Jumatano, 26 Novemba 2014

MAMLAKA YA BANDARI KUJENGA MELI ZIWA NYASA


Na Saidi Mkabakuli, Kyela

Kufuatia adha ya usafiri wa majini inayowakabili wakazi waishio katika fukwe za Ziwa Nyasa, Mamlaka ya Bandari Tanzania kupitia kituo chake cha Kyela ipo mbioni kujenga meli ya abiria na mizigo ili kuwahudumia wakazi hao.


Hayo yaliwekwa bayana na Mkuu wa Bandari ya Kyela, Bw. Percival Ntetema wakati timu wakaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Tume ya Mipango ilipotembelea na kukagua bandari za Itungi na Kiwira zilizopo wilaya ya Kyela, mkoani Mbeya.


Bw. Ntetema alisema kuwa Mamlaka imeshakamilisha mchakato wa manunuzi na tayari imempata mkandarasi M/S Songoro Marine Transport Ltd kwa ajili ya ujenzi wa meli yenye uwezo wa kubeba jumla ya tani 200 za mizigo na abiria 200.


“Mamlaka ipo kwenye hatua za mwisho za kuandaa mkataba unaotarajiwa kutiwa saini mwezi ujao  na kazi itaanza mwanzoni mwa mwaka ujao,” alisema.


Bw. Ntetema aliongeza kuwa mpaka sasa Bandari ya Kyela imeshaanza maandalizi ya kuvuta umeme uliofadhiliwa na Wakala wa Umeme Vijijini pamoja na kuaanza kwa kujenga matishari mawili ili yaweze kurahisisha utoaji wa huduma mara meli hiyo itakapoanza kazi mwishoni mwa mwaka ujao.


Akizungumza wakati wa ziara hiyo, kiongozi wa timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri aliupongeza uongozi wa Mamlaka kwa hatua yake hiyo kwani itaongeza tija ya shughuli za kiuchumi katika kanda hiyo ya Ziwa Nyasa.


“Ninaupongeza uongozi wa Mamlaka ya Bandari kwa kuanza mchakato huu utakaofungulia fursa za kiuchumi na maendeleo kwenye ukanda huu, hivyo kuunga mkono jitihada za serikali za kupunguza vikwazo mbalimbali vinavorudisha kasi ya kusaka kupunguza umaskini nchini,” alisema. 


Bibi Mwanri aliongeza kuwa kukamilika kwa mradi huo kutatoa fursa za kuhudumia shehena na abiria kutoka mikoa ya Mbeya, Njombe, na Ruvuma. Pamoja na kuhudumia nchi za jirani ikiwemo Malawi, Msumbiji na Zambia.


Kwa mujibu wa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011/2012 – 2015/2016) bandari ni mojawapo ya vipaumbele vitano vya kimkakati vyenye lengo la kufungulia fursa za ukuaji uchumi wa nchi ili kuweka misingi wa uchumi kwa watu walio wengi.  

Vipaumbele vingine ni Kilimo ambapo lengo kuu likiwa ni kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao ya kilimo ili kujitosheleza kwa chakula na kuwa na ziada ya kuuza nje ya nchi; Maendeleo ya viwanda: 

Msisitizo umewekwa katika kuvutia, kuanzishwa na kuendeleza viwanda vinavyotumia malighafi zinazopatikana nchini (kama vile viwanda vya nguo, mbolea, saruji, makaa ya mawe, chuma na bidhaa za chuma) na pia sekta ya madini kwa lengo la kuongeza mapato ya Serikali. 


Pamoja na kipaumbele cha Maendeleo ya rasilimali watu na ujuzi: Mpango unahimiza kuwekeza katika elimu (hasa katika elimu ya juu na vyuo vya ufundi) na huduma za afya (kuongeza ubora na upatikanaji wa huduma) katika kujenga nguvu kazi itakayotuletea maendeleo ya kiuchumi na kijamii; na Utalii, Biashara, na huduma za Fedha ambapo jitihada zimewekwa kwenye uendelezaji uwezo wa kuuza katika masoko ya ndani na nje, kuongeza   idadi ya watalii na matumizi yao wawapo nchini, na kuongeza upatikanaji wa huduma za kifedha.

Jumatatu, 24 Novemba 2014

NI CCM NA CHADEMA SERIKALI ZA MITAA MBALIZI




VYAMA viwili pekee, ndivyo vimethibitisha na kurejesha fomu za kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Mtaa wa Mbalizi, Mbeya Vijijini,mkoani hapa, ili kuunda mji mdogo wa Mbalizi.


 
Msimamizi wa uchaguzi wa eneo hilo, ambaye ni afisa mtendaji wa Kijiji cha Mbalizi, Malongo Sumuni, alivitaja vyama hivyo kuwa ni Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha demokrasia na Maendeleo(Chadema).

