Jumamosi, 28 Oktoba 2017

DKT MWANJELWA AFUNGUA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA TFA JIJINI ARUSHA

 Mgeni Rasmi- Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wakulima wa Tanganyika (TFA). leo Octoba 28, 2017 Jijini Arusha. Picha zote Na Mathias Canal
 Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wakulima wa Tanganyika (TFA). leo Octoba 28, 2017 Jijini Arusha.
 Mgeni Rasmi-Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) akishiriki sala ya kumuombea Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli mara baada ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wakulima wa Tanganyika (TFA). leo Octoba 28, 2017 Jijini Arusha.
 Wanachama wa Chama cha Wakulima wa Tanganyika (TFA) wakifatilia Mkutano Mkuu wa Mwaka uliofanyika katika ukumbi wa TFA Shooping Centre, Ngarenaro – Jijini Arushaleo Octoba 28, 2017. 
  Muwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe Gabriel Fabian Daqarro akitoa salamu za Mkoa muda mfupi kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi-Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) kwa ajili ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wakulima wa Tanganyika (TFA). leo Octoba 28, 2017 Jijini Arusha. 
 Mkazi wa Moshi Mkoani Kilimanjaro ambaye ni Mwanachama wa TFA Shekh Ally Mwamba akiongoza wanachama wa TFA kumuombea Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli mara baada ya Mgeni Rasmi-Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) kufungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wakulima wa Tanganyika (TFA). leo Octoba 28, 2017 Jijini Arusha.
 Mgeni Rasmi-Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) akisalimiana na Katibu wa Kampuni ya TFA na Ofisi ya kisheria Bi Pendo Jacob mara baada ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wakulima wa Tanganyika (TFA), Mwingine ni Bi Cathy Elizabeth S. Long'lway. leo Octoba 28, 2017 Jijini Arusha.
 Mgeni Rasmi-Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) akisikiliza maelezo kuhusu Kazi za TFA banda la TFA mara baada ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wakulima wa Tanganyika (TFA), Kulia kwake ni Mwenyekiti wa TFA Ndg Peter Ezrah Sirikikwa, na kushoto kwake ni Muwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe Gabriel Fabian Daqarro. leo Octoba 28, 2017 Jijini Arusha. 

 Mwanachama wa Chama cha Wakulima wa Tanganyika (TFA) Bi Mwanahamisi Salim Bakari akitoa shukrani zake kwa Mgeni Rasmi-Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka uliofanyika katika ukumbi wa TFA Shooping Centre, Ngarenaro – Jijini Arushaleo Octoba 28, 2017. 

Picha ya pamoja Mgeni Rasmi-Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Mb), Mwenyekiti wa TFA Ndg Peter Ezrah Sirikikwa, Muwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe Gabriel Fabian Daqarro na viongozi wengine wa TFA mara baada ya ufunguzi wa MkutanoMkuu wa Mwaka uliofanyika katika ukumbi wa TFA Shooping Centre, Ngarenaro – Jijini Arushaleo Octoba 28, 2017. 

Na Mwandishi Wetu

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) leo Octoba 28, 2017 amekipongeza Chama cha Wakulima wa Tanganyika (TFA) kwa kuendelea kufungua matawi mengi nchini ya kuuza pembejeo bora za kilimo.

Mhe Mwanjelwa ametoa pongezi hizo wakati akihutubia kwenyeUfunguzi wa Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Tanganyika Farmers’ association (TFA) uliofanyika katika ukumbi wa TFA Shooping Centre, Ngarenaro – Jijini Arusha.

Alisema kuwa hiyo ni ishara njema ya kuunga mkono Ilani ya Chama cha Mapinduzi na juhudi za Serikali katika kuendeleza Sekta za kiuchumi ambazo ni Kilimo, Mifugo na Uvuvi.

Alisema kuwa Kwa wajibu huo, Wizara ya kilimo imeona juhudi kubwa na za makusudi za  Kampuni ya TFA jinsi ilivyojipanga katika kuwahudumia Wananchi na Wakulima nchini.

