Ijumaa, 5 Januari 2018

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya ulinzi ya Wilaya ya Mbarali wakati wa ziara yake ya kikazi kukagua shughuli za maendeleo, Jana Januari 4, 2018. Picha Zote Na Mathias Canal
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mhe Reuben Mfune mara baada ya kuwasili wilayani humo kwa ziara ya kikazi ya siku moja, Jana Januari 4, 2018. 
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisalimiana na Viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Mbarali mara baada ya kuwasili wilayani humo kwa ziara ya kikazi ya siku moja, Jana Januari 4, 2018. 
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya ulinzi ya Wilaya ya Mbarali wakati wa ziara yake ya kikazi kukagua shughuli za maendeleo, Jana Januari 4, 2018

Na Mathias Canal, Mbeya

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa amemuagiza Mrajis Mkuu wa Maendeleo ya Ushirika nchini kuanza uchunguzi mara moja kwenye SACCOS ya Wakulima wa mpunga Madibila iliyoko Wilayani Mbarali, Mkoani Mbeya ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya Watendaji waliohusika na upotevu wa fedha pamoja na matumizi mabaya ya madaraka.

Mhe Mwanjelwa alitoa agizo hilo Jana Disemba 4, 2018 wakati akipokea taarifa ya kilimo ya Wilaya ya Mbarali akiwa katika ziara yake ya kikazi Wilayani humo.

Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mhe Reuben Mfune alimueleza Mhe Mwanjelwa kuwa katika SACCOS ya Madibila kumekuwa na hasara kubwa kutokana na matumizi mabaya ya madaraka kwa baadhi ya viongozi wa vyama vya ushirika.

Hivyo alimuomba Naibu Waziri kuwachukulia hatua za kinidhamu haraka viongozi wote waliosababisha hasara kwenye vyama hivyo vya ushirika baada ya uchunguzi kufanyika katika kipindi cha siku 14.

Aliongeza kuwa taarifa ya ukaguzi iliwasilishwa kwa Mrajis wa vyama vya ushirika kwa barua Kumb Na. MDC/C.20/10/89 tarehe 23/01/2017 lakini mpaka sasa hazijachukuliwa hatua zozote za kinidhamu jambo ambalo linafifihisha shughuli za wananchi kujipatia maendeleo endelevu.

Naibu Waziri Mhe Mwanjelwa ametoa wiki mbili (siku 14) kwa Mrajis kufika katika SACCOS hiyo ya Madibira na kutoa majibu haraka ya matokeo ya uchunguzi huo katika kipindi tajwa.

Mhe Mwanjelwa alisema kuwa sekta ya ushirika ni moja kati ya sekta muhimu katika kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja, Vikundi, Wilaya, Mkoa na Taifa kwa ujumla katika kukuza pato la mwananchi na kupunguza umasikini hivyo ni lazima kuwa na majibu ya haraka pindi kunapobainika uhujumu wa vyama hivyo.

Alisema kuwa Viongozi wa Wilaya zote nchini wana jukumu muhimu la kuhamasisha na kuhiza wanachama kuongeza thamani ya mitaji yao ili kuviwezesha vyama kukuza mitaji ya ndani badala ya kuwa tegemezi kwenye Taasisi zingine za kifedha.

Aidha, Kuendelea kutoa elimu juu ya mfumo wa stakabadhi ya Mazao ghalani ili mkulima apate bei stahiki ya Mazao yake.

Jumatano, 3 Januari 2018

NAIBU MEYA JIJI LA MBEYA (CHADEMA) AAHIDI USHIRIKIANO NA WATEULE WA RAIS MAGUFULI AMSIFU MHE MWANJELWA KUSHIRIKIANA NA VYAMA VYA UPINZANI

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Mtaa wa Kagwina Kata ya Sinde Jana Januari 2, 2018. Picha Zote Na Mathias Canal
Naibu Meya wa Jiji la Mbeya Mhe Fanuel Kyanula ambaye ni Diwani wa Kata ya Sinde akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa katika Mtaa wa Kagwina Kata ya Sinde Jana Januari 2, 2018
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua hatua zilizofikiwa katika ujenzi wa Vyumba vya madarasa Shule ya Sekondari Sinde kabla ya kuzungumza na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Mtaa wa Kagwina Kata ya Sinde Jana Januari 2, 2018
Baadhi ya wananchi wakimlaki Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa mara baada ya kuwasili kwa ajili ya Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Mtaa wa Kagwina Kata ya Sinde Jana Januari 2, 2018.
Diwani wa Kata ya Manda Mkoani Mbeya Mhe Newton Mwakijobe akitoa salamu za wananchi wa Kata yake kwenye mkutano wa wananchi wa kata jirani ya Sinde kabla ya Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa kuzungumza na wananchi waliohudhuria kwenye mkutano huo Jana Januari 2, 2018

