Wanafunzi wa
Kidato cha Sita wa shule ya Sekondari ya Mwakaleli wakiwa kwenye picha
ya pamoja na Katibu wa NEC Siasa na Mahusiano ya Kimataifa Dk.Asha-Rose
Migiro na Mbunge wa Viti maalum wanawake mkoa wa Mbeya Dk.Mary
Mwanjelwa.
Mzee Issa Simion
akitoa salaam kwa niaba ya wazee wa Kijiji cha Katende na pia kushukuru
kwa Serikali na Chama Cha mapinduzi na pia kuelezea kero zinazohusu
wakazi wa kata ya Katende.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kijiji cha
Katende ambapo alihimiza sana kuwa makini na vyama vinavyojita vya
siasa kwani sasa vimeanza kupoteza muelekeo.
Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Mbeya, Dk.Mary Mwanjelwa akiwasalimia wakazi Katende
Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye picha ya pamoja na wazee wa
kijiji ambao walimpa heshima ya kuwa Mzee wa Katende na kumvisha
mgolole kama heshima ya mtu mzima.
Katibu wa NEC
Siasa na Mahusiano ya Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akiwa ameketi kwenye
mkeka unaojulikana kama Kalili aliopewa zawadi na wakina mama wa
Katende.
Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Katende na kuwaahidi
CCM inatekeleza ilani yake ya uchaguzi na kusema ahadi zilizoahidiwa
zitatimizwa.
Katibu Mkuu wa CCM aliwaambia wananchi hao kuwa lazima tuhoji serikali pesa za maendeleo kwa nini haziji kwa wakati.
chanzo;ccm blog
Ijumaa, 29 Novemba 2013
TAARIFA KWA UMMA
MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA MBEYA, DR. MARY MWANJELWA(CCM), ANAWATANGAZIA WANANCHI WA KATA YA IYUNGA NA NZOVWE JIJINI MBEYA, KUWA LEO TAREHE 29/11/2013, SAA TISA ALASIRI, ATAKUWA ENEO LA NJIA PANDA ITENDE.
MBUNGE ATAKUWA KATIKA SHUGHULI ZA KIKAZI KWA AJILI YA KUWAWEZESHA VIJANA WAENDESHA BODABODA KATIKA KIKUNDI CHAO.
NYOTE MNAKARIBISHWA.
IMETOLEWA NA;
OFISI YA HABARI NA MAHUSIANO YA MBUNGE DR. MARY MWANJELWA.
MBUNGE ATAKUWA KATIKA SHUGHULI ZA KIKAZI KWA AJILI YA KUWAWEZESHA VIJANA WAENDESHA BODABODA KATIKA KIKUNDI CHAO.
NYOTE MNAKARIBISHWA.
IMETOLEWA NA;
OFISI YA HABARI NA MAHUSIANO YA MBUNGE DR. MARY MWANJELWA.
MAKABILA YALIYOPO MKOANI MBEYA
1. Wanyakyusa
2. Wasafwa
3. Wamalila
4. Wandali
5. Wanyiha
6. Wakinga
7. Wabungu
8. Wanyamwanga na
9. Wasangu
Hali ya hewa katika mkoa wa Mbeya.
Mkoa una
hali ya hewa nzuri na ni milima milima katika baadhi ya wilaya zake.
Wilaya ya
Kyela ni Tambalale na kuna Joto.
Jumapili, 24 Novemba 2013
ZIARA YA KINANA KYELA MBEYA
Kulia ni katibu mkuu wa CCM Taifa, ndugu Abdulhaman Kinana akisalimiana na Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. MARY MWANJELWA mara baada ya kufika wilayani Kyela jana.
Kutoka kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Songwe mkoani Mbeya, Philipo Mulugo, Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa na Mbunge wa Jimbo la Kyela, Dr. Harrison Mwakyembe. Wakati wa ziara ya katibu mkuu wa CCM Taifa, aliyoianza mkoani Mbeya jana.
Kinana akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Rungwe Magharibi, Dr. David Mwakyusa.
Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Kyela, Dr. Mwakyembe akitoa ufafanuzi wa jambo kuhusu kivuko cha Itungi, ambacho kwa sasa hakifanyi kazi...
Chanzo; michuzi blog
Kutoka kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Songwe mkoani Mbeya, Philipo Mulugo, Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa na Mbunge wa Jimbo la Kyela, Dr. Harrison Mwakyembe. Wakati wa ziara ya katibu mkuu wa CCM Taifa, aliyoianza mkoani Mbeya jana.
Kinana akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Rungwe Magharibi, Dr. David Mwakyusa.
Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Kyela, Dr. Mwakyembe akitoa ufafanuzi wa jambo kuhusu kivuko cha Itungi, ambacho kwa sasa hakifanyi kazi...
Chanzo; michuzi blog
Ijumaa, 22 Novemba 2013
WILAYA ZA MKOA WA MBEYA
MKUU WA MKOA WA MBEYA ABBAS KANDORO
Baadhi
ya wakuu wa wilaya za mkoa wa Mbeya, wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa mkoa wa
Mbeya Bw. Abbas Kandoro pamoja na aliyekuwa Katibu tawala wa mkoa Bi. Mariam
Mtunguja, pamoja na baadhi ya waandishi wa habari, mara baada ya kuapishwa.
