TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 28.10.2014.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU MMOJA MKAZI
WA KIJIJI CHA SAMANGOMBE ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA SHIDA WILSON MAZWILE (35)
ALIUAWA KWA KUCHOMWA KISU TUMBONI BAADA YA KUVAMIWA NA MTU/WATU WASIOJULIKANA
AKIWA AMELALA NYUMBANI NA MKE WAKE MDOGO AITWAYE CHRISTINA SAITON TANDALA.
TUKIO HILO
LIMETOKEA MNAMO TAREHE 27.10.2014
MAJIRA YA SAA 00:01 USIKU HUKO
KATIKA KIJIJI CHA SAMANGOMBE, KATA NA TARAFA YA KAMSAMBA, WILAYA YA MOMBA, MKOA
WA MBEYA. CHANZO CHA MAUAJI HAYO BADO HAKIJAFAHAMIKA. JUHUDI ZA KUWATAFUTA
WATUHUMIWA WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI ZINAENDELEA.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE
MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO/WALIPO WATU WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI AZITOE
KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MTU MMOJA MKAZI
WA SENJELE WILAYA YA MBOZI ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA SEMENI SHANGU (22) ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA
GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.426 CXT
AINA YA YUTONG LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE BRUGE MZAVA (37) MKAZI WA SUMBAWANGA.
AJALI HIYO
IMETOKEA MNAMO TAREHE 27.10.2014
MAJIRA YA SAA 14:00 MCHANA HUKO KATIKA
KIJIJI CHA SENJELE, KATA YA MYOVIZI, TARAFA YA IYULA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA
MBEYA KATIKA BARABARA YA MBEYA/TUNDUMA. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI, DEREVA
AMEKAMATWA NA GARI LIPO KITUONI.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
MADEREVA NA WATUMIAJI WENGINE WA VYOMBO VYA MOTO KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO
HIVYO IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI
KUEPUKA AJALI ZINAZOEPUKIKA.
TAARIFA ZA MISAKO:
KATIKA
MSAKO WA KWANZA, MTU MMOJA AITWAYE EDAH
SING’OMBE (32) MKAZI WA
MACHINJIONI ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA POMBE YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 05
PAMOJA NA MTAMBO WA KUTENGENEZEA POMBE HIYO.
MTUHUMIWA
ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 27.10.2014
MAJIRA YA SAA 15:00 ALASIRI HUKO KATIKA
KIJIJI NA KATA YA MAKONGOLOSI, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA
MBEYA. MTUHUMIWA NI MPIKAJI NA MUUZAJI
WA POMBE HIYO, TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KATIKA
MSAKO WA PILI, MTU MMOJA AITWAYE JOSHUA
MWAKAJA (43) MFANYABIASHARA NA
MKAZI WA MAJENGO ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA POMBE
KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU AINA YA DOUBLE
PUNCH PAKETI 66.
MTUHUMIWA
ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 27.10.2014
MAJIRA YA SAA 15:30 ALASIRI HUKO
KATIKA MTAA WA MAJENGO, KIJIJI NA KATA YA MAKONGOLOSI, TARAFA YA KIWANJA,
WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA POMBE HIZO, TARATIBU
ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KATIKA
MSAKO WA TATU, MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ELIZABETH ERNEST (20)
MKAZI WA MAKONGOLOSI ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA POMBE YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 10.
MTUHUMIWA
ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 27.10.2014
MAJIRA YA SAA 14:30 MCHANA HUKO
KATIKA KITONGOJI CHA MACHINJIONI, KIJIJI NA KATA YA MAKONGOLOSI, TARAFA YA
KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA POMBE HIYO.
KATIKA
MSAKO WA NNE, MTU MMOJA MKAZI WA MKWAJUNI WILAYANI CHUNYA AITWAYE SHUGHULI SIX (30) ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA BHANGI UZITO WA ROBO KILO.
MTUHUMIWA
ALIKAMATWA NA KUKUTWA NA BHANGI HIYO MNAMO TAREHE
27.10.2014 MAJIRA YA SAA 17:00 JIONI
HUKO KATIKA KITONGOJI CHA KIKUYU, KIJIJI NA KATA YA MKWAJUNI, TARAFA YA KWIMBA,
WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA ALIKUTWA NA BHANGI HIYO BAADA YA
KUPEKULIWA KATIKA BANDA LAKE LA KUUZIA POMBE. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI
ZINAFANYIKA.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII
KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA [BHANGI], POMBE HARAMU YA MOSHI PAMOJA NA POMBE
KALI [VIROBA] ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA
NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANAENDELEA KUTOA WITO KWA WANANCHI KUTOA
TAARIFA ZA MTU/WATU AU MTANDAO WA WATU WANAOJIHUSISHA NA UUZAJI NA USAMBAZAJI
WA BIDHAA HARAMU ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.