Na Mathias Canal, Mbeya

IMEBAINIKA kuwa tofauti za kiitikadi baina ya madiwani katika Halmashauri nyingi  nchini, zimekuwa ni kikwazo kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo yenye tija kubwa kwa wananchi.
Tofauti hizo zimekuwa chanzo kikubwa katika utekelezaji wa miradi inayobuniwa na Halmashauri husika, au inayoletwa na Serikali Kuu na wafadhili. Mitazamo ya kisiasa, tofauti ya uwakilishi wa vyama na ubinafsi, ndio sababu kuu.
Katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya inayoongozwa na Meya na Naibu Meya wanaotokana na vyama vya upinzania hali imekuwa tofauti kwani asilimia kubwa ya madiwani wanaunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli tofauti kabisa na Halmashauri zingine.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa Jana 2 Januari 2018 uliofanyika katika Mtaa wa Kagwina, Kata ya Sinde Naibu Meya wa Jiji la Mbeya Mhe Fanuel Kyanula ambaye ni Diwani wa Kata ya Sinde alisema kuwa utendaji wa Rais Magufuli ni faida ya watanzania wote hivyo kuna kila sababu ya wananchi kuunga mkono juhudi za serikali yake.
Kyanula alisema kuwa pamoja na kuwa kiongozi anayetokana na chama cha upinzani lakini serikali ni moja hivyo anaungana na wateule wote wa Rais Magufuli katika kutekeleza dhamira ya serikali ya kuwaletea wananchi maendeleo huku akimtaja Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa kama kiongozi wa mfano katika Mkoa wa Mbeya hivyo kuahidi kushirikiana nae kwa karibu.
Naibu Meya huyo amempongeza Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa kwa kuchangia jumla ya mifuko 40 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya Sekondari Iyera (Mifuko 20) na Shule ya Sekondari Sinde (Mifuko 20) zilizopo Jijini Mbeya.
Alimtaja Mhe Mwanjelwa kwamba amekuwa mwalimu mzuri wa somo la Uraia Mkoani Mbeya akifundisha kuhusu umoja na mshikamano huku akisisitiza kuwa Maendeleo ni dhana pana kwa wananchi na hayapaswi kufanywa kwa mipaka ya vyama vya siasa.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa yupo ziarani Mkoani Mbeya ambapo amesifu Uongozi wa Wilaya ya Mbeya kwa kazi kubwa katika utendaji ikiwemo kuanza mchakato wa ujenzi wa vyumba vya madarsa ili kuikabili changamoto ya wingi wa wananfunzi waliofaulu kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2018.

Jumanne, 2 Januari 2018

DIWANI WA CHADEMA MBEYA ASIFU UTENDAJI WA RAIS MAGUFULI, MHE MWANJELWA AONGOZA MAOMBI KWA AJILI YA RAIS NA SERIKALI

Diwani wa Kata ya Sinde Mkoani Mbeya Mhe Newton Mwakijobe akizungumza mbele ya waumini wakati wa ibada ya Mwaka Mpya iliyofanyika katika kanisa La Huduma ya Maombezi na Uponyaji (Jesus Healing Centre T. Ministry) lililopo Katika Mtaa wa Sinde B, Kata ya Manga Jijini Mbeya, Jana Januari Mosi, 2017. Picha Zote Na Mathias Canal
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akiongoza waumini wa kanisa La Huduma ya Maombezi na Uponyaji (Jesus Healing Centre T. Ministry) lililopo Katika Mtaa wa Sinde B, Kata ya Manga Jijini Mbeya kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli na serikali yake wakati wa ibada ya Mwaka Mpya, 2017.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisalimiana na Diwani wa Kata ya Sinde Mkoani Mbeya Mhe Newton Mwakijobe wakati wa ibada ya Mwaka Mpya iliyofanyika katika kanisa La Huduma ya Maombezi na Uponyaji (Jesus Healing Centre T. Ministry) lililopo Katika Mtaa wa Sinde B, Kata ya Manga Jijini Mbeya, Jana Januari Mosi, 2017.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akiongoza waumini wa kanisa La Huduma ya Maombezi na Uponyaji (Jesus Healing Centre T. Ministry) lililopo Katika Mtaa wa Sinde B, Kata ya Manga Jijini Mbeya kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli na serikali yake wakati wa ibada ya Mwaka Mpya, 2017.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akiongoza waumini wa kanisa La Huduma ya Maombezi na Uponyaji (Jesus Healing Centre T. Ministry) lililopo Katika Mtaa wa Sinde B, Kata ya Manga Jijini Mbeya kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli na serikali yake wakati wa ibada ya Mwaka Mpya, 2017.

