Jumapili, 9 Februari 2014

NJEZA; AJIRA ILIYOBAKI KWA VIJANA TANZANIA NI KILIMO

  KAMANDA wa UVCCM Mbeya Vijijini, ORAN NJEZA, akihutubia wananchi wa eneo la Jojo, kata ya Santilya, wilaya ya Mbeya, kwenye kampeni za udiwani, ambapo alishangiliwa aliposema kuwa ''Kipele kimempata mkunaji'' akiwa na maana kuwa anatosha kuwa kamanda wa UVCCM wilayani humo.
  KAMANDA wa UVCCM Mbeya Vijijini, ORAN NJEZA,(kulia),akizungumza na vijana wa UVCCM kata ya Santilya wilaya ya Mbeya, Jimbo la Mbya Vijijini, jana.
 Mkutano wa kampeni Jojo kata ya Santilya wilaya ya Mbeya.
 
MTAALAM aliyebobea katika masuala ya mifumo ya benki barani Afrika, Oran Njeza, amesema kuwa ajira nzuri iliyobaki kwa vijana wa kitanzania ni kilimo.

Hayo ameyasema jana Februari 8, mwaka huu, alipokuwa akizungumza na vijana wa kata ya Santilya wilaya ya Mbeya, Jimbo la Mbeya Vijijini wakiwa wanajiandaa kuelekea katika uchaguzi mdogo wa udiwani wa kata hiyo, uliomalizika jana jioni.

Njeza, ambaye pia ni kamanda wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) UVCCM katika wilaya hiyo, alisema vijana wengi hawawezi kumwelewa kirahisi kwasababu ya mazoea.

‘’Najua wengi hamnielewi, lakini ajira nzuri Tanzania ni kilimo ambacho kwa hekali moja ukilima vizuri, kwa mwaka unaweza kupata Milioni mbili na zaidi, sifanyi utafiti maana mimi nimeacha kazi za benki Lagos nchini Nigeria sasa nalima, na nimelima karibia maisha yangu yote’’ alisema Njeza.

Akijibu maswali ya vijana hao ambao baadhi walihoji kuwa tatizo ni upatikanaji wa ardhi na masoko, alisema siyo kweli, kwasababu katika nchi ambayo haina tatizo la ardhi ni Tanzania. Ila vijana wengi wanachagua ardhi na wanataka kulima maeneo ya kwao tu, ila suala la soko alikiri kuwepo na tatizo hilo.

Aliwaonya vijana kote nchini, kujiepusha kuanzisha vurugu katika chaguzi mbaimbali kwa kutumiwa na wanasiasa ambao kiuhalisia hawawezi kubadilisha maisha yao kiuchumi bali wao wenyewe wanapaswa kutia bidii katika kufanya kazi.

‘’Taifa linapoharibika wanaoumia ni vijana kwa kutumika kwenye miparaganyiko na wanasiasa, kila mmoja ajiulize anawajibu gani kwa taifa maana ukitaka ushindi mzuri siyo magoli bali ni uchumi. Mimi nipo tayari kushirikiana kwa ushauri na yeyote anayetaka kujishughulisha katika kilimo ili kujikwamua kiuchumi’’alisema Njeza.

MBUNGE WA CCM MBEYA VIJIJINI, AJERUHIWA KWENYE UCHAGUZI MDOGO SANTILYA

 Mbunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini Mch. Luckson Mwanjale.(Picha na maktaba ya kalulunga media)

*SABA WAKAMATWA, WENGINE WASAKWA.

MBUNGE wa Mbeya Vijijini, Mchungaj Luckson Mwanjale, amejuruhiwa na vijana wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), alipokuwa eneo la Shipongo akifuatilia uchaguzi mdogo wa kata ya Santilya katika Jimbo hilo leo asubuhi.

Habari zinasema kuwa, Mbunge huyo alifika katika eneo hilo na kukuta uchaguzi  unaendelea salama ingawa awali kulikuwa na rabsha za hapa na pale kati ya vijana wageni katika eneo hilo na vijana wa CCM wenyeji.