Aliwataja wagombea wa nafasi hiyo kuwa ni Asifiwe Godwin  Mwakalonge(CCM), na Elia Wilson  Mkono(Chadema), ambaye ni Mwenyekiti wa Kijiji hicho na ni diwani wa kata ya Utengule Usongwe kupitia Chadema.

“Mbali na kurejesha fomu na kuteuliwa kuwania nafasi hiyo, hawaruhusiwi kufanya kampeni mpaka zitakaporuhusiwa tarehe 30/11/2014 na mwisho itakuwa Desemba 13, mwaka huu” alisema msimamizi huyo.

Alipoulizwa idadi ya wakazi wa eneo hilo, alisema kuwa takwimu alizonazo zinaonesha wakazi 13,690, takwimu ambazo amesema siyo halisi.”Tuna vitongozji vitano ambavyo ni Mlimareli yenye kaya 2900 wakazi 3700, Chapa Kazi kaya 1800 wakazi 3200, DDC kaya 1534 wakazi 2320, Pipeline kaya 1250 wakazi 1650 na Mtakuja kaya 1650 chenye wakazi 3200” alisema Sumuni.

Uchunguzi umebaini kuwa, ofisi yake ilipelekewa idadi ndogo ya wakazi kwa kile wenyeviti wa vitongozi walichokuwa wakihofia katika ukusanyaji wa michango, kuwa endapo wakazi wachache wangechagia, wangesumbuliwa wao kufuatilia.

Mji huo wa Mbalizi, ndiyo kitovu cha siasa za Jimbo la Mbeya Vijijini, ambapo vyama vine vya siasa vimekuwa vikichuana vikiwemo Chama cha wananchi (CUF), NCCR-Mageuzi, CCM na Chadema.

Baadhi ya wananchi wa eneo hilo wameendelea kujiandikisha kwa ajili ya upigaji kura wa viongozi wa serikali za mitaa ifikapo Desemba 14, mwaka huu, huku kila kituo kikiwa na mawakala wa vyama vya siasa, hususani CCM na Chadema.

IRINGA YAJIVUNIA USAFI WA MAZINGIRA



 Vijana wa kikundi cha usafi na uhifadhi wa mazingira cha Umoja wa vijana wazalendo Mbeya(UVIWAMBE), kutoka Mbalizi Mbeya, wakiwa katika picha ya pamoja mjini Iringa wakati wa ziara yao ya mafunzo.
HALMASHAURI ya Manispaa ya Iringa, imesema inajivunia kuwa ni moja ya Halmashauri zenye mazingira safi nchini, kutokana na juhudi za uelimishaji wananchi wake, ikiwa ni pamoja na kutumia vyombo vya habari.

Hayo yalielezwa juzi katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa hiyo na Afisa Afya wa Manispaa hiyo, Christian Ndenga, alipokuwa akitoa taarifa ya maarifa wanayoyatumia kuweka mji safi, alipotembelewa na kikundi cha usafi na uhifadhi wa mazingira cha Vijana wazalendo Mbeya(UVIWAMBE), kutoka wilaya ya Mbeya Vijijini, mkoani Mbeya.

Ndenga alisema kuwa, manispaa hiyo imepata tuzo ya mshindi namba moja kuhusu usafi wa mji, kutokana na jitihada kubwa zinazofanywa baina ya serikali, vikundi vya usafi na wadau wengine wakiwemo wafanyabiashara.

“Tunajivunia mafanikio haya kutokana na kwanza kuwepo kwa sheria zinazodhibiti wachafuzi wa mazingira ambao hutozwa faini isiyozidi Shilingi Elfu Hamsini, kukasimu madaraka ya masuala ya usafi ngazi za kata, uwepo wa vikundi vya usafi na kutosubiri makontena ya uchafu yajae ndipo yakamwagwe” alisema Ndenga.

Alitaja pia vyombo vingine wanavyotumia ili kuhakikisha mji unakuwa safi kuwa ni pamoja na kuwatumia viongozi wa dini, shule na vyuo, huku akisema kuwa waandishi wa habari wamekuwa mstari wa mbele kufika katika ofisi za manispaa kuhoji kama kuna sehemu wameona uchafu jambo ambalo alisema kuwa linawapa msukumo wa kufanya vizuri zaidi na kutoa elimu kwa wananchi.

Alisema kwa sasa, wanapanga mpango wa miaka 20 ijayo kuandaa eneo la kutupia taka badala ya kusubiri eneo walilonalo kwa sasa mpaka hapo litakapojaa.

Baada ya taarifa hiyo, kikundi cha Uviwmbe waliongoza na afisa mmoja wa Manispaa hiyo kitengo cha Afya, Ezekiel Mbushi, kwenda kutembelea soko la Iringa mjini na kukutana na uongozi wa kikundi cha usafi cha mjini hapo kijulikanacho kwa jina la Kikundi cha wafanyabiashara wa masoko(KWBS).