Kupitia Mkutano huo Aliwaomba Wananchi wote kuendelea kuiunga mkono Kampuni ya TFA ili waweze kupata maendeleo ya haraka kwa kuongeza tija na uzalishaji katika Sekta ya Kilimo ili kuondokana na kilimo cha mazoea na kuingia katika kilimo cha kisasa.

Mheshimiwa Dkt Mwanjelwa alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli imetoa msukumo mkubwa katika  kuendeleza Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na hasa kwa kuzingatia kuwa nchi imeaanza safari ya kuelekea kwenye uchumi wa Viwanda ambao unazitegemea Sekta hizo kama chanzo cha malighafi kwa ajili ya kuziongeza thamani bidhaa lakini pia kuzisindika kwa ajili ya biashara katika soko la ndani na nje.

Alitoa Rai kwa Wananchi wote na Wanachama wa TFA kutumia vizuri mtandao wa Mawakala wa TFA, kwani inalenga kumuondolea Mkulima matatizo ya upatikanaji na matumizi ya pembejeo hafifu za kilimo.

Alisema hiyo ndiyo ishara ya kuifanya TFA iweze kuendelea kutoa huduma zake kwa kipindi chote cha zaidi ya miaka 80 tangu kuanzishwa kwake.

“Nichukue fursa hii nafasi hii kuwakumbusha wanachama wa TFA na Wananchi kwa ujumla kuwa, Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuliamedhamiria kuendeleza Viwanda vilivyopo hapa nchini, na kuanziasha vipya, nanyi kama Wabia, Wadau wa Wakulima katika kuchangia maendeleo ya viwanda hivyo, natoa rai kwenu kuendelea kukithamini kilimo kwa kuongeza tija na uzalishaji, ili viwanda vilivyopo na vitakavyoanzishwa viweze kupata malighafi na rasilimali zakutosha na hatimaye tufikie kwenye uchumi wa kati” Alikaririwa Mhe Mwanjelwa

Mhe Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Dkt Mary Mwanjelwa alisema kuwa Wizara ya Kilimo imeamua kuweka utaratibu wa kununua mbolea hapa nchini kupitia Mfumo wa Ununuaji wa Pamoja ya “Bulk Procurement System - BPS” na wakati huohuo kuanzisha Mfumo wa Kuuza Mbolea kwa bei Elekezi, ambapo kwa sehemu kubwa ya nchi mbolea imeshuka kwa zaidi ya asilimia 30.

Mfumo huo unalenga kupunguza kero ya upatikanaji na ulanguzi katika bei za mbolea. Kupitia mfumo huo, Serikali inaamini matumizi ya mbolea hapa nchini yataongezeka kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na miaka iliyopita, na kuwa na ongezeko kubwa la uzalishaji wa mazao ya kilimo.

Huduma zinazotolewa na TFA ni kuuza Zana bora za kilimo, Pembejeo za kilimo kama Mbolea, Mbegu bora, Viuwatilifu mbalimbali pamoja na kutoa huduma za ushauri wa kitaalamu kwa Wakulima, kama juhudi ya kumpunguzia mkulima, mmekuwa mkiagiza baadhi ya pembejeo toka nje ya nchi kwa kuzingatia sheria na taratibu zote.  Nawapongeza kwa jinsi mlivyojipanga vema katika kutekeleza majukumu yenu kwa ufanisi wa hali ya juu ili kuleta mabadiliko makubwa katika Sekta ya Kilimo.

Katika Mkutano huo hoja mbalimbali zimeibuka kutoka kwa wanachama ikiwemo Ongezeko la gharama za mahindi katika Mkoa wa Njombe hoja ambayo Mhe Naibu Waziri ameahidi kuzuru Mkoani Mbeya kufatilia jambo hilo.

