9:30 alasiri hali yake ilibadilika ghafla.
“Walijitahidi kuokoa uhai wake bila mafanikio na ilipofika saa 10: 15 alikata roho, alisema Aligaesha huku akikataa kueleza tatizo lililokuwa linamsibu.
“Huyu ni kiongozi wa Serikali, bila shaka wakubwa huko serikalini wataeleza zaidi kuhusu kifo hicho,” alisema.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Hawa Ghasia alithibitisha kutokea kwa kifo hicho mchana wa jana, baada ya kiongozi huyo kusumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu.
Alisema amemwagiza katibu wake (wa waziri) na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Stella Manyanya kufuatilia na kushughulikia msiba huo na taarifa zaidi kuhusu utaratibu zitapatikana leo baada ya kuzungumza na familia.
Chang’a kabla ya kuhamishiwa katika Wilaya ya Kalambo alikuwa DC wa Wilaya Mpya ya Mkalama.

GAZETI ZA KIKRISTO TANZANIA JUMAPILI APRIL 20,2014

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

ASKARI AKAMATWA KWA TUHUMA ZA KUIBA MTOTO WA UMRI WA SIKU SABA

ASKARI wa Jeshi la Polisi aliyefahamika kwa jina la Prisca Kilwai mwenye namba WP 5367 wa Ilala Jijini Dar es Salaam amekamatwa kwa tuhuma za wizi wa mtoto  
Baba Mzazi  wa mtoto aliyeibiwa  Salehe Issah Mwangosi(31) ndiye alieshirikiana na polisi huyo kumwiba mtoto

 Mboka Mwakikagile(20) mama mzazi wa mtoto aliyeibwa



ASKARI wa Jeshi la Polisi aliyefahamika kwa jina la Prisca Kilwai mwenye namba WP 5367 wa Ilala Jijini Dar es Salaam amekamatwa kwa tuhuma za wizi wa mtoto jinsi ya kiume aliyefahamika kwa jina la Goodluck Salehe(siku 7) aliyeibwa April 6 mwaka huu huko Kasumulu Kata ya Itope Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya.

Mtoto alizaliwa Machi 30 na alipoibiwa alikuwa na umri wa siku sita ambapo mtuhumiwa alishirikiana na Baba Mzazi aliyefahamika kwa jina la Salehe Issah Mwangosi(31) mkazi wa Matankini Kyela aliyemtambulisha kwa mama mzazi aliyefahamika kwa jina la Mboka Mwakikagile(20) kuwa Prisca ni shangazi yake Salehe hivyo anakuja kumwona mtoto aliyezaliwa.

Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ahmed Msangi amethibitisha kukamatwa kwa Askari huyo ambapo amesema kuwa ikithibitika kutenda kosa hilo atafikishwa mahakama ya kijeshi na baada ya taratibu hizo kukamilika atafikishwa Mahakamani ili kujibu tuhuma zinazo mkabili.

Mtuhumiwa amekamatwa April 17 mwaka huu huko eneo la Meta Jijini Mbeya majira ya saa nne asubuhi akiwa na mtoto huyo mkononi ambapo alitiwa nguvuni na kufikishwa makao makuu ya Polisi Mkoa Forest ya Zamani kwa mahojiano zaidi.

Msangi amesema kuwa Salehe na Prisca hawana mahusiano ya Damu ila wana mahusiano ya kibiashara ambapo wanaendelea kufanya uchunguzi wa tukio hilo na upelelezi ukikamilika watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazo wakabili.
 
 

MTOTO ALIYEIBWA AKABIDHIWA KWA WAZAZI

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi akimkabidhi kwa mama yake mzazi mtoto Goodluck mara baada ya kupatikana

Akipokea Mtoto wake Mama mzazi Mboka Mwakikagile(20) amelishukuru Jeshi la polisi na wananchi wema kwa kufanikisha kupatikana kwa mtoto wake  Goodluck Salehe aliyeibwa na Askari wa Jeshi la Polisi WP 5367 Prisca Kilwai April 6, mwaka huu huko Kasumulu wilayani Kyela.


 Mtoto  Goodluck Salehe 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi,akizungumza baada ya kukabidhi mtoto huyo aliwasihi wazazi kuwa makini na utunzaji wa watoto ili kuepuka vitendo kama hivyo kujirudia.





Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi akizungumza na shangazi wa mtoto aliyeibiwa pembeni ni baadhi ya waandishi wa habari walioshuhudia makabidhiano hayo




BAADA ya Jeshi la Polisi mkoani Mbeya  kumtia nguvuni Askari wake anayetuhumiwa kuiba mtoto wilayani Kyela,Mtoto huyo akabidhiwa kwa wazazi wake huku wakiendelea na uchunguzi zaidi.
Makabidhiano hayo yamefanyika   katika Hospitali ya Wazazi Meta alikokuwa akipatiwa matibabu mtoto huyo katika chumba cha Joto na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi.
Akipokea Mtoto wake Mama mzazi Mboka Mwakikagile(20) amelishukuru Jeshi la polisi na wananchi wema kwa kufanikisha kupatikana kwa mtoto wake  Goodluck Salehe aliyeibwa na Askari wa Jeshi la Polisi WP 5367 Prisca Kilwai April 6, mwaka huu huko Kasumulu wilayani Kyela.
Aidha mwanamke huyo amemshukuru zaidi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi pamoja na Askari wengine  waliofanikisha mtoto wake kupatikana akiwa hai.
Baadhi ya ndugu waliofurika katika Hospitali ya Meta kushuhudia makabidhiano hayo wamesema hawaamini  kile kilichotokea baada ya kuwa katika hofu takribani siku kumi na moja baada ya kuibwa katika zahanati ya Njisi iliyopo Kasumulu Kyela.
Aidha ndugu hao wamelipongeza Jeshi la Polisi kwa kufanikisha kupatikana mtoto na wasamaria wote walioshirikiana nao katika maombi hata kufanikisha upatikanaji wa mtoto huyo akiwa salama salimini.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi,akizungumza baada ya kukabidhi mtoto huyo aliwasihi wazazi kuwa makini na utunzaji wa watoto ili kuepuka vitendo kama hivyo kujirudia.
Ameongeza kuwa Jeshi la polisi bado linafanya upelelezi na kukusanya ushahidi zaidi ili waweze kuwafikisha mahakamani watumiwa kujibu mashtaka wanayokabiliana nayo.
Amesema Mtoto huyo alipatikana Aprili 17, mwaka huu akiwa na Askari huyo majira ya saa nne asubuhi  na kuongeza kuwa mpaka sasa sababu za kuiba mtoto huyo hazijafahamika na atafikishwa mahakamani wakati wowote baada ya kuhukumiwa kijeshi.

Na Mbeya yetu

Jumanne, 15 Aprili 2014

KUHUSU HATI YA MUUNGANO, IKULU YA DAR ES SALAAM YALONGA



THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
              P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAMKO LA KATIBU MKUU KIONGOZI KWA VYOMBO VYA HABARI
KUHUSU HATI YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR
IKULU, DAR ES SALAAM, TAREHE 14 APRILI, 2014
__________________________________________________

            Siku 12 zijazo tutasherehekea miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, na kuzaliwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wamezaliwa watu ndani ya Muungano huu na wengine wana wajukuu.

            Inasikitisha sana kuwa leo, miaka 50 baadaye ipo dhana potofu inayojengwa kuwa Muungano huu si halali kwa vile hakuna Hati ya Muungano (Articles of the Union).

            Waasisi wa Taifa letu ambao tarehe 22 Aprili, 1964 kule Zanzibar walitia saini Hati hiyo, mbele ya mashuhuda, nao wameonekana kama walichokifanya kilikuwa kiini macho, na kwa hiyo kwamba waliongoza Taifa jipya la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa msingi wa kiini macho hicho kwa miaka yote hadi Mwenyezi Mungu alipowaita.

            Mambo yote mawili yametusononesha sana sisi Serikalini, na bila shaka yamewasononesha wananchi wanaoipenda nchi yao, wanaowapenda Waasisi wa Taifa letu na kuuenzi Muungano wao.

            Madai ya kuonyeshwa Hati ya Muungano yalianza siku nyingi lakini hatukuweza kuamini hali itafikiwa ilipofikia, ambapo wapo watu wanathubutu kudai na kuapa kuwa Hati hiyo haipo.