Mwenyekiti wa kikundi hicho Augustino Ngao na katibu wake Aldo Kaduma, walisema kuwa, ili wananchi waweze kutii sheria za usafi ni muhimu wakapatiwa elimu kwanza kabla sheria haijaanza kufanya kazi ambapo walikiri kuwa pamoja na baadhi kupata elimu katika manispaa hiyo, lakini bado wanakuwepo wanaokaidi.

“Changamoto tunayopata katika kutekeleza kazi za usafi ni pamoja na baadhi kukaidi kutii sheria, watu wa haki za binadamu kutukamata wanapowakuta baadhi ya vibarua wa kikundi wakifanya kazi bila kuvaa grovu na pia vifaa kuwa duni yakiwemo matolori ambayo ni tofauti na yale yaliyokuwa yakitengenezwa Mbeya na kiwanda cha ZZK ambacho kilikufa” alisema Kaduma.

Mwanasheria wa Halmashauri ya Mbeya, Prosper Msivala, ambaye aliongozana na wana kikundi cha Uviwambe, alisema kuwa yeye alikuwa mwanasheria wa Manispaa ya Iringa na ni mzawa wa mkoa huo, ambapo anaikumbuka historia mbaya ambayo iliwezesha manispaa hiyo kufika hapo ilipo kuhusu suala la usafi.

“Hapa Iringa mwaka 1988, kulitokea mlipuko wa kipindupindu ambapo kwa siku zaidi ya wananchi 50 walikuwa wakifa na kuzikwa, jambo ambalo lilihamasisha jamii nzima kuanza kuzingatia suala la usafi na kuna wakati tulifikia mahala tukavunja vibanda vilivyowekwa kiholela na baadhi ya nyumba na tukatishiwa kuuawa, lakini kwa sasa mambo safi” alisema Msivala.

Mwenyekiti wa kikundi cha Uviwambe, Ayas Yusuph, aliishukuru Halmashauri ya Mbeya kwa kugharamia safari hiyo na Manispaa ya Iringa kwa kuwapa elimu na kuwaunganisha na kikundi cha usafi cha KWBS na kwamba elimu na maarifa waliyopata katika ziara hiyo ya mafunzo wataitumia vema.

MAGAZETINI LEO NOVEMBA 2014

Benki Kuu ya Tanzania
Benki Kuu ya Tanzania

NIPASHE
Chama cha Wananchi CUF kimemtaka Waziri mkuu Mizengo Pinda ajiuzulu kwa kupotosha umma kuhusu kashfa ya fedha zaidi ya bilioni300 zilizochotwa katika akaunti ya Escrow ndani ya benki kuu ya Tanzania ‘BoT’.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Mwenyekiti wa CUF Ibrahim Lipumba wakati akitoa taarifa kuhusu sakata hilo lililotokea na mkataba wa kuuziana umeme wa dharura kati ya Tanesco na IPTL.

Alisema kuwa Waziri mkuu ndiye kiongozi wa Serikali  ambaye Mei mwaka huu aliupotosha umma na kudai fedha za Escrow zilizoibiwa si za wananchi bali ni za wanahisa.

“Tunamtaka Waziri mkuu awajibike kwa kitendo cha kupotosha umma,kama asipojiuzulu basi afukuzwe kazi mara moja,amekua akitafuta visingizio vya kufuta mjadala na taarifa ya CAG,”Alisema Lipumba.


NIPASHE
Jeshi la Zimamoto na uokoaji nchini limesema ukosefu wa vitendeakazi,rasilimali watu na ufinyu wa fedha wanazokusanya kutoka kwa wananchi ni changamoto zinazokwamisha jeshi hilo kushindwa kutoa huduma za uhakika kwa jamii pindi majanga ya moto yanapotokea.


Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano kwa umma wa jeshi hilo Miraji Kilolo alisema wanapokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kutokana na kutoridhishwana huduma zetu,lakini sisi tumejipanga kumaliza changamoto zote na kutoa huduma bora kwa jamii hasa katika majanga ya moto.

Alisema kuwa magari makubwa ya kuzimia moto yaliyopo hivi sasa hayaendani na mabadiliko ya kukua kwa miji nchini kutokana na hivu sasa magorofa marefu yanayojengwana jeshi hilo hayana vifaa vya kisasavya kuzimia moto.

Alisema jeshi hilo lmefanya mazungumzo na Wenyeviti wa Serikali za mitaa wote kujenga visima vya maji katika mitaa yao ili janga lolote la moto likitokea wapate huduma kwa haraka.


NIPASHE
Ripoti ya uchunguzi wa kashfa ya kampuni ya kufua umeme ya IPTL ya uchotwaji wa shilingi bilioni306 kwenye akaunti ya Tegeta Escrowiliyopobenki kuu ya Tanzania BOT zimeibwa na kuzua mambo.