1. Kyela
2. Rungwe
3. Ileje
4. Momba
5. Mbozi
6. Chunya
7. Mbeya Vijijini
8. Mbeya Mjini
9. Mbarali
Alhamisi, 21 Novemba 2013
UJUMBE WANGU LEO KWENU; WARUMI 12;14-18
WABARIKINI wanaowaudhi; barikini wala msilaani. Furahini pamoja nao wafurahio; lieni pamoja nao waliao.+ Mpatane nia zenu ninyi kwa ninyi. Msinie yaliyo makuu, lakini mkubali kushughulishwa na mambo manyonge, msiwe watu wa kujivunia akili.
Msimlipe mtu ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote. Kama yamkini, kwa upande wenu, mkae katika amani na watu wote.
Msimlipe mtu ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote. Kama yamkini, kwa upande wenu, mkae katika amani na watu wote.
DR. MARY MWANJELWA; MWANAMKE SHUPAVU WA SIASA ZA VITENDO
Na,
Marymwanjelwa Reporter-Mbeya
UNAPOPATA
kujua historia za wanasiasa wanawake nchini Tanzania wanaofanya vizuri katika
majimbo ama mikoa yao, ni dhahili huwezi kukosa jina la Dr. Mary Mwanjelwa.
Mwanamke
huyo ni Mbunge wa Viti maalum kutokea mkoani Mbeya kupitia Chama Cha Mapinduzi
(CCM).
Sifa yake ya
kwanza ni ucheshi ambao yeye anasema kuwa ucheshi wake unatokana na wokovu
alionao(kumcha Mungu).
Kabla ya
kujikita katika masuala ya siasa alikuwa Mkurugenzi wa shirika la PSI Tanzania
ambako historia haimuhukumu hata baada ya kutoka huko kwa kile kinachojieleza
kuwa alitoka na utumishi uliotukuka.
Katika
mahojiano na Mwandishi wa makala haya, Dr. Mary Mwanjelwa anasema kuwa alipata
ubunge kupitia viti maalum mwaka 2010.
Anasema kwa
sasa katika mkoa wa Mbeya, kuna wabunge wa viti maalum wawili ambao ni yeye na
Hilda Ngoye.
‘’Najivunia
nafasi niliyonayo maana imenipa na nafsi ya kuwa Mbunge wa Bunge la Ulaya
nikiwakilisha Tanzania’’ anasema Dr. Mwanjelwa.
Alipoulizwa
kuwa tangu achaguliwe kuwa Mbunge wa mkoa huo amefanya nini cha kujivunia mpaka
sasa, alisema ameweza kuwainua makundi mbalimbali hasa wanawake wa wilaya zote
za mkoa wa Mbeya.
Anasema
anapenda sana kushiriki katika shughuli za kimaendeleo za jumuiya na hata
familia moja moja.
‘’Kuanzia
mwaka 2010, kwa kukumbuka baadhi ya niliyoyafanya ni pamoja na kujumuika na
kuwasaidia yatima, kusaidia vikundi vya
akina mama na kufadhili semina za madiwani wa vyama vyote juu ya utendaji
bora’’ anasema Dr. Mwanjelwa.
Elimu.
Anataja
maeneo ambayo amewahi kujumuika na jamii kuhusu elimu kuwa ni kushona sare za shule nguo na viatu kwa
watoto yatima 100 kata za Kambasegele na Kiwira wilayani Rungwe.
Anasomesha
watoto yatima 2 wa kike kila wilaya za mkoa wa Mbeya ambazo ni Mbeya mjini,
Kyela, Rungwe, Mbeya Vijijini, Mbarali, Chunya, Ileje na Mbozi.
Si hayo tu
bali nimesaidia ujenzi wa sekondari kata ya Itagano-Jiji la Mbeya, mifuko ya
saruji tani Moja, ujenzi wa sekondari ya kata ya Ruanda saruji tani Moja na
niligawa vitabu katika sekondari 9 zote za mkoa wa Mbeya, kila wilaya shule
Moja na Kugawa vitanda 19 katika hosteli ya wasichana Sekondari ya Isansa ’’
anasema Mbunge huyo.
Ujasiliamali
Anasema
amefanikiwa kuanzisha vikundi vya ujasiriamali kwa kina mama kila wilaya -zote
za mkoa wa Mbeya na kufadhili Mashine za
kutotolea vifaranga na kutoa pesa za mitaji wilaya zote za mkoa wa Mbeya.
‘’Nilitoa
mafunzo ya ujasiriamali kwa kina mama juu ya incubators hizo nilizowafadhili
ili waweze kuendelea kujitegemea katika kukuza uchumi wao badala ya kuwa
wategemezi kila wakati na niliendesha mafunzo ya ujasiriamali kwa wana Mbeya
kwa kuzingatia jinsia’’ anasema Mbunge huyo.
