Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa -MB, akitoa mada
juu ya kumwezesha mwanamke na uongozi katika maamuzi kwenye Bunge la
ACP-EU Women Forum Brussels-Belgium Jumamosi tarehe 15/6/2013
****************************************************************************
UNAPOPATA
kujua historia za wanasiasa wanawake nchini Tanzania wanaofanya vizuri katika
majimbo ama mikoa yao, ni dhahili huwezi kukosa jina la Dr. Mary Mwanjelwa.
Mwanamke
huyo ni Mbunge wa Viti maalum kutokea mkoani Mbeya kupitia Chama Cha
Mapinduzi (CCM).
Sifa yake ya kwanza ni ucheshi ambao yeye anasema kuwa ucheshi
wake unatokana na wokovu alionao(kumcha Mungu).
Kabla ya
kujikita katika masuala ya siasa alikuwa Mkurugenzi wa shirika la PSI Tanzania
ambako historia haimuhukumu hata baada ya kutoka huko kwa kile kinachojieleza
kuwa alitoka na utumishi uliotukuka.
Katika mahojiano
na Mwandishi wa makala haya, Dr. Mary Mwanjelwa anasema kuwa alipata ubunge
kupitia viti maalum mwaka 2010.
Anasema kwa
sasa katika mkoa wa Mbeya, kuna wabunge wa viti maalum wawili ambao ni yeye na
Hilda Ngoye.
‘’Najivunia
nafasi niliyonayo maana imenipa na nafsi ya kuwa Mbunge wa Bunge la Ulaya
nikiwakilisha Tanzania’’ anasema Dr. Mwanjelwa.
Alipoulizwa kuwa
tangu achaguliwe kuwa Mbunge wa mkoa huo amefanya nini cha kujivunia mpaka
sasa, alisema ameweza kuwainua makundi mbalimbali hasa wanawake wa wilaya zote
za mkoa wa Mbeya.
Anasema anapenda
sana kushiriki katika shughuli za kimaendeleo za jumuiya na hata familia moja
moja.
‘’Kuanzia
mwaka 2010, kwa kukumbuka baadhi ya niliyoyafanya ni pamoja na kujumuika na
kuwasaidia yatima, kusaidia vikundi vya
akina mama na kufadhili semina za madiwani wa vyama vyote juu ya utendaji bora’’
anasema Dr. Mwanjelwa.
Elimu.
Anataja maeneo
ambayo amewahi kujumuika na jamii kuhusu elimu kuwa ni kushona sare za shule nguo na viatu kwa
watoto yatima 100 kata za Kambasegele na Kiwira wilayani Rungwe.
Anasomesha
watoto yatima 2 wa kike kila wilaya za mkoa wa Mbeya ambazo ni Mbeya mjini,
Kyela, Rungwe, Mbeya Vijijini, Mbarali, Chunya, Ileje na Mbozi.
Si hayo tu
bali nimesaidia ujenzi wa sekondari kata ya Itagano-Jiji la Mbeya, mifuko ya
saruji tani Moja, ujenzi wa sekondari ya kata ya Ruanda saruji tani Moja na niligawa
vitabu katika sekondari 9 zote za mkoa wa Mbeya, kila wilaya shule Moja na
Kugawa vitanda 19 katika hosteli ya wasichana Sekondari ya Isansa ’’ anasema
Mbunge huyo.
Ujasiliamali
Anasema amefanikiwa
kuanzisha vikundi vya ujasiriamali kwa kina mama kila wilaya -zote za mkoa wa
Mbeya na kufadhili Mashine za kutotolea
vifaranga na kutoa pesa za mitaji wilaya zote za mkoa wa Mbeya.
‘’Nilitoa
mafunzo ya ujasiriamali kwa kina mama juu ya incubators hizo nilizowafadhili
ili waweze kuendelea kujitegemea katika kukuza uchumi wao badala ya kuwa
wategemezi kila wakati na niliendesha mafunzo ya ujasiriamali kwa wana Mbeya
kwa kuzingatia jinsia’’ anasema Mbunge huyo.
Aliwezesha
kaya 300 mbuzi wawili wawili kaya -kata
ya Kambasegela na Kiwira wilayani Rungwe.