Kufuatiatukio hilo Jeshi la Polisi Dodoma limewatia mbaroni vijan wawili wanaotuhumiwa kusambaza mitaani ripoti feki ya ukaguzi wa hesabu za fedha hizo uliofanywa na CAG kuhusiana na kashfa hiyo.


Vijana hao ambao wanadaiwa kuwa ni baadhi ya watu waliomo katika kikosi cha Waziri mmoja kilichongia mijini Dodoma,wanadaiwa kusambaza ripoti hiyo feki kwa kutumwa na Waziri huyo.

Kamanda wa Polisi DodomaDavis Misime alithibitisha kukamatwa kwa vijana hao tangu juzi na kusema kuwa walipohojiwa walikiri kupewa nyaraka hizo na mmoja wa Wabunge,ambaye hata hivyo alikataa kumtaja kwa sababu za kiuchunguzi.


UHURU
Watu sita wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa baada ya kupigwa na radi iliyoambatana na mvua kubwa katika chuo cha Mifugo na Uvuvi katika Wilaya ya Songea Vijijini Mkoani Ruvuma.

Kamanda wa Polisi Mkoani humo Mihayo Msekele alisema tukio hilo lilitokea juzi usiku ambapo mvua kubwa ilinyesha ikiambatana na mvua kubwa ambapo wanachuo wawili na wapishi wanne waliokua katika vibanda wakikwepa mvua walifariki baad aya radi kuwapiga.

“Wanafunzi walikua wanakula katika vibanda vyao huku waiikinga na mvua na ndiporadi hiyo ilipiga na sita kati yao walifariki papo hapo na wengine wawili kujeruhiwa na sasa wapokatika ,hospitali ya Wilaya wakipatiwa matibabu,”alisema Mihayo.

Mihayo alisema kulitokea mwanga mkali wakati tukio hilo likitokea na sauti kubwa ambayo ilisababisha nguzo za vibanda hivyo kuchanikachanika huku wanafunzi wengine wakikimbia.


UHURU
Utupaji watoto wachanga katika mto Ngarenaro Mkoani Arusha umekithiri hali inayohatarisha maisha ya wkaazi wa maeneo hayo ambayo hutumia maji ya mtu huo kwa shughuli zao za kila siku.

Kutokana na hilo wakazi wa eneo hilo hulazimika kufanya usafi mara kwa mara na kulalamikia kukuta miiili ya vichanga ambayo hutupwa maeneo hayo kila wakati.

Baadhi ya wakazi hao walisema mto huo ambao chanzo chake kinatoka katika Mlima Meru ni muhimu kwao kutokana na maji yake kutumika kwa matumizi ya nyumbani na hata umwagiliaji wa mboga mboga.

“Unaweza kwenda kuteka maji ukakutana na mabaki ya miiili ya watoto huku wengine wakitupa taka kwa kukwepa kulipa ushuruwa takataka ambao ni shilingi 1000 kwa Halmashauri ya jiji.


MTANZANIA
Chama cha wamiliki wa Mabasi Tanzania TABOA kinakusudia kusitisha huduma za usafiri wa mabasi nchi nzima muda wowote kuanzia sasa,endapo madai yao ya msingi hayatashughulikiwa na mamlaka ya uthibiti wa usafiri wa nchi kavu na majini Sumatra.

Uamuzi wa kufikiwa kwa mgomo huo ambao unatarajiwa kusababisha tatizo la usafiri wakati huu wa kuelekea katika sikukuu za mwisho wa mwaka,ulifikishwa juzi katika mkutano mkuu wa TABOA uliofanyika jijini Dar es salaam.

Mweka Hazina wa Chama hicho Issa Nkya alisema mgomo huo una lengo la kuishinikiza SUMATRA ili isikilize kero zao ambazo zimedumu kwa muda mrefu sasa.

Alisema kitendo cha Sumatra kugoma kuhudhuria mkutano mkuu waChama hicho unaonyesha wazi namna ambavyo haiko tayari  kumaliza matatizo na wamiliki wa mabasi.

Alisema katika mkutano huo wamiliki wa mabasi wamelitaka Jeshi la Polisi na Sumatra kuacha kufungia makampuni pindi basi mojawapo linapopata ajali.


MWANANCHI
Serkali imeunda kamati ya watu10 kutoka kada tofauti wakiwamo viongozi wa dini ambao watapea jukumu la kufanya kazi ya usuluhishi kwenye vijiji vyenye migogoro baina ya wakulima na wafugaji Wilayani Kiteto Mkoani M anyara.

Waziri mkuu Mizengo Pinda alisema hayo jana wkaati akiwasilisha salamu za Serikali kwenye ibada ya kumweka wakfu Askofu wa sita wa Dayosisi ya Central Tanganyika ya kanisa la Anglikana Dk Dickson Chilongani lililofanyika kwenye kanisa kuu mjini Dodoma.

Alisema hali ya Kiteto si shwari na inahitajika ufumbuzi ili kuzuia mapigano na migogoro inayoendelea kwa sasa na kusema wameteua kamati maalum itakayokwenda kufanya usuluishi baina ya vijiji hivyo.