Aidha, Baadhi ya wanachama wamempongeza Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufulikwa kufuta

Jumla ya tozo 80 ambapo kati ya tozo 139 zimefutwa na tozo nne (4) zimepunguzwa viwango. Tozo, kodi na ada zinajumuisha  kufutwa kwa tozo kumi (10) na mbili (2) kupunguza viwango kwenye zao la tumbaku.  Kwenye zao la kahawa zimefutwa tozo 17 na moja (1) kupunguzwa kiwango; sukari zimefutwa 16; pamba tozo zilizofutwa ni mbili (2); kwenye korosho tozo mbili zimefutwa na chai imefutwa tozo moja (1).

Katika kuongeza upatikanaji wa pembejeo tozo tatu (3) zimefutwa na moja (1) imepunguzwa kiwango kwenye mbolea na  tozo saba (7) zilizokuwa kwenye mbegu nazo zimefutwa. Katika Ushirika jumla ya tozo 20 zimefutwa katika ngazi mbalimbali.

Alhamisi, 19 Oktoba 2017

DKT MWANJELWA: TUMIENI USHIRIKA KUPIGA VITA ADUI NJAA, UJINGA, MARADHI NA UMASKINI

Mgeni Rasmi, Naibu Waziri – Wizara ya Kilimo, Dkt. Mary Mwanjelwa akiangalia sehemu ya bidhaa za chakula zilizosindikwa kutoka katika Vikundi vilivyoanzishwa chini ya  Ushirika wa Akiba na Mikopo wa TANESCO (TANESCO - SACCOS) katika Viwanja vya Chuo cha Mipango wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kitaifa ya SACCOS inayoadhimishwa Kitaifa Mkoani Dodoma
Mgeni Rasmi, Naibu Waziri – Wizara ya Kilimo, Dkt. Mary Mwanjelwa akipa maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Ngome SACCOS Brigedia Jenerali Charo Hussein Yateri namna ambavyo inajiendesha kwa mafanikio makubwa ikiwa na Wanachama zaidi ya 12,500 nchini katika Viwanja vya Chuo cha Mipango wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kitaifa ya SACCOS inayoadhimishwa Kitaifa Mkoani Dodoma


Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Dkt. Mary Mwanjelwa amewataka Washiriki wa Mkutano wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS), kuvitumia Vyama hivyo kama silaha ya kujikwamua kiuchumi na kujiletea maendeleo ya kweli.
Dkt. Mary Mwanjelwa ambaye ndiye mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya kuadhimisha Uanzishwaji wa Vyama vya Akiba na Mikopo amesema hakuna ubishi kuwa mafanikio yaliyopatikana kupitia Vyama hivyo yanadhihirisha kuwa ni njia madhubuti ya Wananchi katika kupambana na adui njaa, ujinga, maradhi na umaskini.
Dkt. Mwanjelwa amekaririwa akisema “Nimetembelea mabanda kadhaa ya Vyama vya Akiba na Mikopo kutoka Taasisi za Umma kama Ngome SACCOS, TANESCO SACCOS, Bandali SACCOS, wameniambia kiasi cha mitaji waliyonayo ni unazungumzia mabilioni ya Shilingi za Kizanzania, ambapo Wanachama wanakopeshana kwa riba nafuu na kwa muda mzuri”
“Jambo hilo linatia moyo na niwaombe Viongozi na ninyi Wanachama ambao mmejiunga kwenye Vyama vya Akiba na Mikopo kuwahamasisha wengine kujiunga na Vyama vya Akiba na Mikopo ili tuongeze wigo wa idadi kubwa ya Watanzania”. Amekaririwa Naibu Waziri.
“Na kama Watanzania wengi watajiunga basi tutakuwa na nafasi kubwa kama Taifa kupambana na maadui hawa watatu ambao ni ujinga, maradhi na umaskini”. Amekaririwa Naibu Waziri Dkt. Mwanjelwa.
Aidha, Naibu Waziri, Dkt. Mwanjelwa ameuagiza Mrajis wa Vyama vya Ushirika nchini Bwana Tito Haule, kuhakikisha anaitumia nafasi ya kuelimisha umma kuhusu faida na uzuri wa USHIRIKA kupitia Vyama vya Kuweka na Kukopa kama ndiyo silaha ya kupeleka mbele maendeleo ya Ushirika nchi.
“Mrajis elimu kwa Umma ni jambo la muhim sana, hata kama mnafanya mambo mazuri lakini kama Wananchi hawatafahamu kuhusu faida na mambo mazuri yanayohusu kujiunga na Vyama vya Akiba na Mikopo itakuwa ni kazi bure, fanyeni kila linalowezekana ili kuwaelimisha Watanzania”.
Dkt. Mwanjelwa ameongeza kuwa USHIRIKA pia ni njia ya kuongeza tija na uzalishaji katika mazao ya kilimo na kwa njia hiyo, uzalisahaji wa mazao ya kilimo kwa ajili ya viwanda vya kati na vikubwa unaweza kuongezeka kwa kutumia Vyama vya Akiba na Mikopo.
“Msisahau kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imedhamilia katika kulifikisha Taifa kwenye uchumi wa viwanda na Watanzania wengi wanaojihusisha na Sekta ya Kilimo ni zaidi ya asilimia 75 kwa maana hiyo, Vyama vya Akiba na Mikopo pia vitumike katika kuongeza tija na uzalishaji wa malighafi za viwanda vya usindikaji vidogo, vya kati na vikubwa”. Amemalizia Dkt. Mary Mwanjelwa.
Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS) yalianza rasmi jana tarehe 18 Oktoba na yanafikia kilele leo tarehe 19 Oktoba, 2017 katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango, Mjini Dodoma.