            Ukweli ni kuwa hati hiyo ipo, ilikuwepo siku zote. Hata hivyo, lazima tukubaliane kuwa zipo Hati fulani ambazo ni kiini cha uwepo wetu kama Taifa huru, Jamhuri huru na Muungano huru, ambazo tunazihifadhi kama mboni ya jicho. Hati hizo ni pamoja na Hati ya Uhuru wa Tanganyika ya mwaka 1961, Hati ya Tanganyika kuwa Jamhuri mwaka 1962, na Hati ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ya mwaka 1964. Hati za aina hii zinahifadhiwa maeneo maalum ambayo ni salama ili zisipotee wala kuharibika. Kwa kawaida hatuzitoi, tunazifungua ili kuzihifadhi kwa namna yoyote ile.

            Lakini sasa maneno yanakua mengi, tuhuma zimekuwa nyingi, dhihaka zimekuwa nyingi, kiasi cha wananchi kuanza kutiwa mashaka iwapo kweli Hati ya Muungano ipo au la.

            Hivyo, kwa maagizo na ridhaa ya Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ninaleta mbele yenu Hati ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar iliyotiwa saini Zanzibar na waasisi wetu, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mzee Abeid Aman Karume, ili muione na kuwahakikishia Watanzania kuwa yanayosemwa kuwa hakuna Hati hiyo si kweli. Hati hiyo ipo tangu wakati huo, imetunzwa vizuri na waliotutangulia, tumeirithi, na tutaendelea kuihifadhi.

            Na, tukiombwa kufanya hivyo na Mwenyekiti wa Bunge Maalum nina uhakika Rais ataridhia ipelekwe huko ili kuondoa mjadala wa kama Hati ipo au la.

            Isitoshe, tufanye utaratibu wa kuweka nakala kwenye Makumbusho ya Taifa ili kila atakayetaka kuiona katika miaka mingine 50 ijayo na kuzidi aione.

            Mwisho, narejea kusema kuwa kwa upande wa Serikali tunasikitishwa na kufadhaishwa sana na tuhuma nzito kwamba labda waasisi wetu hawakuwa makini au walitufanyia kiini macho. Hatukutarajia wawepo Watanzania wenzetu, wafikie hapo.

            Ni jambo zito. Vile vile hatukutarajia kuwa Serikali itatuhumiwa kuwa haikuwa makini kuhifadhi waliosaini waasisi wetu.

            Matumaini yetu ni kuwa baada ya leo tutaendelea na mambo ya msingi kwa mustakabali, umoja na uimara wa Taifa letu badala ya kuchochea hisia kuwa Muungano wetu hauna msingi imara wa kisheria.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
14 Aprili, 2014

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 15.04.2014.




KATIKA TUKIO LA KWANZA:

MTU MMOJA AITWAE MSUKUMA PENGO [48] MKAZI WA MTAA WA MWAMBENE ALIFARIKI DUNIA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA JIJINI MBEYA TAREHE 14.04.2014 MAJIRA YA SAA 06:00 ASUBUHI WAKATI ANAENDELEA KUPATIWA MATIBABU HOSPITALINI HAPO.

MAREHEMU ALISHAMBULIWA  KWA KUPIGWA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI WAKITUMIA SILAHA ZA JADI FIMBO, MAWE, MATOFALI NA MARUNGU TAREHE 13.04.2014 MAJIRA YA  SAA 20:00 USIKU  HUKO KATIKA MSIKITI WA SAE, KATA YA  ILOMBA, TARAFA YA  IYUNGA. INADAIWA CHANZO CHA TUKIO HILO NI TUHUMA ZA WIZI WA BAISKELI MOJA AINA YA BAMBUCHA YENYE THAMANI YA TSHS 150,000/= MALI YA IDDY OMARY [37] IMAMU WA MSIKITI WA SAE, MKAZI WA IGANZO.

AWALI MAREHEMU AKIWA MSIKITINI HAPO ALITOKA NDANI YA  MSIKITI NA KUIBA BAISKELI HIYO WAKATI IMAMU AKIWA NDANI NA  WANANCHI WALIMUONA KISHA KUMKAMATA NA KUMSHAMBULIA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA  WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA  KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI BADALA YAKE WAHAKIKISHE WANAWAFIKISHA KATIKA MAMLAKA HUSIKA WATUHUMIWA WANAOWAKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI ILI HATUA ZA KISHERIA DHIDI YAO ZICHUKULIWE. AIDHA ANATOA RAI KWA JAMII KUJENGA TABIA YA KUJITAFUTIA KIPATO KWA NJIA HALALI BADALA YA KUTAKA UTAJIRI WA HARAKA KWA NJIA ZA MKATO ZISIZO HALALI KWANI ZINA MADHARA KATIKA JAMII.


