Nchemba katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CCm Ifunda |
NAIBU
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha,
Mwigulu Nchemba amewataka wabunge wa bunge maalumu la Katiba wanaotaka nyongeza
ya posho kujiondoa katika bunge hilo kama hawaridhiki nayo.
“Ndio
wachape mwendo; maana kuna wengine wanasema wana biashara zao zinawalipa zaidi
ya Sh 300,000 zinazotolewa kwa siku na serikali, ni vizuri wakaenda kusimamia
biashara zao,” alisema.
Akizindua
kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge katika jimbo la Kalenga kwa kumnadi mgombea
ubunge wa jimbo hilo kupitia CCM , Godfrey Mgimwa, Nchemba serikali haitawatendea
haki watanzania kama itakubaliana na matakwa ya baadhi ya wabunge wanaotaka nyongeza
ya posho.
“Nimekataa, sitakubali serikali iongeze posho
kwa kuzingatia sababu zilizotolewa na baadhi ya wabunge wanaotaka nyongeza
hiyo.”
Alisema
anajua kuwepo kwa kamati iliyokuwa ikilifanyia kazi suala hilo na mapendekezo
yake kuyawasilisha kwa Rais Jakaya Kiwete.
“Rais
ni mtu mwenye hekima na busara nyingi, amesikia kilio cha watanzania, anajua
hali ya kiuchumi ya taifa hili, anajua mahitaji mengine mengi ya watanzania kwa
kutumia rasilimali hizi hizi tulizonazo; ni lazima atatuomba ushauri sisi kama
wasaidizi wake,” alisema.
Alisema
posho wanayopewa wabunge hao inazingatia hali halisi ya nchi na kwamba
hatakubali iongezwe.
Alisema
badala ya kudai nyongeza ya posho, wabunge wanaoshiriki bunge hilo wanatakiwa
kuonesha uzalendo kwa kujisifu kupata fursa hiyo muhimu ili wawakilishe
watanzania wenzao kutengeneza sheria mama ya nchi.
“Ni
mambo ya uzalendo; nakumbuka nikiwa mdogo kuna watu walisikitika kukosa fursa
ya kwenda kupambana na Nduli Idd Amin wakati wavita ya Kagera, na wale
waliokwenda walifuraji na kuonesha ushajaa wao pamoja na kwamba maisha yao
yalikuwa hatarini,” alisema.
Alisema
watu wanaotaka kuikomboa nchi yao wakitanguliza maslai yao mbele ni hatari kwa
maendeleo ya Taifa.
Alisema
wabunge wa bunge maalumu la Katiba hawajakodishwa, hawafanyi kazi kama washauri
wataalamu, wanafanya kazi hiyo kwa niaba ya watanzania wengine wanaotaka kuona
nchi inakuwa na Katiba Mpya.
Alisema
wakati wabunge hao wakidai nyongeza ya posho wanasahau kwamba nchi hii ina
mambo mengi yanahitaji fedha ili isonge mbele.
“Wanajua
kwamba hatujalipa wakandarasi, wanajua kwamba walimu zaidi ya 36,000 wanaidai
serikali na wanajua kwamba kuna baadhi ya watumishi wa serikali wanapata kwa
mwezi chini ya kiwango wanacholipwa wao kwa siku,” alisema.
Alisema
ili nchi ipate maendeleo ni lazima mambo yote ya msingi yaendelee kufanyika kwa
kutumia rasilimali zilizopo.
“wanajua
wananchi wanahitaji mbolea ya ruzuku, maji, barabara, umeme, huduma nzuri za
afya, shule na mengine mengi” alisema.
Alisema
wanaona kiasi hicho hakiwatoshi na wana matumizi zaidi ya Sh 300,000 kwa siku
wakendelee na shughuli zinazowafanya wapate zaidi ya kiasi hicho.
Akimnadi
Godfrey Mgimwa, Nchemba alikishangaa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) kwa kuingia katika uchaguzi huo.