“Tunataka kutumia Kiteto kama mradi wa majaribio kwenye suala la kutafuta amani kwenye maeneo yake,watu wanauana kwa sababu ya ha sira,ni hasira ga ni hiyo inayokufanya mpaka uweze kuta roho ya mwenzako huu ni unyama lazima tusimame kidete”alisema Pinda.

Alhamisi, 20 Novemba 2014

MAGAZETI LEO TANZANIA 21/11/2014

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wa

POLISI MBEYA JELA KWA KUMUUA MWANAFUNZI

  Huu ni mwili wa Marehemu kijana Daniel Mwakyusa mara baada ya kufanyiwa uchunguzi baada ya kuuawa, Daniel alikuwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika chuo cha TEKU Mbeya, aliuawa na askari alipokutwa Univesal Pub siku ya Valentine day 2013, akiwa na mwanamke aliyesadikiwa kuwa alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na askari Maduhu.



 Mwili wa mwanafunzi huyo kabla ya kuzikwa mara baada ya kuagwa na ndugu,jamaa na marafiki.Jeshi la polisi liligharamia shughuli za maziko ya mwanafunzi huyo na hapo ndipo shitaka likaanza kuunguruma mahakamani.
                             
                        HABARI KAMILI
MAHAKAMA Kuu kanda ya Mbeya imemhukumu kunyongwa hadi kufa aliyekuwa askari wa jeshi la polisi F 5842 DC Maduhu aliyekuwa akikabiliwa na shitaka la mauaji ya mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU) Daniel Mwakyusa.
Aidha mahakama hiyo pia imewaaachia huru washitakiwa wengine wawili wa kesi hiyo F 7769 DC Shaban na WP 6545 DC Neema baada ya kuwakuta hawana hatia.
Hukumu hiyo ya kesi namba 16 ya mwaka 2013 imetolewa leo(Nov 19) na jaji Rose Temba baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na pande zote mbili.
Awali ilielezwa mahakamani hapo na mawakili wa serikali Archiles Mulisa akisaidiwa na Catherine Paul kuwa washitakiwa walifanya mauaji ya kukusudia mnamo Februari 14 mwaka 2012 kinyume cha kifungu namba 196 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002.
Kwa mujibu wa Wakili Mulisa washitakiwa hao kwa pamoja walihusika na mauaji ya Daniel Mwakyusa baada ya kumpiga marehemu huyo kwa kutumia silaha inayodhaniwa kuwa ni bunduki nje ya ukumbi wa starehe ujulikanao Univesal uliopo Uyole jijini Mbeya.
Akitoa hukumu ya kesi hiyo,jaji Temba amesema mshitakiwa namba moja DC Maduhu anahusika moja kwa moja na mauaji hayo kutokana na ushahidi wa kimazingira ikiwamo yeye kuwa mtu wa mwisho kuondoka na marehemu eneo la tukio na kumpeleka kwenye gari,risasi tatu kupungua kwenye bunduki yake na pia kuwa mtu wa mwisho kurejesha silaha kituoni.
 
Credit;lyamba lya mfipa blog

Jumatano, 19 Novemba 2014

MTOTO 1 KATI YA 9 WANAOZALIWA HAI TANZANIA NI NJITI


Vunja ukimya wa watoto njiti wa Tanzania!


Paza sauti yako kwa ajili yao!

 
Zaidi ya watoto 210,000 huzaliwa njiti Tanzania kila mwaka

Ni sawa na mtoto 1 kati ya kila watoto  9 wanaozaliwa hai Tanzania ni njiti

Watoto wachanga 9,400 hufariki kila mwaka kutokana na matatizo ya kuzaliwa njiti

Idadi hiyo ni sawa na karibu robo ya vifo vyote vya watoto wachanga 


 
Habari njema ni kuwa kuna njia rahisi zinazoweza kusaidia kuwaokoa wengi!
  •  matumizi ya njia za uzazi wa mpango;
  • uanzishaji mapema wa unyonyeshaji na unyonyeshaji maziwa ya mama pekee;
  • kuhakikisha watoto wanapewa joto la mwili hasa ngozi kwa mgozi baina ya mzazi na mtoto mchanga (njia hii inajulikana pia kama kangaroo mothercare);
  • uangalizi sahihi baada ya kuzaliwa, kujifungulia kwenye vituo vya afya na kuhakikisha mtoto anachunguzwa na wataalamu na kupata uangalizi sahihi baada ya kuzaliwa

TAHA YAHAMASISHA WAKULIMA WA MBOGAMBOGA KUTUMIA UWANJA WA NDEGE WA SONGWE


Ofisa Ufundi wa TAHA Isaac Ndamanhyilu akiwa katika moja ya mashamba ya Nyanya ambalo TAHA limesaidia mafunzo na teknolojia