Vyanzo vyetu vya uhakika, vimesema kuwa, vijana hao wageni, walipohojiwa kuwa walikuwa wakitafuta nini walidai kuwa wao ni mawakala wa Chadema ili hali mawakala walikuwa kweye vyumba vya uchaguzi.

Imeelezwa kuwa, vijana hao waitawanywa na askari polisi kisha wakapigiana simu na wenzao ambao walienda umbali wa zaidi ya mita 300 ambako walimvizia Mbunge huyo na kumjeruhi vibaya kichwani na wakati wanataka kukimbia, walikumbana na mkono wa dola huku wengine wakifanikiwa kukimbia.

Mbali na Mbunge huyo, mwingine aliyejeruhiwa ni Mchumi wa CCM wilaya hiyo, aliyefahamka kwa jina la Mwanjuguja.

Baada ya hapo, gari moja lilishikiliwa na polisi huku lingine walilokuwa nalo vijana hao lilitolewa upepo eneo hilo. Gari lililokuwa limetolewa upepo mpaka majira ya saa saba mchana lilikuwa eneo la tukio ni lenye namba za usajiliT 222 AKG Toyota Hilux.

Alhamisi, 6 Februari 2014

KARIBUNI SANA MBEYA

 DR. MARY MWANJELWA, AKISALIMIANA NA MAKAMU MWENYEKITI WA CCM TAIFA, MZEE PHILIP MANGULA ALIPOWASILI OFISI YA CCM MKOANI MBEYA KWA AJILI YA MAAZIMISHO YA MIAKA 37 YA CCM TAIFA.

Jumanne, 4 Februari 2014

MVUA KUBWA ILIYOAMBATANA UPEPO YAHARIBU NYUMBA ZAIDI KUMI ILOLO JIJINI MBEYA





Mwandishi wa Mbeya yetu joseph mwaisango akimpa pole bibi Enea kwa kumpa kiasi kidogo cha msaada ili kimsaidie kwa siku hiyo maana chakula chote kimeharibika na maji


Kanisa la Moravian Ilolo likiwa limejaa maji ndani



Hakika inasikitisha watoto hawa wametoka shule wanakuta nyumba yao imebomoka na mvua kubwa ilionyesha jijini Mbeya  wazahi wa watoto hao hawakuwepo nyumbani









Mwenyekiti wa mataa Sinde A  Anyandwile Mwansanu akiongea na waandishi wa habari



Mama na mwanae mgongoni hajui aanzie wapi kutoa maji yalioingia nyumbani kwake






Jumatatu, 3 Februari 2014

UJIO WA RAIS JAKAYA KIKWETE UWANJA WA NDEGE SONGWE MBEYA, VIONGOZI WAKIMSUBIRI

16Dr.Mary Mwanjelwa Mbunge wa viti maalum CCM mkoa wa Mbeya, akisalimiana na makada wa chama hicho kushoto ni Kada wa CCM Richard Kasesela. 17Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mh. Dr. Norman Sigalla wakati alipokuwa akizungumza jambo naye katikati ni Kada wa CCM, Charles Mwakipesile na kulia ni Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abas Kandoro.  19Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya SACP  AHMED Z. MSANGI wakati wa mapokezi hayo. 20Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na viongozi wanawake wa mkoa wa Mbeya.

DR. MARY MWANJELWA ASHIRIKI KAMPENI ZA UDIWANI MBEYA VIJIJINI NA WILAYANI RUNGWE

 Dr.Mary Mwanjelwa akigalagala kama mila ya Kinyakyusa, Mgombea wilayani Rungwe mkoani Mbeya.



 Dr. Mary Mwanjelwa, akimnadi mgombea udiwani kata ya Santilia, wilaya ya Mbeya Vijijini, Anthon Mboma.


Wialayani Rungwe.






Dkt. Mary Mwanjjelwa (katikati) akiwa na Katibu Mkuu wa UWT Taifa mhe. Amina Makilagi (kushoto) na Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Mbeya Priuscila Mbwaga wakiongoza Wanawake wa Jiji la Mbeya CCM waliokwenda kuwafariji wagonjwa huko kituo cha Afya Igawilo Uyole Kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 37 Jiji la Mbeya.