Aliwezesha
kaya 300 mbuzi wawili wawili kaya -kata
ya Kambasegela na Kiwira wilayani Rungwe.
Afya
Anaeleza
kuwa ni mambo mengi ya jamii aliyoshiriki na mengine ameyasahau lakini
anakumbuka pia aligawa magodoro 250 katika hospital za serikali katika wadi za
wazazi wilaya ya Ileje, Mbozi, Chimala(Mbarali), Ruanda na hospitali ya Rufaa
ya Mbeya kitengo cha wazazi Meta Jijini Mbeya.
Aidha
anasema amegawa vitanda 19 katika hosteli ya wasichana Sekondari ya Isansa
iliyopo wilayani Mbozi, kutoa gari ya sinema katika Jiji la Mbeya juu ya
uelimishaji Umma katika Tiba kwa Kadi kupitia mfuko wa Bima ya afya ya
Taifa(NHIF).
Kushiriki kampeni ya kufanya usafi
katika Jiji la Mbeya.
‘’Nilitoa
vyakula katika vituo cha watoto yatima cha Iwambi na kugawa nguo na mablanketi
katika kituo cha watoto yatima cha Uyole vyote vya Jijini Mbeya’’ anasema Dr.
Mwanjelwa.
Sanjali na
vitu hivyo, anasema kuwa alitoa pia viti vya walemavu wa viungo katika Jiji la
Mbeya mbele ya Askofu kiongozi wa kanisa la Moravian Tanzania Alinikisa Cheyo
siku alipkuwa akimshukuru Mungu kwa kumponya na mauti katika ajali mbaya
aliyoipata mwaka jana 2012.
Uongozi.
Katika
masuala ya uongozi, anasema aliendesha na atazidi kufanya hivyo kwa kufadhili
mafunzo/semina za mara kwa mara kwa Madiwani wote wa Mkoa wa Mbeya, juu ya
Uongozi na uwajibikaji.
‘’Mbali na
mafunzo ya madiwani hao, nimewahi kuendesha mafunzo/semina kwa watendaji wote
wa ngazi ya kata juu ya Uongozi na uwajibikaji na nitazidi kufanya hivyo’’
anasema.
Anajipambanua
kuwa pia amewahi kuendesha mafunzo/semina kwa wenyeviti na makatibu wa umoja wa
wanawake wa chama chake UWT katika wilaya zote za mkoa wa Mbeya jinsi ya
Uongozi na Uwajibikaji.
Mbali na
kazi za kijamii, anasema mara kadhaa huwa anashiriki kazi za kusaidia vikundi,
waimbaji na hata makanisa ambapo hivi karibuni alitoa vyombo vya Muziki Kanisa
la Ruanda Moravian kwaya Kuu Jiji la Mbeya.
Mbali na
makanisa anaeleza kuwa anashiriki pia kusaidia michango mbali mbali ya kijamii
kama vile-michango misikitini, makanisani, matamasha, harambee n.k
Alipoulizwa
kuwa kuwa anapenda nini katika utumishi wake wa Ubunge, anasema anapendelea
sana na atazidi kuhimiza/kuhamasisha uanzishwaji wa vikundi vya aina mbali mbali vya ujasiriamali, Sanaa n.k. kwa
wa kina mama, vijana na wazee.
Kuhusu ajali aliyoipata
Anasema kwa
sasa alirudi nyuma kidogo katika kufanya kazi hizo za kuikomboa jamii kiuchumi
kutokana na ajali mbaya aliyoipata mwaka jana 2012 katika mteremko wa mlima
Iwambi eneo la Mbalizi wilaya ya Mbeya ambayo ilisababisha kifo cha msaidizi
wake.
‘’Ajali
mbaya niliyopata mwaka jana ilinikwamisha mambo mengi nilikuwa nimepanga
kuendelea kuteketeleza Ilani ya CCM lakini namshukuru Mungu afya yangu
inaimarika na nitazidi kuwatumikia ndugu zangu wa Mbeya kutoka rohoni, ndivyo
nilivyo asili mwana jamii hata kabla sijawa Mbunge, Mungu anisaidie niwatumikie
kwa maendeleo na tukishirikiana wote vema tutajikomboa katika mengi’’ anasema
Dr. Mary Mwanjelwa.
Kuhusu
kugombea tena mwaka 2015, anasema kuwa Mungu akimpa kibali na afya njema
atagombea na anaamini sifa anazo za kuendelea kuwa Mbunge wa Jimbo ama viti
maalum.
MAREKEBISHO.
* Blogu hii inafanyiwa marekebisho madogo ili kuendana na wakati.
* Asante kwa kuendelea kutembelea.
**Mungu awabariki.
Imetolewa na uongozi wa uendeshaji wa blogu hii ya www.marymwanjelwa.blogspot.com
Jumatano, 20 Novemba 2013
MBEYA REGIONAL DOMESTIC TOURISM
APART Mbozi Meteorite, Kitulo National Park and Lukwati in Mbeya there are also other tourism attractions which have not been publicities and declared as Domestic tourism attractions......
IJUE MBEYA
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...