Mkulima wa mbogamboga na matunda Daniel Wabare akiwaonesha wakulima wa mboga mboga na matunda namna ambavyo alifanikiwa katika kilimo cha Nyanya kwa msaada wa Shirika la TAHA

Mtaalamu wa kilimo kutoka TAHA kanda ya Mashariki Annania Bansimbile akiwaelekeza wakulima namna ambavyo umwagiliaji kwa mfumo wa matone unavyoleta tija kwa kilimo cha Mbogamboga na matunda

Katibu Tawala wa wilaya ya Mbarali Alfred Mzurikwao akiwapa nasaha wakulima kwenye kilele cha siku ya wakulima Shambani katika kijiji cha Ilaji wilayani Mbarali
Ofisa Ufundi TAHA Isaac Ndamanhyilu akiwapa zoezi la uelewa wakulima waliohudhuria katika maadhimisho ya siku ya wakulima Shambani katika kijiji cha Ilaji wilayani Mbarali.
 
WAKULIMA wa mbogamboga na matunda mkoani Mbeya wametakiwa kuutumia vyema uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Songwe kwa kuzalisha na kusafirisha  mazao yenye ubora ili waweze kujiinua kiuchumi.
 
 
Kauli hiyo imetolewa na Ofisa Ufundi wa Shirika lisilo la Kiserikali linalojihusisha na utaalamu na mafunzo ya uzalishaji mazao ya mbogamboga, matunda, maua na viungo (TAHA) Isaac  Ndamanhyilu  wakati wa kuadhimisha siku ya wakulima shambani kijiji cha Ilaji wilayani Mbarali mkoani Mbeya.
 
 
 Ndamanhyilu alisema kuwa wakulima wa mbogamboga, maua na matunda mkoani Mbeya wanayo fursa ya nzuri ya masoko kwa kuutumia uwanja wa Kimataifa wa Songwe kwa kushindana na masoko ya Kimataifa kuzalisha kwa ubora.
 
 
 
‘’Ardhi ya mkoa wa Mbeya ni rafiki kwa mazao yote, ikitumiwa vyema kwa kilimo cha mbogamboga na matunda itakuwa ni mkombozi wetu  kiuchumi,’’alisema.
 
 
Ndamanhyilu alisema kuwa kwa kuthamini mpango wa shirika hilo katika kuchangia maendeleo ya kilimo cha mbogamboga na matunda nchini serikali imetoa ruzuku ya sh.bilioni 1.4 ili kusukuma jitihada za wakulima kujiinua  na kuongeza tija.
 
 
Alisema matarajio ya TAHA ni kuongezeka kwa hamasa ya kilimo na matumizi ya teknolojia ya umwagiliaji na kilimo cha Matone kwa kutumia mfumo wa usambazaji maji kwa kutumia mpira katika matuta, ‘’Drip Irrigation’’ ambao humsaidia mkulima kuzalisha kwa tija.
 
 
Naye Mkulima wa mboga mboga katika kijiji cha Ilaji wilayani Mbarali Daniel Wabare alisema kuwa kwa kipindi kisichozidi miezi mitatu amemudu kuandaa shamba la nyanya kwa kutumia utaalamu unaozingatia vigezo vya maandalizi bora ya shamba la Mbogamboga.
 
 
Alisema ameweza kuandaa shamba la hekari moja kwa gharama ya sh milioni 2.5 ambapo anatarajia kukusanya zaidi ya sh. milioni 8 na kuwa mafanikio hayo yametokana na uchaguzi wa mbegu bora, maandalizi ya vitalu, matumizi ya mbolea, maji na dawa za kuulia wadudu.
 
 
Awali akizungumza katika maadhimisho hayo Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbarali Alfred Mzurikwao alisema kuwa wakulima wa mbogamboga na matunda wanapaswa kuzingatia utaalamu kutoka kwa maofisa ugani na kuwataka maofisa ugani kutokaa maofisini na badala yake watembelee mashambani kukutana na wakulima.
 
 
‘’Watumieni vyema maofisa ugani walioko katika maeneo yenu, nanyi maofisa ugani msikae maofisini watembeleeni wakulima ili mjue changamoto wanazokutana nazo katika kilimo,’’alisema.
 
 
credit; fasihi media inc

Ijumaa, 14 Novemba 2014

WAZIRI WA AFYA DKT SEIF RASHID MGENI RASMI KONGAMANO LA TISA LA NHIF NA WAANDISHI WA HABARI

Pichani juu ni Mgeni rasmi Waziri wa Afya,Dkt.Seif Rashid akizungumza wakati wa kuzindua kongamano la tisa la NHIF na Waandishi wa Habari,lililofanyika leo katika moja ya ukumbi wa Dodoma hotel mkoani humo,ambapo kauli mbiu ya kongamano hilo ni ''Tanzania na Huduma bora za matibabu inawezekana''.