Na Mathias Canal, Mbeya

Diwani wa Kata ya Manda Wilaya na Mkoa wa Mbeya Mhe Newton Mwakijobe amesifu Utendaji wa serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwa kuwatetea wanyonge huku akisimamia nidhamu na uwajibikaji kazini.

Diwani Huyo ametoa pongezi hizo wakati akitoa salamu wakati wa ibada ya Mwaka Mpya iliyofanyika katika kanisa La Huduma ya Maombezi na Uponyaji (Jesus Healing Centre T. Ministry) lililopo Katika Mtaa wa Sinde B, Kata ya Manga Jijini Mbeya.

Katika ibada hiyo iliyohudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa, Diwani Huyo amesifu zaidi usimamizi madhubuti wa rasilimali za Taifa unaofanywa na Rais Magufuli ambao utawanufaisha wananchi wote si MTU mmoja mmoja.

Mhe Mwakijobe pia amempongeza Rais Magufuli kwa kumchagua Mhe Mwanjelwa katika serikali yake kuwa Naibu Waziri anayeshughulikia sekta ya Kilimo jambo ambalo limeonyesha chachu na hamasa ya kuwakumbuka wakazi wa Mbeya Mjini kwa kupata Waziri wa kwanza tangu nchi ilipopata Uhuru.

Aidha, Mhe Mwakijobe alimsihi Mhe Mwanjelwa kumfikishia salamu Rais Magufuli ikiwa ni pamoja na kumuomba kuzuru Mkoani Mbeya katika ziara yake ya kikazi ili kuzungumza na wananchi wa Mkoa wa Mbeya ambao wanatambua majukumu makubwa na mazito anayoyafanya kwa manufaa ya wananchi wote.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo aliongoza waumini wa kanisa la Huduma ya Maombezi na Uponyaji (Jesus Healing Centre T. Ministry) kumuombea Rais Magufuli sambamba na serikali kwa ujumla ili wananchi waendelea kujivunia matunda ya kiongozi Huyo makini na shupavu.

Mhe Mwanjelwa Alisema kuwa maombi hayo ni kwa ajili ya kumshukuru Mungu, kwa kuwawezesha kumpata Rais John Magufuli, ambaye amekuwa akiibua na kufichua maovu mbalimbali yaliyokuwa yakitendeka nchini.

Aliongeza kuwa, juhudi alizozionyesha Mhe Rais Magufuli zinafaa kuungwa mkono na jamii yenye hofu na Mungu kwani ndani yake kuna mtihani mgumu unaohitaji kumuweka kwenye maombi ya wananchi ya kila siku katika sehemu yeyote iwe kazi na hata majumbani.

Kanisa hilo pia limefanya ibada maalumu kwa ajili ya Mhe Mwanjelwa ili awe kiongozi shupavu mwenye maono na utendaji uliotukuka katika serikali na aweze kuwa muwakilishi mzuri wa wananchi wa Mkoa wa Mbeya na Taifa kwa Ujumla wake.

Jumapili, 31 Desemba 2017

DIWANI WA CHADEMA MBEYA ASIFU UTENDAJI WA RAIS MAGUFULI, MHE MWANJELWA AONGOZA MAOMBI KWA AJILI YA RAIS NA SERIKALI

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua Maabara ya Kutazama kiwango cha Uotaji wa Mbegu wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Morogoro alipotembelea Taasisi ya Udhibiti wa Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI), Jana 30 Disemba 2017. Picha Zote Na Mathias Canal
 Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akizungumza na wafanyakazi wa Taasisi ya Udhibiti wa Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Morogoro, Jana 30 Disemba 2017. 
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua Maabara ya Kutazama kiwango cha Uotaji wa Mbegu Mkoani Morogoro wakati wa ziara yake ya kikazi alipotembelea Taasisi ya Udhibiti wa Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI), Jana 30 Disemba 2017.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na wafanyakazi wa Taasisi ya Udhibiti wa Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) Mkoani Morogoro wakati wa ziara yake ya kikazi, Jana 30 Disemba 2017. 

