Jumamosi, 29 Machi 2014
Jumatano, 26 Machi 2014
MAENDELEO YA UJENZI WA MRADI WA DARAJA LA KIGAMBONI
Meneja wa Mradi wa ujenzi wa daraja la
Kigambonio Bw. Lin Tao kutoka kampuni ya China
Railway Construction Engineering Group and
Major Bridge Co. Ltd (CRCEG-MBEC JV) akionesha jinsi ambavyo daraja la kigamboni litakavyoonekana
baada ya kukamilika.
Kulia kwake ni Mratibu wa Mradi kutoka Wizara ya
Miundombini Bw. Hussein Mativila.
Daraja hilo kutoka Kurasini mpaka Kigamboni
takribani kilometa moja litakuwa na njia sita kwa ajili ya magari.
Daraja hili linajengwa kwa ufadhili wa
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Shirika la Hifadhi ya Jamii
(NSSF)
Timu
ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango
wakipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa daraja la kigamboni kutoka kwa Bw
Lin Tao (katikati) kulia kwake (mwenye tai nyekundu) ni Naibu Katibu Mtendaji
wa Tume ya Mipango anayesimamia Kongane ya Sekta za Uzalishaji.
Wa kwanza kulia
(mwenye suti nyeusi) ni Meneja wa Mradi kutoka NSSF, Bw Karimu Mataka.
Mafundi
wa Kampuni ya ujenzi wa daraja la
Kigamboni wakisuka nondo katika moja ya nguzo zitakazoshika daraja hilo.
Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango anayesimamia Kongane ya Sekta za
Uzalishaji, Bw. Maduka Kessy akisisitiza jambo wakati wa ziara ya kukagua
ujenzi wa daraja la Kigamboni. Mbele yake ni Menaja wa Mradi kutoka Kampuni ya
ujenzi wa daraja hilo (CRCEG-MBEC JV).
Moja ya nguzo inayosukwa katikatika ya maji ya bahari huku kukiwa na bomba la
pembeni linalotoa maji nje ya eneo linalosukwa nondo na zege kali.
Mhandisi wa Mradi wa ujenzi wa daraja la Kigamboni, Aldelsomond Elthag kutoka Arab Consulting Engineers (katikati)
akifafanua jambo kwa Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Bw. Maduka Kessy
(mwenye tai nyekundu), kulia kwake ni
Mhandisi Omari Athumani kutoka Tume ya Mipango wakati wa kukagua maendeleo ya
ujenzi wa daraja hilo.
Mafundi wa Kampuni ya ujenzi wa
daraja la Kigamboni wakisuka nondo katika moja ya nguzo zitakazoshika daraja
hilo.
Picha
zote na Joyce Mkinga,
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Ofisi
ya Rais, Tume ya Mipango
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...