Jumapili, 15 Oktoba 2017

DKT MWANJELWA AISHAURI (IITA) KUONGEZA SPIDI UTOAJI ELIMU KWA WANANCHI KUKABILIANA NA SUMU KUVU

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa akisikiliza maelezo kuhusu namna ya kuikabili Sumu Kuvu kutoka kwa Msaidizi wa Mawasiliano wa Utafiti katika Taasisi ya Kimataifa ya Kilimo ukanda wa Kitropiki (IITA) nchini Tanzania Bi Eveline Massam wakati alipotembelea Banda la Taasisi hiyo wakati wa maadhimisho ya siku ya chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika katika uwanja wa CCM Kalangalala Mkoani Geita.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa akipokea zawadi ya Boga kutoka kwa Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe mara baada ya kutembelea Banda la Taasisi hiyo wakati wa maadhimisho ya siku ya chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika katika uwanja wa CCM Kalangalala Mkoani Geita.
Afisa habari na Uelimishaji Jamii kutoka Mamkaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Bi Robert Feruzi (Kulia) akimuelezea Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa jinsi Mamlaka hiyo inavyofanya kazi wakati alipotembelea Banda la Taasisi hiyo kwenye maadhimisho ya siku ya chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika katika uwanja wa CCM Kalangalala Mkoani Geita.
Meneja Mwendeshaji wakulima wadogo kutoka Benki ya wakulima (TADB) Ndg Joseph Mabula (Kulia) akimuelezea Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (KUshoto) jinsi inavyofanya kazi wakati alipotembelea Banda la Benki hiyo hiyo kwenye maadhimisho ya siku ya chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika katika uwanja wa CCM Kalangalala Mkoani Geita.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa akionyesha Mvinyo uliotengenezwa na wajasiriamali wadogo wakati alipokuwa akitembelea mabanda mbalimbali kwenye maadhimisho ya siku ya chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika katika uwanja wa CCM Kalangalala Mkoani Geita.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa akikagua mashine mbalimbali katika Banda la kampuni ya POLY MACHINERY CO.LTD kwenye maadhimisho ya siku ya chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika katika uwanja wa CCM Kalangalala Mkoani Geita.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa akikagua baadhi ya vyakula vilivyohifadhiwa kwenye vifungashio kwenye maadhimisho ya siku ya chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika katika uwanja wa CCM Kalangalala Mkoani Geita.

Na Mathias Canal, Geita

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa ameishauri Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Kilimo ukanda wa Kitropiki (IITA) kuongeza kasi ya utoaji elimu kwa wakulima nchini kuhusu kadhia ya Sumu Kuvu.