Pichani ni baadhi ya Wadau mbalimbali na wanahabari wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye kombano hilo la siku mbili linalofanyika mkoani Dodoma.
Washiriki katika kongamano la tisa la NHIF na Waandishi wa Habari,lililofanyika leo Dodoma hotel ikiwa ni siku ya pili ya kilele chake huku likiwa limebeba kauli mbiu ''Tanzania na Huduma bora za matibabu inawezekana''.
 
Kongamano hilo lilizinduliwa jana na Waziri wa Afya Dkt Seif Rashid,ambapo pia Kabla ya uzinduzi wa kongamano hilo Wanahabari walishiriki kutembelea miradi mbalimbali ya afya,ikiwemo hopsitali ya Mkoa wa Dodoma pamoja na Kituo cha kisasa cha uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya binadamu kilichopo ndani ya chuo kikuu cha Dodoma (UDOM),ambacho imegharimu kiasi cha shilingi bilioni 36 zilizotolewa na NHIF,kituo hicho kinatarajiwa kuanza kazi rasmi mapema mwakani.
 
Picha kwa Hisani ya Michuzi Media Group

Alhamisi, 6 Novemba 2014

CCM MBEYA MJINI KUMPATA LEO KATIBU MWENEZI

KUTOKANA na kifo cha aliyekuwa katibu wa siasa na uenzi wa CCM wilaya ya Mbeya, Mjini, Emmanuel Mbuza, leo chama hicho kinatarajia nkufanya uchaguzi wa nafasi hiyo.

BREAKING NEWS......BASI LA KAMPUNI YA HAPPY NATION LAPINDUKA IGURUSI MBEYA

BASI la kampuni ya Happy Nation, limeripotiwa kupinduka asubuhi ya leo eneo la Igurusi wilayani Mbarali mkoani Mbeya, likitokea mjini Mbeya kwenda Dar es Salaam.

Abiria kadhaa wameripotiwa kujeruhiwa.

Taarifa zaidi tutaendelea kuwaletea. Endelea kutembelea mtandao huu wa www.marymwanjelwa.blogspot.com

BREAKING NEWS......BASI LA KAMBUNI YA HAPPY NATION LAPINDUKA IGURUSI MBEYA

BASI la kampuni ya Happy Nation, limeripotiwa kupinduka asubuhi ya leo eneo la Igurusi wilayani Mbarali mkoani Mbeya, likitokea mjini Mbeya kwenda Dar es Salaam.

Abiria kadhaa wameripotiwa kujeruhiwa.

Taarifa zaidi tutaendelea kuwaletea. Endelea kutembelea mtandao huu wa www.marymwanjelwa.blogspot.com

KfW YAWAFUMBUA WANAUME MBEYA,SASA WAHAMASIKA KUWASINDIKIZA WAKE ZAO WAJAWAZITO KLINIKI

 Meneja wa NHIF mkoani Mbeya Dk.Mohamed Kilolile akiwasilisha moja ya mada kwa watoa huduma wa KFW wakati wa semina iliyofanyika katika ukumbi wa Mtenda jijini Mbeya


MRADI wa Afya ya Mama na Mtoto(KfW) unaoendeshwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) kwa ufadhili wa benki ya maendeleo ya watu wa Ujerumani umewezesha wanaume kushiriki shughuli za uzazi kwa kuwasindikiza wake zao kliniki wanapokuwa wajawazito.

Hayo yamebainishwa na watoa huduma wa KFW walipohudhuria semina ya siku mbili ya mafunzo ya kuwajengea uwezo iliyofanyika jijini Mbeya.

Watoa huduma hao wanasema tofauti na awali hivi sasa kumekuwa na mwamko mkubwa wa wanaume kuongozana na wake zao kwenda kliniki  wanapokuwa wajawazito na kupata elimu kwa pamoja juu ya njia sahihi zinazotakiwa katika kumhudumia mama mjamzito.

“Kwa sasa wanaume wanashiriki kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na awali. Wanapenda kuongozana na wake zao ili wapate elimu kwa pamoja.

Tunaamini kupitia elimu tunayoitoa upitia KfW wamebadilika na wametambua kuwa wanawajibu pia wa kuhudhuria kliniki ili kupata tarifa sahihi za ujauzito wa wake zao” anasema mmoja wa watoa huduma hao Elizabeth Mwamlima kutoka zahanati ya kijiji cha Utulo wilayani Mbarali.

Mwamlima amesema kwa ushiriki huo wa wanaume hivi sasa familia zimekuwa zikijipanga mapema wakati wa ujauzito ili kuhakikisha mwanamke husika anapata huduma stahiki ikiwemo kupelekwa katika hospitali waliyoshauriwa na wataalamu mara wakati wa kujifungua unapowadia.

Amesema hali hiyo inawaepusha wanawake wajawazito kuepuka hatari ambazo zilikuwa zikiwakumba awali na kuhatarisha maisha yao na watoto wachanga wakati wa kujifungua na baada.