Afya
Anaeleza kuwa
ni mambo mengi ya jamii aliyoshiriki na mengine ameyasahau lakini anakumbuka
pia aligawa magodoro 250 katika hospital za serikali katika wadi za wazazi
wilaya ya Ileje, Mbozi, Chimala(Mbarali), Ruanda na hospitali ya Rufaa ya Mbeya
kitengo cha wazazi Meta Jijini Mbeya.
Aidha
anasema amegawa vitanda 19 katika hosteli ya wasichana Sekondari ya Isansa
iliyopo wilayani Mbozi, kutoa gari ya sinema katika Jiji la Mbeya juu ya
uelimishaji Umma katika Tiba kwa Kadi kupitia mfuko wa Bima ya afya ya
Taifa(NHIF).
Kushiriki kampeni
ya kufanya usafi katika Jiji la Mbeya.
‘’Nilitoa
vyakula katika vituo cha watoto yatima cha Iwambi na kugawa nguo na mablanketi
katika kituo cha watoto yatima cha Uyole vyote vya Jijini Mbeya’’ anasema Dr.
Mwanjelwa.
Sanjali
na vitu hivyo, anasema kuwa alitoa pia viti vya walemavu wa viungo
katika Jiji la Mbeya mbele ya Askofu kiongozi wa kanisa la Moravian
Tanzania Alinikisa Cheyo siku alipkuwa akimshukuru Mungu kwa kumponya na
mauti katika ajali mbaya aliyoipata mwaka jana 2012.
Uongozi.
Katika masuala
ya uongozi, anasema aliendesha na atazidi kufanya hivyo kwa kufadhili
mafunzo/semina za mara kwa mara kwa Madiwani wote wa Mkoa wa Mbeya, juu ya
Uongozi na uwajibikaji.
‘’Mbali na
mafunzo ya madiwani hao, nimewahi kuendesha mafunzo/semina kwa watendaji wote
wa ngazi ya kata juu ya Uongozi na uwajibikaji na nitazidi kufanya hivyo’’
anasema.
Anajipambanua
kuwa pia amewahi kuendesha mafunzo/semina kwa wenyeviti na makatibu wa umoja wa
wanawake wa chama chake UWT katika wilaya zote za mkoa wa Mbeya jinsi ya
Uongozi na Uwajibikaji.
Mbali na
kazi za kijamii, anasema mara kadhaa huwa anashiriki kazi za kusaidia vikundi,
waimbaji na hata makanisa ambapo hivi karibuni alitoa vyombo vya Muziki Kanisa
la Ruanda Moravian kwaya Kuu Jiji la Mbeya.
Mbali na
makanisa anaeleza kuwa anashiriki pia kusaidia michango mbali mbali ya kijamii
kama vile-michango misikitini, makanisani, matamasha, harambee n.k
Alipoulizwa kuwa
kuwa anapenda nini katika utumishi wake wa Ubunge, anasema anapendelea sana na
atazidi kuhimiza/kuhamasisha uanzishwaji wa vikundi vya aina mbali mbali vya ujasiriamali, Sanaa n.k. kwa
wa kina mama, vijana na wazee.
Kuhusu ajali
aliyoipata
Anasema kwa
sasa alirudi nyuma kidogo katika kufanya kazi hizo za kuikomboa jamii kiuchumi
kutokana na ajali mbaya aliyoipata mwaka jana 2012 katika mteremko wa mlima
Iwambi eneo la Mbalizi wilaya ya Mbeya ambayo ilisababisha kifo cha msaidizi
wake.
‘’Ajali mbaya
niliyopata mwaka jana ilinikwamisha mambo mengi nilikuwa nimepanga kuendelea
kuteketeleza Ilani ya CCM lakini namshukuru Mungu afya yangu inaimarika na
nitazidi kuwatumikia ndugu zangu wa Mbeya kutoka rohoni, ndivyo nilivyo asili
mwana jamii hata kabla sijawa Mbunge, Mungu anisaidie niwatumikie kwa maendeleo
na tukishirikiana wote vema tutajikomboa katika mengi’’ anasema Dr. Mary
Mwanjelwa.
Kuhusu
kugombea tena mwaka 2015, anasema kuwa Mungu akimpa kibali na afya njema
atagombea na anaamini sifa anazo za kuendelea kuwa Mbunge wa Jimbo ama viti
maalum.