Na Mathias Canal, Morogoro

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa, Jana 30 Disemba 2017 ametangaza KIAMA kwa wafanyabiashara wa mbegu  nchini wanaouza Mbegu feki zilizopigwa marufuku na serikali.

Amewataka wafanyabiashara wote wa mbegu ambao wamekuwa wakifanya biashara hiyo kwa kuwauzia wakulima mbegu feki zilizopigwa marufuku na serikali kuacha haraka iwezekanavyo kwani serikali itawachukulia hatua za kisheria wale wote watakaobainika kukiuka maagizo ya serikali.

Ametoa agizo hilo akiwa ziarani Mkoani Morogoro ambapo pamoja na mambo mengine alitembelea Taasisi ya Udhibiti wa Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI), Taasisi iliyopewa jukumu na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania la usajili wa wafanyabiashara wa mbegu (Seed Dealers).

"Serikali imepokea malalamiko mengi kwa wananchi kuhusu Ubovu wa mbegu jambo ambalo limepelekea kwa kiasi kikubwa kuwa na mavuno kidogo pasina kukidhi matakwa ya wakulima wetu nchini" Alikaririwa Mhe Mwanjelwa

Naibu Waziri huyo pia ameiagiza Taasisi ya udhibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) kujitathmini kwa utendaji duni kwani wameshindwa kutimiza majukumu yao kwa kuwabaini wafanyabiashara wanaokiuka maagizo ya serikali pamoja na taratibu na sheria za nchi.

Ijumaa, 29 Desemba 2017

MHE MWANJELWA ATOA SIKU MOJA KWA WAFANYABIASHARA WALIOFUNGA MAGHALA YA MBOLEA KUYAFUNGUA LA SIVYO KUNYANG'ANYWA LESENI

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa (Katikati) akikagua mbegu zilizohifadhiwa ghalani kabla ya kuanza kusambazwa alipotembelea Wakala wa mbegu za kilimo (Agricultural Seeds Agency-ASA) wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Morogoro, Leo 29 Disemba 2017. Wengine ni Kaimu Mkurugenzi Wakala wa Mbegu Dkt Sophia Kashenge Kilenge (Kulia) na Meneja uzalishaji Wakala wa Mbegu Ndg Charles Levi (Kushoto). Picha Zote Na Mathias Canal 
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisalimiana na Mkurugenzi Wakala wa Mbegu Dkt Sophia Kashenge Kilenge alipotembelea Wakala wa mbegu za kilimo (Agricultural Seeds Agency-ASA) wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Morogoro, Leo 29 Disemba 2017.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo baada ya kukagua baadhi ya mashine za mbegu alipotembelea Wakala wa mbegu za kilimo (Agricultural Seeds Agency-ASA) wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Morogoro, Leo 29 Disemba 2017. 
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua namna mbegu za mazao mbalimbali zilivyohifadhiwa alipotembelea Wakala wa mbegu za kilimo (Agricultural Seeds Agency-ASA) wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Morogoro, Mwingine ni Kaimu Mkurugenzi Wakala wa Mbegu Dkt Sophia Kashenge Kilenge (Kushoto). Leo 29 Disemba 2017. 

Na Mathias Canal, Morogoro

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa leo Disemba 29, 2017 amewaagiza wafanyabiashara wa mbolea kote nchini walioweka mgomo wa kupeleka mbolea kwa wakulima kufikia 30 Disemba 2017 wawe wamefungua maghala yao kwa ajili ya kuwauzia mbolea wakulima.

Alisema endapo wafanyabiashara hao wasipofanya hivyo serikali itawanyang'anya leseni zao haraka iwezekanavyo ili kuruhusu wafanyabiashara wenye uwezo wa kufanya jukumu hilo pasina kuwaumiza wakulima kutokana na bei ghali ya mbolea.

Mhe Mwanjelwa ametoa agizo hilo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Morogoro alipotembelea Wakala wa mbegu za kilimo (Agricultural Seeds Agency-ASA) Mara Baada ya kubaini kuwa kuna wafanyabiashara ambao wameanza kufunga maghala kwa madai ya kupanda kwa mbolea katika soko la Dunia.

Alisema kuwa kufanya hivyo ni kinyume na sheria na kuijaribu serikali kwani malalamiko yao ya kupanda kwa bei katika soko la Dunia hayana tija kwani mbolea zote zilipo nchini tayari wakishanunua kipindi soko likiwa kwenye unafuu mkubwa.

