KHADIJA
(MOSA) Juma Mrisho, anayeishi mitaani Jijini Dar es Salaam, anaomba msaada wa
kumpata mama yake mzazi aliyepo mkoani Mbeya.
Anahitaji
msaada huo kutokana na mateso anayoyapata mitaani, ikiwa ni pamoja na kutendewa
vitendo visivyo vya utu.
Kila
atakayeguswa kwa nia ya kumsaidia, hasa wenye vyombo vya habari vinavyosoma na
kusikika(redio), mkoani Mbeya, hapa chini ni waraka wa binti huyo, ambao
unaweza kusomwa au kuandikwa kwa nia ya kumuunganisha na mama yake.
NAMTAFUTA MAMA YANGU ANAYEITWA JANE
Jina langu naitwa Hadija na jina
langu la utoto naitwa Mosa. Jina la baba yangu anaitwa Juma Mrisho kabila lake
Mnyamwezi.
Mama yangu anaitwa Jane jina la baba
yake silikumbuki. Kabila la mama yangu ni muwanji,msafa.
Nilizaliwa Mwanjelwa, mkoani Mbeya
mwaka 1985.
Nilipofikisha umri wa miaka mitano(5)
baba na mama walitengana, nikachuliwa na baba yangu kwa njia ya kunitorosha
kutoka Mbeya akanipeleka Sikonge,Tabora
kwa bibi ambaye ni mama yake baba.
Bibi yangu anaitwa Hadija Iddi
Mhozya.
Baba aliniacha kwa bibi yangu na yeye akaondoka pasipo mimi kujua alikwenda
wapi sababu nilikuwa mdogo. Bibi yangu aliniambia baba yangu aliondoka kwenda
kutafuta maisha.
Sikuonana na baba yangu kwa muda wa
miaka mingi na badaye nilikuja kuonana
na baba mwaka 2008 Kibaha Dar es salaam, mimi wakati huo nikiwa na umri wa
miaka 23.
Lakini wakati huo wote nilikuwa
nikimwuliza bibi yangu mama yangu yuko wapi, bibi alikuwa akinieleza mama yangu
yuko mbeya anaitwa Jane.
Mwaka 2005 niliamua kwenda kumtafuta
mama yangu mbeya nikampata akiwa anaishi maeneo yanaitwa ILEMI DARAJANI,
Mwanjelwa , Mbeya .
Nilikaa na mama yangu muda wa wiki
moja nikaondoka. Baadaye mimi na bibi
tulihamia kwa baba kibaha nikaendelea kuishi na bibi baadaye bibi alifariki na
baadaye baba alifariki pia na mimi sikuwa na sehemu tena ya kuishi na sikupata nafasi ya kusoma shule,
ndipo nikaanza maisha ya taabu ya kujitafutia riziki mwenyewe.
Nimepitia mambo mengi ya taabu na
shida, kubezwa na kudharauliwa na jamii kwasababu ya maisha yangu
ninayoishi ya mitaani.
Sijawahi kupata msaada wowote kwa
ndugu wa baba yangu wala mama yangu kunitafuta.
Kwasababu ya maisha magumu
kuendelea ya kujitafutia riziki
mitaani mwenyewe sijaweza kupata fedha
ya kutosha nauli kwenda mbeya kumtafuta mama yangu kwa vile napata riziki ya kula tu.
Pia sina hakika kama mama yangu bado
yupo mbeya au alishahama au sijui kama yupo hai.
Nimeamua kumtafuta mama yangu kama
yupo hai ili tuweze kuishi pamoja, naumia kutomwona mama yangu na kutojua kama
bado anaishi au hapana.
Nimeamua kupitia redio hii kumtafuta.
Kama kuna mtu yeyote ambaye anajua mama yangu alipo au kama mama atapata
nafasi ya kusikia kwenye redio apige namba ifutatayo: 0764168544.
MAMA
NAKUTAFUTA NATESEKA hata kama uliolewa na mwanamume mwingine mimi ni mwanao nahitaji
tuwasiliane ni kuone mama.
Mimi Hadija (Moza) Juma Mrisho –
MWANAO MAMA NAKUTAFUTA NINA HUZUNI MNO KUKOSA BABA, MAMA.
Pia naishukuru hii kwa kunisaidia kurusha taarifa hii ili
nimpate mama.