Alisema kuwa elimu hiyo inatakiwa kutolewa katika maeneo mbalimbali nchini ili wananchi waweze kutambua namna bora katika uandaaji wa mashamba wakati wa msimu wa kilimo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha mashamba hayashambuliwi na magugu wala wadudu waharibifu.

Naibu Waziri ametoa ushauri huo wakati akizungumza na Msaidizi wa Mawasiliano wa Utafiti katika Taasisi ya Kimataifa ya Kilimo ukanda wa Kitropiki (IITA) nchini Tanzania Bi Eveline Massam mara baada ya kutembelea Banda hilo wakati wa Maonesho ya 36 ya siku ya Chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika Katika Uwanja wa CCM Kalangalala Mjini Geita kuanzi Octoba 10 mpaka Octoba 16.

Dkt Mwanjelwa alisema kuwa wakulima wengi nchini wanalima pasina kufahamu taratibu za kilimo cha kisasa jambo ambalo linapelekea mazao yao kuathiriwa na wadudu husani Sumu Kuvu na kupelekea uduni wa mavuno.

Alisema kuwa endapo Taasisi hiyo ya (IITA) itaongeza nguvu ya utoaji elimu kwa wakulima kwa kushirikiana na wataalamu wa Wizara ya kilimo, wananchi watanufaika na kilimo chao ikiwa ni pamoja na kuwa na mavuno mengi.

Alisema Sumu Kuvu inahatarisha afya za watumiaji wa mazao mbalimbali ya chakula na biashara, kwani chakula na malisho ya mifugo iliyo athiriwa na sumu kuvu hupunguza uzalishaji huku mazao yenye kiwango kikubwa cha Sumu Kuvu zaidi ya kiwango kinachoruhusiwa kutekelezwa au yanauzwa kwa bei ya chini.

Aidha, zipo athari za moja kwa moja kwani endapo binadamu au mnyama atakula chakula chenye malisho yenye kiwango kikubwa cha Sumu Kuvu anaweza kupoteza maisha.

Kwa upande wake Msaidizi wa Mawasiliano wa Utafiti katika Taasisi ya Kimataifa ya Kilimo ukanda wa Kitropiki (IITA) nchini Tanzania Bi Eveline Massam alisema kuwa Sumu Kuvu huzalishwa wakati fangasi aina ya Aspergillus anaposhambulia mbegu shambani/ghalani.

Aliongeza kuwa Ukuaji wa fangasi na athari za sumu kuvu husababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa (Ukame wa ongezeko la joto), Mbinu duni za kilimo kabla na baada ya kuvuna mazao kwa mfano; ukaushaji hafifu wa mazao punde yanapovunwa, na uhifadhi duni wa mazao ghalani na wadudu waharibifu.

Sumu Kuvu ni aina za kemikali za sumu zinazozalishwa na aina ya Ukungu au Fangasi wanaoota kwenye mbegu za nafaka kama vile mahindi, mbegu za mafuta kama karanga, jamii ya kunde na pia mazao ya mizizi. Pia sumu Kuvu hupatikana katika bidhaa za mifugo kama vile maziwa, mayai na nyama pale ambapo chakula kinacholiwa na mifugo kitakuwa kimechafuliwa na sumu hizo.

Sambamba na hayo pia Naibu waziri wa Kilimo  Mhe Dkt Mary Mwanjelwa alitembelea Banda la Benki ya Maendeleo ya kilimo, Banda la Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe, Banda la Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe na Banda la Mamlaka ya chakula na dawa (TFDA).


Maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani hufanyika kila mwaka kuanzia Octoba 10 mpaka Octoba 16 ambapo kwa mara kwanza  yalianza mwaka 1981. Hivyo maadhimisho ya mwaka huu ni ya 36 na yanasherehekewa kwa pamoja na maadhimisho ya  miaka 72 ya kuanzishwa kwa FAO tarehe 16 Oktoba, 1945.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...