Alisema kuwa serikali ilitoa bei elekezi katika mbolea ya kukuzia na kupandia ikifahamu fikra kuwa kupitia gharama hiyo wakulima watanufaika lakini pia wafanyabiashara watanufaika kutokana na faida wanayoipata lakini wameamua kubadili utaratibu wa kutaka kupata faida kubwa zaidi pasina kujali wakulima wataumizwa na bei hiyo kwa kiasi gani.

Mhe Mwanjelwa ameitaka kampuni ya Premium ambayo ni moja ya kampuni zilizogoma kufungua maghala na kupeleka mbolea kwa wakulima kwa bei elekezi iliyotolewa na serikali.

Alisema kuwa wafanyabiashara hao kwa makusudi wameamua kufifisha juhudi za Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli ya kuwakomboa wakulima kupitia gharama nafuu ya mbolea hivyo kufikia kesho wasipofungua maghala hayo watanyang'anywa leseni zao ikiwa ni pamoja na kuchukuliwa sheria.

Jumapili, 24 Desemba 2017

MHE MWANJELWA AWATAKA WAKUFUNZI WA VYUO VYA KILIMO NCHINI KUTOFANYA KAZI KWA MAZOEA

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua Kitalu Nyumba (Green House) katika ziara yake ya kikazi alipotembelea Chuo cha Kilimo Mtwara Kilichopo katika kijiji ch a Naliendele katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Mjini, Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha Kilimo Mtwara Ndg Elias L. Maijo, Juzi 22 Disemba 2017. Picha Zote Na Mathias Canal
 Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua mashamba mbalimbali ya uzalishaji wa mazao ya kilimo katika ziara yake ya kikazi alipotembelea Chuo cha Kilimo Mtwara Kilichopo katika kijiji cha Naliendele katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Mjini, Juzi 22 Disemba 2017.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akizungumza na Wakuu wa Idara na Wafanyakazi wa Chuo cha Kilimo (MATI) Mtwara Kilichopo katika kijiji cha Naliendele katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Mjini, Juzi 22 Disemba 2017.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo mara baada ya kukagua mashamba mbalimbali ya uzalishaji wa mazao ya kilimo katika ziara yake ya kikazi alipotembelea Chuo cha Kilimo Mtwara Kilichopo katika kijiji cha Naliendele katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Mjini, Juzi 22 Disemba 2017.

Na Mathias Canal, Mtwara

Wakufunzi wa Vyuo vya Kilimo kote nchini wametakiwa kutofanya kazi kwa mazoea badala yake kufanya kazi kwa Weledi, Ubunifu na Maarifa ili kuongeza tija katika majukumu yao ya kufundisha wanafunzi ambapo baadae wanazalisha wataalamu mbalimbali katika sekta ya Kilimo.

Kauli hiyo imetolewa juzi 22 Disemba 2017 na Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa wakati akizungumza na Wakuu wa Idara na Wafanyakazi wa Chuo cha Kilimo (MATI) Kilichopo katika kijiji cha Naliendele katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Mjini.

Alisema kuwa watendaji hao wanapaswa kuwa wabunifu katika nyanja mbalimbali zitakazowawezesha kuwa na kipato cha ziada kwa kufuata sheria, taratibu na kanuni.

Alisema kuwa kufanya hivyo kutawanufaisha kuwa na kipato kitakachowawezesha kuendesha chuo pasina kutegemea serikali kwa kina jambo ambalo litapunguza malalamiko dhidi ya serikali kufanya kila kitu.

Aidha, alisisitiza viongozi wa vyuo vyote vya Kilimo nchini kutumia vyombo mbalimbali vya Habari sambamba na mitandao ya kijamii ili kutangaza maudhui ya vyuo na kozi zinazofundishwa ili kurahisisha wanafunzi kupata wepesi katika uchaguzi wa vyuo vya kusoma.

Katika ziara hiyo Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa alitembelea na kujionea miundombinu ya Taasisi na kazi za mafunzo ikiwa ni pamoja na kuangalia shughuli za uzalishaji wa mazao mbalimbali.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Chuo cha Kilimo Mtwara Ndg Elias L. Maijo alimpongeza Naibu Waziri huyo wa Wizara ya Kilimo kwa kuaminiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli na hatimaye kuteuliwa kumsaidia katika majukumu yake ambapo pia ameahidi kutekeleza maelekezo yote yaliyotolewa.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMUAGIZA MRAJIS KUFANYA UCHUNGUZI SACCOS YA MADIBIRA-MBARALI NDANI YA SIKU 14

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya uli...