KATIKA TUKIO LA PILI:

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI 1. ABDULSALAM MOHAMED [19] NA 2. ABRUHAMAN HAYALEMASI [28] WOTE RAIA NA WAKAZI WA NCHINI ETHIOPIA WAKIWA WAMEINGIA NCHINI BILA KIBALI.

WATU HAO WALIKAMATWA TAREHE 14.04.2014 MAJIRA YA SAA 10:50 ASUBUHI KATIKA KIJIJI CHA NTENGANO, KATA YA IJOMBE, TARAFA YA TEMBELA, WILAYA YA MBEYA VIJIJINI KUFUATIA TAARIFA ZILIZOTOLEWA NA WASAMALIA WEMA  KWA JESHI LA POLISI AMBALO LILIFANIKIWA KUWAKAMATA.TARATIBU ZA KUWAKABIDHI IDARA YA  UHAMIAJI ZINAFANYIKA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA  MSAIDIZI MWANDAMIZI  WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA JUU YA  MTU/WATU WANAOWATILIA SHAKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA DHIDI YAO ZICHUKULIWE IKIWA NI PAMOJA NA RAIA WA KIGENI.


Signed by:
[BARAKAEL MASAKI – ACP]
Kny: KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Alhamisi, 10 Aprili 2014

KIMBUNGA CHAHARIBU NYUMBA 104, MSAADA WAHITAJIKA HARAKA


Juu na chini ni Kamanda wa UVCCM wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya, Ibrahimu Ismail(Mwakabwanga),(Kulia) akimkabidhi bati 96, Mwenyekiti wa Kijiji cha Manienga, Cosmas kasoli, baada ya kijiji hicho kuezuliwa na kimbunga nyumba 104 wilayani humo

  Kamanda wa UVCCM Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya, Ibrahimu Ismail(Mwakabwanga), akiwapo pole baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Manienga wilayani humo, baada ya kukumbwa na kimbunga ambacho kiliezua nyumba 104 na kuziacha familia 86 zikiwa hazina makazi, ambapo kamanda huyo alitoa msaada ya bati 96.

WAZAWA wa wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya, wameombwa kujitokeza kusaidia familia 86, zilizokumbwa na kimbunga eneo la Manienga wilayani humo na kuezua jumla ya nyumba 104.

Tukio hilo lililoleta madhara makubwa na kuhitaji msaada wa kiutu, lilitokea April 7, mwaka huu.

Akizungumza na wananchi wa eneo hilo, Mwenyekiti wa Vijana wa UVCCM, wilayani humo, Amin Kimulungu, aliviomba vyombo vya habari kufikisha taarifa ya tatizo hilo kwa wazawa wote wa Mbarali waliopo ndani na nje ya wilaya hiyo, kujitokeza kusaidia familia zilizoathirika.

Kimulungu aliyasema hayo alipoongozana na Kamanda wa UVCCM wilayani humo, Ibrahimu Ismail(Mwakabwanga), alipowatembelea wananachi hao na kutoa bati 96 kwa uongozi wa Kijiji hicho cha Manienga.

Akikabidhi bati hizo, Ibrahimu, alisema kuwa, aliguswa na tatizo hilo na alionya kuwa msaada wake hauendani na masuala ya kisiasa.

‘’Hapa siyo mahala pa kupiga siasa, naomba mpokee bati hizi 96 na uongozi wa Kijiji utajua uzigawanye kwa mtiririko upi’’ alisema Ibrahimu Ismail(Mwakabwanga), ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Usangu Logistics.

Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho Modestus Mjimu, alito taarifa kuwa, kimbunga hicho licha ya kusababisha hasara kubwa ya mazingira, kiliezua nyumba 104, makazi 86 na nyumba za taasisi zikiwa 7.

Naye Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Cosmas Kasoli, alisema nyumba 34 zilikuwa za nyasi, madhara ya kibinadamu pia yalijitokeza ambapo wananchi 9 walijeruhiwa.

‘’Majeruhi walikuwa tisa ambao wote walipelekwa hospitali ya wilaya ya Mbarali(Rujewa), wanaume walikuwa wawili na wanawake saba na tathimini yote tumemkabidhi Mkuu wa wilaya na kamati yake ya Ulinzi na usalama ’’ alisema Kasoli.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...