MIAKA 37 YA CCM MBEYA 02/02/2014

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, akiwasili katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini Mbeya kuwaongoza wana-CCM katika kilele cha maadhimisho ya miaka 37 ya CCM leo  Rais Jakaya Kikwete akiwapungia wananchi waliofurika katika Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya alipoingia Uwanjani huku akiwa na Mwenyekiji wake, Katibu Mkuu wa CCM, Abdurlahman Kinana

 Hii ndiyo CCM, Rais Jakaya Kikwete akisema, huku akionyesha alama ya CCM ya jembe na nyundo ambayo aliichukua kwa mmoja wa mashabiki wa CCM walioingia nayo Uwanjani.


MWENYEKITI wa CCM, Rais Jakaya Kikwete leo amevunja ukimya na kuzungumzia suala la mawaziri waliotuhumiwa na wananchi kuwa mizigo wakati wa ziara za Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na baadhi ya wajumbe wa sekretarieti katika mikoa kadhaa nchini mwishoni mwa mwaka jana.
 
"Najua wapo baadhi ya watanzania, walitaka Mawaziri waliotajwa kuwa ni mizigo wafukuzwe kazi, na kwa vile halikufanyika basi suala hilo limegeuzwa kuwa la malumbano,  ni vyema ieleweke kuwa kuitwa kwa Mawaziri hao na Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), hakuna maana ya kuishia kufukuzwa", alisema, Kikwete leo akihutubia maelfu ya watu katika sherehe za kilele cha miaka 37 ya CCM, kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya. 

Alisema Mawaziri hao waliitwa kwa sababu ya kuwepo matatizo yaliyoonekana yanatakiwa yapatiwe ufumbuzi, matatizo hayo yamezungumzwa na maelekezo kutolewa kuhusu cha kufanya.

"Kamati Kuu ya CCM imetimiza wajibu wake uliobaki ni wa serikali.Kamati Kuu itaendelea kufuatilia na kama hakuna maendeleo ndipo inapoweza kuamua kuomba mamlaka ya uteuzi ichukue hatua zipasazo dhidi ya mhusika.Huko hatujafika" alisema Rais Kikwete.

Rais Kikwete alimpongeza Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akisema, ziara ambazo amekuwa akifanya ni mfano unaopaswa kuigwa na viongozi wengine hasa wa CCM kwa sababu ndio hasa unaotakiwa.

Alisema ziara za Kinana zinakijenga Chama na kutoa taswira nzuri ya CCM katika jamii kwani zinahuisha uhai wa CCM kwa kuwa Katibu Mkuu huyo katika ziara hizo huenda hadi kwa wanachama waliopo ngazi za chini.

"Katibu Mkuu Kinana amekuwa anafanya mambo ambayo baadhi ya watu wanadhani kuwa ni mageni, lakini katika kufanya hayo amekuwa pia akionyesha umahiri na ujasiri mkubwa kwa kwenda  maeneo ambayo ni magumu kufikika" alisema Rais Kikwete na kuongeza;

"Katika ziara hizo  wakati mwingine amekuwa anatumia njia za usafiri zinazoogopesha, amewahi kutumia meli  ya MV Songea kutoka mkoani Ruvuma hadi Mbeya, amepanda milima na mabonde kwa magari katika maeneo ambayo ni hatari, lakini lengo likiwa ni kuhakikisha anawafikia wanachama wa ngazi za chini kabisa".

Rais Kikwete alisema mambo mengine yalivyomvutia katika ziara za Kinana, ni hatua ya Katibu mkuu huyo kwenda kukaa na  kula na wananchi katika ngazi za chini na kisha kufanya nao kazi za maendeleo  na zaidi kutoa fursa kwa wananchi kueleza matatizo na manung'uniko yanayowasibu.

Mwenyekiti huyo wa CCM Taifa alisema Katibu mkuu wa Chama amekuwa anashiriki katika kutafuta majawabu na matatizo anayoambiwa hali ambayo imesaidia sana kumaliza baadhi ya matatizo kulekule mikoani.

"Pale ambapo pamekuwa panahitaji hatua zaidi za serikali hakusita kutoa taarifa kwa Waziri Mkuu, vile vile amekuwa anatoa taarifa ya ziara zake kwenye Kamati Kuu ya CCM" alisema Rais Kikwete.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...