“Watanzania
lazima waelewe dhana ya uchaguzi mdogo; uchaguzi huu hauendi kubadili serikali,
serikali iliyopo ni ya CCM na inatekeleza Ilani yake,” alisema.
Alisema
wananchi walikwishatoa ridhaa mwaka 2010 kwa kuchagua mbunge na madiwani wote
wa CCM kwahiyo kinachofanyika katika uchaguzi huo ni kuziba nafasi.
“Haiwezekani
mchezaji wa Simba akatolewa uwanjani akaingizwa wa yanga au wa Yanga akatolewa
akaingizwa wa Simba; kwenye siasa hatuhitaji ushabiki, mpeni kura zenu mgombea
wa CCM kwasababu yeye ndiye anayetekeleza Ilani ya CCM,” alisema.
Alisema
CCM ina mkataba na wana Kalanga na imejipanga vyema kutekeleza Ilani yake kama
ilivyoahidi wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2010.
Alisema
hakuna litakalofanywa na mgombea wa Chadema katika kipindi kilichobaki kama
atachaguliwa kuwa mbunge wao.
“Mkimchagua
na mtakapomuuliza tena majibu yake yatakuwa yale yale, sijatekeleza ahadi zangu
kwasababu serikali ya nchi hii imeundwa na CCM,” alisema.
CREDIT; Bongo leaks
MWIGULU ALIVYOZINDUA KWA KISHINDO KAMPENI ZA CCM KALENGA.
Abdul
Adam, Mtoto wa Spika wa Bunge wa zamani Chifu Adamu Sapi Mkwawa,
akimpongeza mgombea wa CCM katika Uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga,
Iringa Vijijini, Godfrey Mgimwa, wakati wa mkutano wa uzinduzi rasmi wa
kampeni za CCM uliofanyika Viwanja vya Ifunda, Februari 27, 2014.
Wananchi
wakinyoosha mikono kuunga mkono kuwa mgombea wa CCM anafaa, wakati wa
mkutano wa uzinduzi rasmi wa kampeni za CCM uliofanyika Viwanja vya
Ifunda, Februari 27, 2014.
Naibu
Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Mwigulu Nchemba akionyesha makada wa CCM,
Alphonce John (kushoto) na Musa Tesha, walionusurika kuuawa na watu
wanaodaiwa kutumwa na Chadema kwa mmoja kumwagiwa tindikali na mwingine
kutobolewa jicho kwenye kampeni zinazohusu udiwani na Ubunge, katika
maeneo ya Igunga na Kahama, alipokuwa akieleza fuji za Chadema, wakati
wa mkutano wa uzinduzi rasmi wa kampeni za CCM uliofanyika Viwanja vya
Ifunda, Februari 27, 2014.
Alfonce aliyetobolewa jicho Kahama akizungumza jukwaani.
Mwigulu akihutubia, wakati wa mkutano wa uzinduzi rasmi wa kampeni za CCM uliofanyika Viwanja vya Ifunda, Februari 27, 2014.
Mwigulu
(4th) na mgombea wakitroti na Green Guard, wakati wa mkutano wa
uzinduzi rasmi wa kampeni za CCM uliofanyika Viwanja vya Ifunda,
Februari 27, 2014.
Katibu
wa CCM, wilaya ya Mufindi, Miraji Mtaturu, alionyesha mbao zenye
misumari inayodaiwa kutegwa njiani na Chadema, kwa nia ya kudhuru
msafara wa mgombea wa CCM ktk jimbo la Kalenga.
Katibu wa CCM mkoa wa Iringa, akishauriana jambo na Mwenyekiti wake Joyce Msavatavangu
Mjumbe
Kamati Kuu ya CCM, Pindi Chana, akitema cheche jukwaani, wakati wa
mkutano wa uzinduzi rasmi wa kampeni za CCM uliofanyika Viwanja vya
Ifunda, Februari 27, 2014.
Godfrey Mgimwa-Mgombea wa CCM uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga, Iringa.
Imetayarishwa na theNkoromo Blog