Kwa upande wake katibu wa Afya mkoa wa Mbeya Juliana Mawala amesema mradi wa KfW ambao kwa hapa nchini unaendeshwa katika mikoa miwili ya Mbeya na Tanga umeleta manufaa makubwa katika utatuzi wa changamoto za Afya za wajawazito na watoto wachanga.

Mawala amesema ni imani ya wadau wa afya kuwa ushiriki wa jamii katika utatuzi wa changamoto zinazowakabili wajawazito na watoto utakuwa endelevu hata baada ya ukomo wa KfW kwakuwa tayari wananchi wamepata uelewa juu ya umuhimu wa kuchangia na kuwekeza katika masuala ya afya.
credit

GAZETI MTANZANIA LEO NOVEMBA 6,2014.... KIKWETE APANGUA LALA SALAMA

Gazeti la Kiswahili linaloongoza Tanzania

Rais KikweteNa Bakari Kimwanga, Dodoma
RAIS Jakaya Kikwete amefanya uteuzi wa wakuu wapya wanne wa mikoa, huku akiwahamisha sita na wengine watatu kuwapangia kazi nyingine.
Taarifa ya Ikulu iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na kusainiwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, wakuu wapya wa mikoa walioteuliwa ni Halima Dendego anayekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Dk. Ibrahim Msengi, Katavi, Amina Masenza, Iringa na John Mongella, Kagera.
Taarifa hiyo ilisema kabla ya uteuzi huo, Halima Dendego alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Dk. Msengi,  Moshi, Masenza, Ilemela na Mongella Arusha Mjini.
“Wakuu hao wapya wa mikoa watahapishwa leo saa saba mchana, Ikulu, Dar es Salaam,” inasema taarifa hiyo.
Kazi mpya
Taarifa hiyo inasema kuwa, wakuu wa mikoa ambao watapangiwa kazi nyingine ni Kanali Mstaafu Fabian Massawe aliyekuwa Kagera, Dk. Christine Ishengoma,  Iringa na Kanali Joseph Simbakalia, Mtwara.
Vituo vipya
Wakuu wa Mikoa ambao wamehamishwa vituo vya kazi ni Magesa Mulongo kutoka Arusha kwenda Mwanza, Dk. Rehema Nchimbi Dodoma kwenda Njombe, Ludovick Mwananzila Lindi kwenda kwenda Tabora, Kepteni Mstaafu Anseri Msangi kutoka Njombe kwenda Mara na Everist Ndikilo Mwanza kwenda kwenda Arusha.
Wengine waliohamishwa ni Luteni Mstaafu Chiku Galawa kutoka Tanga kwenda Dodoma, Dk. Rajab Rutengwe Katavi kwenda Tanga, Fatma Mwasa, Tabora kwenda Geita, na Magalula S. Magalula, Geita kwenda Lindi.
“Wakuu wa Mikoa ya Dar es Salaam, Kigoma, Kilimanjaro, Manyara, Mbeya, Morogoro, Pwani, Rukwa, Shinyanga, Ruvuma, Singida na Simiyu watabakia kwenye vituo vyao vya sasa,” inaeleza taarifa hiyo.
Panga la makatibu wakuu
Rais Kikwete pia ameteua Makatibu Wakuu wapya wanne na kuhamisha mmoja.
Walioteuliwa ni Dk. Donan Mmbando atakayekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Yohana Budeba, Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhandisi Mbogo Futakamba, Wizara ya Maji na Dk. Adelhelm Meru, Wizara ya Utalii na Maliasili.
Kabla ya uteuzi huo Dk. Mmbando alikuwa Mganga Mkuu wa Serikali, Dk. Budeba, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Uvuvi na Mifugo, Mhandisi Futakamba, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maji na Dk. Meru, Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uwekezaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA).
Waliohamishwa ni Maimuna Tarishi kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii kwenda Wizara ya Katiba na Sheria.
Kuhusu uteuzi na uhamisho wa Makatibu Tawala wa Mikoa, Rais Kikwete amemteua Charles Pallangyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, Adoh Steven Mapunda, Mkurugenzi Mtendaji, Manispaa ya Bukoba kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Severine Kahitwa, Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro na Dk. Faisal Issa, Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza.
Wakati huo huo, Rais Kikwete amemteua Kanali Mstaafu Joseph Simbakalia, ambaye alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, kuwa Mkurugenzi Mkuu wa EPZA.
Uteuzi huo ulianza jana ambapo makatibu wakuu hao pamoja na makatibu tawala nao wataapishwa leo Ikulu, Dar es Salaam.
Pamoja na hili Rais Kikwete amefanya uteuzi wa Wakuu wapya wa Wilaya, kuhamisha baadhi yao na kutengua uteuzi wa baadhi ambapo taarifa  kamili itatolewa na Waziri Mkuu baada ya kuwa wamepangiwa vituo vya kazi

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...